Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Kelele za Ukimya

...mwanaharakati maarufu wa haki za watu weusi huko USA, MLK Jr anasheherekewa leo na wao wanapumzika. Ni vizuri kuwaenzi watu waliotoa mchango katika kubadilisha mtizamo wa jamii kuhusu masuala tofauti ikiwemo suala la elimu, mahusiano, jinsia, uongozi, na kadhalika.

Ukimya unaweza ukatafasiriwa tofauti baina ya mtu na mtu, na ndiyo maana napata nguvu ya kuandika ukimywa wenye kelele katika koramu hii ambayo najihisi kuanza kuipenda kuiandika kila ninapopata nafasi. Si tuko mwanzo kabisa wa mwaka mpya, bado nguvu ya kufanya ulichonuia unakuwa nayo hadi mwezi wa tatu ambapo kila kitu kinabaki kama kilivyokuwa mwishoni mwa mwaka jana na juzi.

Waswahili wana msemo kukaa kimya ni jibu la mjinga na ukimywa wa kondoo una kelele nyingi akiamua kuuhamishia kwenye ubongo wake. Hapo utapambana na kichwa kigumu kilichoamua kuuambia mdomo ukae kimya ili pembe zifanye kazi.
Kukaa kimya sio kushindwa kuongea, unaweza kuwasilisha 'kelel' zako kwa namna tofauti kabisa ambayo kina Luther na Gandhi waliitumia kuleta mabadiliko katika jamii na kupambana na udhalimu uliokuwa ukizidisha matabaka katika jamii zao.
Tafasiri unavyoweza, huo uhuru nakuachia wewe maana mimi ninatafasiri ukimya kwa namna yangu na tukitofautiana ndiyo tutakapoelewana kwa makelele ya ukimya



martin-luther-king-quotes-15.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom