Makapuku Forum

Makapuku Forum

Sawa na msafiri asafiriye na asijue aendako basi sawa, sio lazima tutafsiri au sio mtaasisi?

Ha hahahahah
...kutotafasiri nako ni kutafasiri. Si wanasemaga kukaa kimya nalo ni jibu mhakamani uswahili wakaongeza lao eti kukaa kimya ni jibu la mjinga ha hahahahaha, waswahili bhana hawakosi kutofautisha shanga na shangaa, bangi na bangili
 
Muziki wa Mdhamini: Najidhamini kwa Ajili Yako

Unganeni tu na mimi, leo hadi mjue kuwa mimi leo nimedhamiria kikamilifu kumpongeza mama yenu ambaye huwa mnasomaga tule tumaandishi twangu tudogo kwenda kwake.

Huu muziki/wimbo anaupenda nami sitachoka kuucheza hapa tufurahi pamoja..

Naomba kujua ndio umeshakuwa baba yetu?
 
Muziki: Happy Birthday To You

Ujue nimeandika title kiinglishi na asikufiche mtu hakuna kazi ngumu kama kuanza kutengeneza sentensi kwa kiinglishi. Ni ngumu si kidogo maana kwa sisi tuliosoma shule ambazo kengele ilikuwa ni ringi la tairi la roli tunajuana kabisa kuwa kiingereza chetu kuna mahali hakiko sawa. Na ndiyo maana huwa tunasalimiana kiinglishi na baada ya salamu tu hatuendelei na kizungu, tunarudi mstarini kuhesabu namba labda uwe umechelewa ndo utapewa lile likibao la Swahili speaker. Nakusalimia kapuku mheshimika.

Nilikuwa na wakati mzuri leo na nilichofanya yote niliyotaka kutafanya bila shida asante kwako wewe ambaye hujauliza siku yangu ilikuwaje. Nilikuwa na anko wangu huyu mnayemfahamu tukipanga mipango yangu halali na yake haramu maana unawezaje kupanga kwenda kula kitimoto bila bia. Halali huenda na halali na kamwe haramu haiendi na halali, fanya unachoona ni sahihi kwako, mambo ya halali au haramu subiri siku ya hukumu, wewe ni nani hata useme halali na haramu kwa kila mtu. Toto baya zuri kwa mama yake.

Muziki sasa, jana ilikuwa ni tarehe ya kuzaliwa BlessedHope , niliimiss ila sio kwa makusudi maana mjomba aliniambia tusimsumbue kwa sababu BH yuko kwenye siku yake, nikatulia na ninaamini hata wengi tumeona leo. Tunakupenda BH na Heko ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa

Safi sana mtaasisi
 
Naomba kujua ndio umeshakuwa baba yetu?
b62ec2b0-f680-0132-44ed-0a2ca390b447.gif
 
....neno gani tena jingine, huoni maneno yameandikwa kwa herufi kubwa kuonesha msisitizo. Mtaasisi kusoma hujui hata picha nayo unageuza miguu juu kichwa chini
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ha hahahahah
...kutotafasiri nako ni kutafasiri. Si wanasemaga kukaa kimya nalo ni jibu mhakamani uswahili wakaongeza lao eti kukaa kimya ni jibu la mjinga ha hahahahaha, waswahili bhana hawakosi kutofautisha shanga na shangaa, bangi na bangili
Kiroho safi
e9bb7f91ebd5d944313b453e28391d03.jpg
 
[emoji524]TUOMBE
Mungu wetu na Baba yetu Asante kwa Neema yako kutupa siku hii ya leo TAREHE 28 FEBRUARI 2018 Ni Furaha yetu kuona Unazidi kuachilia Neema yako ya Uzima. Tumenyenyekea mbele zako Mungu kuonesha utii wetu kwako. Tunaomba Baraka zako,futa majonzi,masikitiko kwa kila Moyo ulio-kata tamaa na kuachilia Furaha na Pendo litokalo kwako. Kutana na haja za mioyo yetu na kuzidi kutufundisha Kweli yako, Bariki kutoka na kuingia kwetu. Mikono yetu ikakuzalie matunda yadumuyo. Fungua Uchumi wetu,asiye na kazi apate kazi. Mungu wakumbuke wagonjwa na wengine wote wanaotafuta kukuona, wakutane na uso wako. Mioyo yetu ikutukuze wewe sasa na hata milele AMINA.

SIKU NJEMA,JUMATANO YA BARAKA
 
[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji258][emoji253][emoji253][emoji253][emoji253] nimemkumbuka mukongo mm jaman angekuwepo kutoa mauwa binamu Mungu anakuona kwa kunipotezea mukongo wa mama
Mwee mwanangu wewe
 
Back
Top Bottom