Makapuku Forum

Makapuku Forum

...ni shida ndiyo lakini kama nakumbuka sawasawa, kuna chanjo unachanjwa ukiwa mtoto au hata ukiwa na umri ulionao wanakuchanja na kuna baadhi ya nchi huwezi kuingia kama hujachanjwa hii na kama huna rekodi basi wanakuchanja. Itakuwa ni ajabu sana kama Tanzania wanaruhusu mgeni kuingia bila kuwa na kadi inayoonesha alichanjwa si tu hii ya ini bali na mengine pia.

Kuhusu tiba- virusi wengi hawatibiki wanazuilika na hata hawa wanazuilika na wanadhoofishwa kabisa, makala imehemuka kidogo na kuonesha kuwa hakuna tiba, ipo, halafu hivi kondomu tutatumia kwenye mambo mangapi? yaani badala ya kufanya kwa starehe unakuwa na mawazo ya ajabuajabu tu na si ajabu mikojo inakuwa kidoooooogo.

Kama ulitegemea nitaandika kama mtaalamu sahau, mimi nami nimejisomea tu
Ahahahhah binamu wewe ila mbona nasikia chanjo yako ipo lakini ipo juu sana
 
Muziki: Utambulisho

...eeeh, kaa (sio mdudu, au kuweka makalio chini) ukijua kabisa kuwa kuna tofauti ya utambulisho hauhusiani na ugeni au kutojulikana. Suala la msingi ni wewe unataka utambulishweje, wengine tunawajua na tunawatambua kwa namna walivyo na tukichoka kuwatambulisha tunawawekea na lebo kama zile za bei, wanauzwa. Najiaminisha kwako wewe kapuku mheshimika kuwa wewe unajitambua kama Kapuku na kaa ukijua ukapuku sio ule tunaoufasiri mitaani, sisi ni zaidi ya hao na ndo maana tuko humu tukiwa na kila na aina ya ukapuku wa utajiri. Utaitafuta maana siku nyingine kwa wakati wako.

Sijaingia hapa kutambulisha mtu au kitu ila nimeingia hapa nikiwa na nia moja tu ya kukuchangamotisha (challenge +motivation) kuwa ni vizuri kujitambua kabla hujatambulishwa. Ukifanyiwa utambulisho, anayekutambulisha anaweza akakosea asikuseme wewe, kama ilivyotokea kwa anko wangu pale alipomruhusu mume wa mjumbe amtambulishe, kumbuka huyu muwe alikuwa na bifu ya kuchukuliwa mke na anko wangu sasa utambulisho ukawa ni kuvuana nguo wakati anko alikuwa kapiga suti kama diwani mpya.
Muziki sasa, jitambue binafsi na wengine wote tutakutambua bila kukuwekea kitambulisho, kama wewe ni mwalimu basi kuwa mwalimu kweli, kama ni askari fanya yanayostahili kufanywa, na ukiwa mkulima basi baki kuwa mkulima na sio mshamba. Na kama wewe unafanya mazuri ongeza, ukiwa unafanya mabaya, zidisha lakini kaa ukijua hutakiwi kutambulishwa na mwingine wakati una uwezo wa kujitambulisha mwenyewe. Nakupenda Kapuku na unalijua hilo.

Dj Obe Asante
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom