Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafsiri Unavyoweza: Tunza Mazingira

...nakumbuka kati ya masomo niliyokuwa nayaweza sana (sio kufaulu, ila kuhudhuria dakika zote class) mojawapo ilikuwa ni Jiografia, jingine lilikuwa ni somo la lugha ya Kiswahili. Hili nililipenda sema lenyewe halikunipenda kwa kuwa wenzangu wote na mimi tulikuwa tukifundishwa darasani, sisi nje tunaongea kilugha chetu. Ningeweza kufaulu sana na kufika mbali kama masomo yote yangefundishwa kwa kilugha changu ambacho nilikuwa nakimaster kama nyani porini.

Turudi kwenye mada ya kutafsiri unavyoweza, Jiografia, ilivutia kusoma. Mambo ya hali ya hewa, longityudo na latityudo, mito, maziwa, milima na mabonde, misitu na nyika, uoto wa asili na miamba. Nilipenda sana kwa kweli. Ilifikia hata tukaenda 'utalii' Serengeti na Ngorongoro-nilipiga picha lakini mkanda uliungua, hazikuwa zama za smartphone na dijital kamera. zilikuwa ni enzi za kwachaaa mara flashi myakaa kutahamaki umefumba macho na haina kudelete.

Mazingira yanabadilika sana, na hasa mabadiliko ya tabia nchi, mvua zinanyesha, mafuriko na joto linaongezeka. Nina hakika kuna maeneo mengi unayoyajua kuwa na msitu sasa yamekuwa jangwa. Hii pamoja na mambo mengine ya kijiografia yasipoangaliwa vizuri si salama kwa kizazi kijacho.

Tunapoharibu mazingira, tunaweza tusione matokeo yake leo lakini kwa kizazi kijacho kitahangaika na wakigundua ni sisi ndo tumewafanya waishi kwa ugumu basi watatembelea kaburi la kila mmoja, watalifukua na kuanza kuchapa viboko mifupa. labda tubadilike tuanze kuchomana moto tukifa, na kusubiria moto mwingine wa milele kama utabahatika kuukwepa. Tafasiri unavyoweza, nimekuandikia utunze mazingira, ukiyatunza yatakutunza, siuongo!

envrnmnt.jpg
 
...lift tena, kwani nimesema najua kuendesha? Hapa sasa hivi ndo natafuta material nisome namna ya kujifunza kuendesha bodaboda. Baadaye kama una material ya namna ya kuomba lift nielekeze nije kuchukua
Kuendesha utajua tu washa pikpik ikiwaka nyoosha nayo
 
Tafsiri Unavyoweza: Tunza Mazingira

...nakumbuka kati ya masomo niliyokuwa nayaweza sana (sio kufaulu, ila kuhudhuria dakika zote class) mojawapo ilikuwa ni Jiografia, jingine lilikuwa ni somo la lugha ya Kiswahili. Hili nililipenda sema lenyewe halikunipenda kwa kuwa wenzangu wote na mimi tulikuwa tukifundishwa darasani, sisi nje tunaongea kilugha chetu. Ningeweza kufaulu sana na kufika mbali kama masomo yote yangefundishwa kwa kilugha changu ambacho nilikuwa nakimaster kama nyani porini.

Turudi kwenye mada ya kutafsiri unavyoweza, Jiografia, ilivutia kusoma. Mambo ya hali ya hewa, longityudo na latityudo, mito, maziwa, milima na mabonde, misitu na nyika, uoto wa asili na miamba. Nilipenda sana kwa kweli. Ilifikia hata tukaenda 'utalii' Serengeti na Ngorongoro-nilipiga picha lakini mkanda uliungua, hazikuwa zama za smartphone na dijital kamera. zilikuwa ni enzi za kwachaaa mara flashi myakaa kutahamaki umefumba macho na haina kudelete.

Mazingira yanabadilika sana, na hasa mabadiliko ya tabia nchi, mvua zinanyesha, mafuriko na joto linaongezeka. Nina hakika kuna maeneo mengi unayoyajua kuwa na msitu sasa yamekuwa jangwa. Hii pamoja na mambo mengine ya kijiografia yasipoangaliwa vizuri si salama kwa kizazi kijacho.

Tunapoharibu mazingira, tunaweza tusione matokeo yake leo lakini kwa kizazi kijacho kitahangaika na wakigundua ni sisi ndo tumewafanya waishi kwa ugumu basi watatembelea kaburi la kila mmoja, watalifukua na kuanza kuchapa viboko mifupa. labda tubadilike tuanze kuchomana moto tukifa, na kusubiria moto mwingine wa milele kama utabahatika kuukwepa. Tafasiri unavyoweza, nimekuandikia utunze mazingira, ukiyatunza yatakutunza, siuongo!

envrnmnt.jpg
Asanteee
 
Muziki: Hasira Dawa Maji

...tunashauriwa kunywa maji mara nyingi iwezekanavyo! Maji ni dawa, huhitaji kuwa dakitari kulijua hili na ndiyo maana nyumbani tunahakikisha hatukosi maji kwa namna yoyote ile, tena masafi. Nikusalimie kapuku mheshimika na kama ukitaka kujua hali yangu mimi sijambo na siku yangu ilikuwa poa, mchana wote. Sijui wewe siku yako ilikuwaje.

Maji ni uhai, maji ni usafi, maji ni tiba. Unapokunywa maji unajihakikishia mengi mazuri kuanzia uzima wa macho hadi ngozi. Ni vizuri ukaninukuu sahihi kuwa naandika haya bila kuwa na taaluma au weledi wowote wa udaktari. Kuwa na afya njema sihitaji dokta aniambia, naamka najiangali tu. Nikijiangalia naona vyombo viko timamu, halafu naenda maliwatoni hapo simuhitaji dokata aniambie kitu. Hawa madokta nao wana mbwembwe sana, yaani wamekuwa kama mafundi makenika, majuzi nimeenda kutoa jino, dokta (dentist) namwambia jino hili linaniuma, kaingiza x-ray na maskana kibao. majibu kanionesha meno manne yanayohitaji tiba. Nikajiangalia mfukoni maana sina bima, nikamkazia macho 'dokta hili ndo linaniuma haya mengine siku nyingine'. Akasema haya hakuna noma, mwisho wa siku nyama utaomba zitengenezwe uji.

Muziki sasa, kunywa maji yanasaidia sana na hili mimi ni shahidi. Nilikuwa nimekasirika nilipokunywa maji nikaenda kuoga nikagundua hasira zangu hazina faida zaidi ya kunijengea maumivu na kunikondesha tu. Nakupenda Kapuku na uwepo wako hapa unaniongezea mengi.

Binamu asante sana umenikumbusha nilivyokua mdogo naangalia movie ya neria alivyonyanyasika bada ya mumewe kufariki
 
...ukweli ni huu, hii movie huwa sichoki kuiangalia tangu niko tunaiangalia family nzima tumekaa tunaiangalia. ilitufundisha na inanifundisha kila ninapoitizama.

Ulishaiona na ile Yellow card
 
Hiyo movie ya neria ni zaidi ya mafundisho yellow cad niliangalia ya ukimwi binamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom