Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Teknolojia Si Kila Kitu

Tunafanikisha mengi kwa sababu tu ipo teknolojia inayosaidia kufanikisha haya, hali ya hewa kwa mfano, utajua nini kitatokea wiki ijayo. Mawasiliano fikiria, ingekuwa vip bila simu na internet, hivi vimetuwezesha kuwasiliana na ndugu na marafiki zetu katika dunia hii iliyotawanyika. Hospital ndo usiseme, teknolojia inafanya mambo ambayo zamani isingekuwa rahisi kuwezekana. Pamoja na yote, kuna nguvu ya mtu (human touch) inayoishinda teknolojia, tafasiri unavyoweza.

Imekuwa ni kawaida sana, kwa wanafunzi kwa mfano, wengi wao wanaamini kuwa internet itawafanyia kila kitu, na kweli inawasaidia kufaulu mitihani yao. Graphs wanaingiza maswali inachorwa ndani ya dakika. Muda wa kukaa maktaba na maabara hawana tena, muda wa kupekua vitabu haupo kwa kuwa tu teknolojia imewaletea unafuu na kurahisisha maisha ya shule. Na kikubwa zaidi kwa sababu wamekuwa hawatumii muda wao kujisomea basi teknolojia inawawezesha kubet.

Ukweli usemwe, teknolojia haijamaliza kila kitu, maarifa yapo ukiutumia ubongo wako kikamilifu, wengi hatuupi kazi ubongo, ndiyo mimi na wewe kwa sababu tu teknolojia ipo. Tumia muda kujisomea na kusaka maarifa zaidi na hapo ndo utaona teknolojia unaihitaji na pia unamuhitaji mtu halisi katika kurahisisha maisha yako hapa duniani. Tafasiri unavyoweza.

 
Unajisikia raha sana mimi nikinuniwa na aunt yako ...ujue ile list ya wabaya wangu bado ninayo na wewe ntakuweka uwe mdhamini ....

Mwenye mwanya aliniomba nimsindikize kule juu eti sijui kuna rafiki yake kamuazima dela na uzuri ndo njia ya kwenda kule

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Shukrani binamu..unalifanya jukwaa kuwa la kipekee

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Toa hiyo signature basi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…