Obe
Platinum Member
- Dec 31, 2007
- 10,322
- 35,824
Tafasiri Unavyoweza: Swali na Masahihisho
Usije ukadhani kuwa kila swali lina hitaji majibu, usitegemee utakutana na hali ya jana kila siku maana jana na leo ni siku mbili tofauti na kwa kuwa ni mbili basi sahau kuona moja jumlisha moja u=inakuwa tatu na si mbili. Kwa kwa kuwa moja na na moja ni mbili na wala si tatu kwa kujumlisha basi hoja yangu ya kutafasiri inasema kuwa si kila swali linahitaji majibu, maswali mengine yanahitaji marekebisho na si majibu.
Unaweza kujiuliza kwanini pamoja na kuwepo kwa rasilimali chekwa kwenye taifa letu bado umaskini uliokithiri unatamalaki na kumea kama uaridi kwenye samadi. Hapa kujiuliza swali ukitegemea majibu ni kujidanganya na kujilisha upepo tu, swali unalojiuliza ni lazima ulirekebishe kwanza, lifanyie masahihisho ndo liwe swali vinginevyo linabaki kuwa ni maneno yenye kiulizo badala ya nukta.
Unajiuliza haki yangu iko wapi, unapoteza muda, haki huletewi kwenye sahani. Fuatilian na ndipo utagundua kuwa unapaswa kutafasiri unavyoweza kila ninachoandika na kila unachosoma maana asubuhi ninatafasiri vingine na mchana nikishiba tafasiri ya asubuhi inabadilika. Tumewaona wanaotaka tuwaombee ilihali hawataki kuwauliza tuwaombee juu ya nini na hapa ndo majibu kabla ya swali. Tafasiri unavyoweza