BlessedHope
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 7,988
- 32,649
ZABURI 121
1.Nitayainua macho yangu,msaada wangu utatoka wapi.
2.Msaada wangu ni katika Bwana aliyezifanya mbingu na nchi.
3.Asiuache mguu wako usogezwe;asinzie akulindaye
4.Naam ,hatasinzia wala hatalala usingizi,Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5.BWANA ndiye mlinzi wako,BWANA ndiye mlinzi wako BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6.Jua halitakupiga mchana ,wala mwezi wakati wa usiku.
7.BWANA atakulinda na mabaya yote Atakulinda nafsi yako .
8.BWANA atakulinda utokapo na uingiapo Tangu sasa na hata milele.
USIKU MWEMA WAPENDWA.. DAMU YA YESU ITUFUNIKE..
Nawe pia ubarikiweAsante BH kwa maombi na baraka za usiku. Usiku mwema kwako
Asante ObeUsiku mwema Makapuku
The return!pamoja
Asante kaka Obe.Muziki: Ni Likizo, Toa Zawadi
Niko kwenye utalii wa ndani, yeah, mambo ya likizo haya, natalii tu na kuona navyomiss kuviona nikiwa mjini. Si mnajua ninakaa mjini mimi, na nikisema mjini simaanishi Dar maana kuna watu wanadhani Dar yote ni mjini, tembea uone, kuna mitaa Dar hawajawahi kuona gari, na hawajui kama chipsi ni viazi, usiniulize ni wapi utanichosha niko likizo. Ukiondoa hii hali ya mvua lakini ninafaidi mengi sana likizo hii yanayonijenga kiimani, kimwili na kiakili. Nakutana na mazingira halisi na sio feki na hata maisha yangu fake ninayoishi mjini nimeyaacha niliposhuka hapa kijijini. Huku ni uhalisia na sio hisia, kuna tofauti.
Kama ujuavyo kipengele hiki huwa ni kukumbushana na kusogoa kidogo juu ya maisha na hasa maisha yangu ambayo kama yalivyo yako yametawaliwa na vitu hivi, elimu, biashara, teknolojia na mahusiano na utani sijauweka kando. Sasa basi hebu niandike nilichonuaia leo. Likizo ni muhimu, shitaji kukukumbusha hili na kwa wote tunaosafri kuja likizo hata kwa wasiosafir ni vizuri kutoa zawadi, maana kuna vingi tunavyo na hata kama hatuna unaweza kununua vichache ukawazawadie likizoni. Kwanini, likizo ndo muda ambao uanenda kukutana na marafiki ambao waliamua kufanya maisha yao hapo hapo ulipoondoka, wengi ulisoma nao msingi, ukaenda nao sunday school au chuo (madrasa) na zaidi mkaenda kuogelea bwawani pamoja, siongelei jando hapa maana kila mmoja ana kabila lake.
Muziki sasa, likizo itumie vizuri kwa kuwa na muda zaidi wa familia, mazoezi kwa sana maana ni mwendo wa kula na kunywa tu na siku mbili hizi nakaona kakitambi kananijongea kiasi kwamba kujichungulia hadi nijiinamishe nyuzi 45. Likizo njema Kapuku mwenzangu shululu , Tumosa , Transcend , SHIMBA YA BUYENZE , BlessedHope , Shunie , makaveli10 , Lyon Lee , Sakayo , Nyagei , Gentries , dumejeuri , Mndali ndanyelakakomu , mzeewakungoa , moudgulf , husna muba , Werrason , Mussolin5 , Bitoz , Jimena , Mkushi wa kusi , na wewe ambaye hujaenda likizo
Thank you mom.TUOMBE Baba katika jina la Yesu Kristo ni siku mpya kabisa ya ALHAMIS NJEMA BABA UMETUAMSHA TENA SALAMA Tunasema Asante Baba Sifa Shukurani Heshima Utukufu ni kwako peke yako wewe uliye Alfa na Omega Wapo wengi walitamani kuiona leo Baba hawajaweza sisi ni nani Baba ?Hakika TUNAKUSHUKURU tunakuomba Utusamehe Dhambi zetu tulizofanya kwa Mawazo na Maneno na Matendo ,kwakujua na kutojua ,Tushike Mwenendo Mpya
Baba wasamehe na uwabariki wote walioko majumbani kwetu waume zetu ,wake zetu ,watoto wetu, ndugu ,jamaa ,marafiki zetu na wasaidizi wetu siku zote wakutafute wewe
Ponya ndoa zetu Baba
Ponya Familia zetu
Tunaomba ponya Wagonjwa bariki dawa wanazokunywa na wote wanaowahudumia wawahudumie kwa Upendo
Walinde Wasafiri wote wa Nchi kavu Majini na Angani Bwana Yesu awe dereva wa kila chombo na pia Damu ya Bwana Yesu iwafunike
Wafariji Wafiwa Watie moyo Wajane, Wagane, Yatima , Walioachwa, Waliotelekezwa, Wasio na Makazi, Wafungwa, Wakukimbilie wewe Mfalme wa Amani
Baba Bariki Uchumi wetu ukakue kazi za Mikono yetu Ajira Ujasiriamali Biashara Mashamba Bariki Masomo ya kila mmoja Baba ukaonekane kwetu Mungu wetu
Epusha migogoro, magomvi, chuki, dharau, mikosi, balaa zote, ukatukinge na pepo wachafu
Tutakase Baba tunayo mahitaji mengi na kila moja unalifahamu Tunaomba Uonekane katika kila eneo
Asante kwa sababu utatupatia sawa na Mapenzi yako.
TUNAOMBA,TUNASHUKURU TUNAAMINI KATIKA JINA LA YESU AMEN.
SHALOM Muwe na siku njema Mbarikiwe
Salaam mkuu obeAmen mtumishi. Uwe na usiku mwema nawe pia
Salaam makaveliTubarikiwe sote.
Salaam kiongoziAsante ubarikiwe
Nakusalim shunieAmeen mama mama hiyo salaam ya kumsalimia anayetumia jina la binamu umetoa kwa roho moja eenh
SalaamSalaam kiongozi
Sijambo moud za weweNakusalim shunie
Ameen MamaKitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
Yoshua 1 :8
Asante mkuu na kwako pia karibu sanaShunie
husna muba
Sakayo
Blessed Hope
Nyagei
Transcend
Lyon Lee
Obe
makaveli10
shululu
SHIMBA YA BUYENZE
moudgulf
mndali ndanyelakokumu
Nawasalimia kwa jina la Aliye Tuumba
Atuwezeshe kuuona mwaka mpya na Christmass.
Shemela za jioniSijambo moud za wewe