Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Hesabu Saa, Miaka Itakuchosha

...ni muda umepita Kapuku mwenzangu na leo ni Jumamosi ya mwisho kwa mwaka 2017, kuna mengi ya kutakari siku hii ambayo naamini kabisa umejipumzisha. Bado likizo inaendelea kwa wengi wetu, eeeh, likizo naamaanisha ya kazi, shule na vitu kama hivyo maana kuna mambo mengine hayana likizo hata uwe mjanja mjanja namna gani. Ukiyapa likizo tu, imekula kwako. Utakuja unalia sisi unatukuta tunatoa machozi.

Muziki sasa, Jumamosi maneno kidogo tu na muziki unafuata. Video hizi zilibamba sana hapa kwenye kipengele cha muziki. Furahia leo ni wikend ya mwisho 2017

Asante Obe Mungu akubariki asante
 
TUOMBE
Mwenyezi Mungu Mtakatifu, Mfalme wa wafalme,Baba wa Milele,Mshauri wa Ajabu,Mungu mwenye Nguvu Asante kwa kutufikisha siku hii ya leo ya mwisho wa mwaka JUMAPILI,31 DESEMBA 2017 salama wako wengi walitamani kuiona siku ya leo hawajaweza sisi ni nani Baba Mtakatifu
Tunakushukuru kwa sababu Upendo wako ni mkuu kwetu, Kwa sababu unatulinda na kutuongoza, Kwa sababu unatupigania, Kwa sababu Unaweza yote,Unajua yote,Upo kila mahali. Mungu wetu tunaomba usinyamaze kila tukuitapo sisi peke yetu hatuwezi.
Tupiganie katika kila Jambo,Tufundishe,tushauri na kuturudi tunapokukosea. Mungu bariki Afya,Kazi,kusudi,Uchumi na Imani zetu.
Waponye wagonjwa wote Baba majumbani na mahospitalini,
fariji wafiwa wote wape faraja yako popote walipo,angalia wajane,wagane,
yatima Baba wape hitaji la mioyo yao,wasaidie wote wanaopitia changamoto mbalimbali.
Wasaidie wasafiri wote kokote waendako majini,nchi kavu na angani waende na kurudi salama..ponya mioyo yote inayotaabika kwa huzuni ,taabu na dhiki ,matesi tuongezee imani Baba tukuangalie wewe tu maana wewe Baba hukawii wala huwahi jibu lako ni ndiyo.Roho Mtakatifu kaa nasi siku zote za maisha yetu.
Ni katika Jina la Yesu tunaomba tukiamini na kushukuru Amina.

JUMAPILI NJEMA,MUNGU AONEKANE KWETU KATIKA IBADA ZOTE SIKU NJEMA MBARIKIWE.
 
Nimewamiss mawifi,mashemeji bila kumsahau ankoo zaidi ya yote baby buu wangu jamani lyon leewherever you are ABJ kakumis mno ee babaau ushapata mwingine babaangu??
 
*MAOMBI YA KUFUNGIA MWAKA 2017*

*Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu.

Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi.

Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru.

Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza.

Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu.

Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

"Ebu funga mwaka kwa kufungua milango ya kusamehe tena anza sasa na anza na wewe, mwaka 2018 Uwe na kusamehe zaidi"

```Ujumbe huu muhimu na umfikie kila mmoja wetu katika familia yake, na tuutafakari kwa kina Kama nilivyofanya Mimi..

*Nikutakie Mwaka wa mafanikio na Amani binafsi, be blessed*
 
Mom
Asante mnoo jamani... Nimebarikiwa mnoo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom