Makapuku Forum

Makapuku Forum

MAOMBI
Yesu Tunakushukuru kukubali kuzaliwa ndani ya Mioyo yetu. Kwa ajili yako tumefika hadi siku hii ya leo. Karibu ndani ya Mioyo yetu wewe uliye mkombozi wa ulimwengu, mshauri wa Ajabu,Baba wa Milele na mfalme wa Amani. Utulinde na kutuongoza ili vitu vipya vya Kiroho vizaliwe maishani mwetu tuishi sawa sawa na kusudi lako. Ni katika Jina lako Yesu tunaomba Amina.
 
Family, niwakati mwingine tena wa kumshuru Mungu kwa siku hii ya pekee na yenye maajabu yake pia,
Ikiwa ni jumapili nzuri ya kwenda makanisani kumrudushia sifa na shukrani Mungu wako basi nawasalimu..
tumsifu yesu kristu!
Bwana yesu asifiwe!
Mapendo mapendo!
Majeshi majeshi!
Utukufu kwa Bwana Yesu!
Kuweni na jumapili njema ndugu zangu!
Amena asante nawe tena ubarikiwe
 
6 *Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia*,

Luka 2 :6

7 *akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.*

Luka 2 :7

8 * *Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku*.

Luka 2 :8

9 *Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.*

Luka 2 :9

10 *Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;*

Luka 2 :10

11 *maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.*

Luka 2 :11
Asante kwa neno la Noel mama mchungaji
 
MAOMBI
Yesu Tunakushukuru kukubali kuzaliwa ndani ya Mioyo yetu. Kwa ajili yako tumefika hadi siku hii ya leo. Karibu ndani ya Mioyo yetu wewe uliye mkombozi wa ulimwengu, mshauri wa Ajabu,Baba wa Milele na mfalme wa Amani. Utulinde na kutuongoza ili vitu vipya vya Kiroho vizaliwe maishani mwetu tuishi sawa sawa na kusudi lako. Ni katika Jina lako Yesu tunaomba Amina.
Amen
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom