Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Tuwe na Wiki Njema

....siandiki mengi lengo ikiwa ni kukutakia usiku mwema na kukuwish a great week. Ujue kila wakati nakueleza kuwa wewe ni mtu mzuri na unalifanya Jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Unaweza kuona nimekuja usiku sana lakini tambua kuwa JF ni kama unaangalia masaa ya dunia, kwingine ndo kwanza leo ni Jumatatu. Tuwe na wiki nzuri yenye tabasamu na mafanikio

 
Muziki: Tuwe na Wiki Njema

....siandiki mengi lengo ikiwa ni kukutakia usiku mwema na kukuwish a great week. Ujue kila wakati nakueleza kuwa wewe ni mtu mzuri na unalifanya Jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Unaweza kuona nimekuja usiku sana lakini tambua kuwa JF ni kama unaangalia masaa ya dunia, kwingine ndo kwanza leo ni Jumatatu. Tuwe na wiki nzuri yenye tabasamu na mafanikio


Asante Obe Mungu akubariki sana
 
TUOMBE

Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Baba Mungu mwema usiyeshindwa na lolote Mfalme wa Amani
Tunakushukuru Mungu muweza wa yote kwa kutufikisha siku hii ya leo JUMATATU ,11 2017 Salama tukiwa wazima na afya njema wako waliotamani kufika leo hawajaweza sisi ni nani Baba Mwema asante asante asante Baba.

Asante kwa Ajili ya Afya,Ulinzi, Nguvu na vyote ulivyotukirimia.
Asante kwa yote unayotutendea na tunaomba toba pale ambapo hatukuenenda sawa na mapenzi yako kwa mawazo,maneno, matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali uturehemu Baba twakusihi.

Tunaomba utulinde mchana huu wa leo na wiki nzima uwe kiongozi wetu tulipo uwepo Baba.

Bariki kutoka na kuingia kwetu. Tupe leo mkate wa kila siku. Juma hili lote uwe kiongozi wetu.Tutakase kwa Damu Takatifu ya Yesu Kristo,Sema Neno tupone maana wewe ni Uzima wetu,Jawabu la Maisha yetu latoka kwako,achilia Bidii,Utii,Nidhamu, Upole,kiasi, Upendo na Uvumilivu pale tunapo kwazwa
Tufundishe kupenda zaidi,kujali zaidi,kuthamini zaidi, kuchukuliana mizigo ya wengine kwa Upendo.

Wabariki wasafiri majini ,nchi kavu na angani waende na kurudi salama.
Ponya wagonjwa wote majumbani na mahospitalini,watie nguvu wote wanaopitia changamoto mbalimbali,wafariji wafiwa ,wajane,wagane yatima na Baba bariki kazi za mikono yetu.Wabariki wanafunzi wote walioko mashuleni waongoze katika mitihani yao yote wape kushinda Mfalme wa Amani na uwape mafanikio na kukutii wewe,wape afya ya mwili na roho pia.Gusa kila mmoja wetu Baba mpe haja ya moyo wake na mapenzi yako yatimizwe..Roho Mtakatifu kaa nasi tuongoze
Ni katika Jina la Yesu Kristo tunaomba tukiamini na kushukuru Amina.

SIKU NA WIKI NJEMA WAPENDWA MBARIKIWE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom