Makapuku Forum

Makapuku Forum

KWA UNAYESIKIA UMEVUNJIKA MOYO,KWA USIKIAE KUWA NA MZIGO MZITO KWA MAPITO YAKO YALIYOSABABISHWA LABDA NA UNYANYASAJI FULANI,YAKABIDHI KWA MUNGU MKUU UPATE SULUHU LA KUDUMU;

YAKABIDHI HAYO KWA KRISTO YESU AKUSAIDIE;
Mathayo 11:28.
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

MTAFUTE MUNGU,
Zaburi 34:4-5.
4 Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
5 Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya.

MTWIKE YEYE FADHAA ZAKO ZOTE(YAKUSUMBUAYO);
1 Petro 5:7
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

MTEGEMEE MUNGU PEKEE(MUNGU WA AMANI);

Isaya 26:3-4.
3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.

USIZITEGEMEE AKILI ZAKO;

Mithali 3:5-6.
5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

MTUMAINI MUNGU;
Zaburi 42:11.
11 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.


UBARIKIWE,
Shalom.
 
Kwa Makapuku wote
351.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom