Makapuku Forum

Makapuku Forum

MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 37

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp



Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"kivipi"
"sasa mitego yote hio mungu wangu"
"kwa mwanamke mwenye akili, asingeweza kusubutu kufanya ujinga kama huo... Tena akikumbuka alikuwa kipofu na leo kaona kwa ajili ya huyu mwanaume, yaani asingetakiwa kufanya hivyo alitakiwa akumbuke alikuwaje... Lakini ndio hivyo bwana"
"kwahio wewe ulikuwa muuza viazi"
"kabisa.. Ili nisije kupendwa kwa ajili ya pesa zangu... Na unakumbuka siku ile nilikuja kwao nikakukuta"
"eeeeee siku ile ndio naikumbuka"
"nilikuja kumpa mama ukweli wa mtoto wake, lakini mama akatikisa kichwa kuwa nisiseme mbele yako ili mtoto wake asikose bara na pwani... Nyumba ile walikuwa wanadaiwa kodi chungu nzima.. Lakini nikapambana mpaka nikainunua kabisa.. Ebu angali ni jinsi gani roho isiniume saidi.. Lakini moyo wangu ulitulia baada ya kusikia ni wewe ndio unaoa.. Nikaona hakuna shida yote maisha tu"
Sasa katikati ya maongezi yao ghafla simu ya sheby ikaita, kuangalia namba ilikuwa ni ile ya mke wake...
"haloo, jamani nipo bize jamani naombeni dakika chache"
Aliongea sheby huku akipiga meza kwa hasira
"samahani baba... Mkeo analeta fujo huku hataki watoto wake"
"hataki watoto wake... Kwanini asiwatake.. Au kawa chizi"
"hapana.... Hawataki kwasababu watoto hao hawako sawa"
Sheby alishangaa kuskia watoto hao hawako sawa
"watoto hawako sawa kivipi dokta?"
Sheby aliuliza huku akiwa mpole kwa kusubiri majibu toka kwa dokta huyo

ENDxxxELEA......

Unajua wahenga walisema kuwa, hesabu ni mbinguni na malipo ni hapa hapa duniani... Wengine walisema kabla hujafa hujaumbika... Nami nikasema usitukane mamba kabla hujavuka mto... Kijana sheby akiwa ofisini kwake wanapiga story za hapa na pale na rafiki au mfanyakazi wake aitwae saidi, ghafla simu yake inaita na kuipokea bila kusita,... Kijana alipokea taarifa tofauti na alizotarajia katika maskio yake,...
"watoto hawako sawa kivipi dokta"
Sheby aliuliza baada ya kuambiwa kuwa watoto hawako sawa

Wakati huo hata saidi pia alikuwa skio juu ili kuweza kuskia umbea huo
"kiukweli mi naona ungekuja tu hospitali, mana havielezeki kabisa"
"ok nakuja sasa hivi.. Ni wodi namba ngapi"
"njoo huku leba.. Utaelekezwa alipo mkeo"
Sheby alikata simu ghafla na kukusanya baadhi ya vitu vyake hapo ofisini kisha huyo akawa anaondoka bila hata ya kuaga,...
"boss kwani kuna nini"
"hakuna kitu"
Unajua siku zote kijana huyu hua hapendi mambo yake ya ndani kujulikana,
"basi wacha nikupeleke mana hii spidi utakuja kupata ajali boss"
Sheby aliona sio mbaya kama ataenda nae,... Basi saidi alikuwa dereva kwenye gari ya boss wake,...
"kwani dokta kasema watoto wakoje"
"hajaniambia, na kasema nifike nijionee hivyo sijui alimaanisha nini"
"aahhhh itakuwa ni sapraise hio... Lazima kuna kitu kizuri boss"
Ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni mama yake..
"haloo mamy"
"eeehhh ivi una habari gani wewe"
"habari???.... Kwani kuna habari gani"
"mkeo kajifungua kituko kule hospitalini"
"kituko ni kitu gani mama... Mbona mnanichanganya sasa"
"upo wapi"
"ndio naelekea huko sasa hivi"
"hebu wahi utanikuta hapa... Nipo na baba yake baba yako pia yupo hapa"
Mama sheby aliongea hivyo kisha akakata simu, sheby alizidi kuogopa kila anaposikia habari hizo....

Dakika chache wakawa wameshafika hospitalini,... Mara moja wakawa wanaelekea katika kitengo cha wazazi (leba)... Lakini kabla hawajaingia kwanza wakapokelewa na mama yake mwai
"yaani mume mno hujui kinachoendelea kuhusu mkeo"
Sheby kwa jinsi alivyo hampendi mkewe alimjibu mama mkwe kitu kikali mno
"nani??.. Mke??.. Ivi katika wake wa kuoa mwanao nae yumo"
"ati unasemaje wewe??"
Sheby hakitaka kuongea mengi aliingia mpaka ndani huku saidi akifuata kwa nyuma,... Ghafla anakutana na mama yake huku baba akiwa kakaa mahali katulia na mzee mwenzie
"mama vp..."
"ina maana hujui kama leo mkeo anajifungua"
"hilo nalijua, lakini siwezi kuacha kazi zangu nije nimuangalie anavyojifungua huku"
"haya nenda kaone watoto wako"
Sheby akaingia katika wodi ambayo mkewe kalazwa baada ya kuchomwa sindano ya usingizi, mana alikuwa analeta fujo hapo wodini...
"mbona kalala, na niliskia analeta fujo"
"ndio, tena kaharibu vitu vya watu humu ndani"
"kisa nini"
"watoto"
"wako wapi hao watoto"
Mama kamwonyesha mwanae hao watoto.... Sheby kuwaangalia vizuri walikuwa wazuri, sema walizaliwa vilema wote,... Sheby aliangalia mmoja baada ya mwingine,.. Aligundua mmoja alikuwa hana mikono kabisa, alafu mwingine na mwingine alikiwa ni mkubwa wa kichwa afu ni kipofu pia...
"sasa kwani wana tatizo gani hawa.. Si ugonjwa tu huu, na unatibika"
"we mtoto mjinga sana wewe... Hawa watoto ni wako"
"najua, lakini bado sijaona tofauti kuubwa mpaka mseme mke wangu kajifungua kituko"
"sa we waona ni sahihi"
Sasa wakiwa wanaendelea kuongea mama yake mwai kuna maneno kayasikia vizuri kutoka kwa mama yake sheby
"mama sheby, eti umesema hawa watoto sio wake??.. Kwani mume wa mtoto wangu ni nani"
"sikiliza we mama mwai.... Familia yetu imechoka kuishi na mtoto wako,.. Mimba aliobeba mwanao haikuwa ya mtoto wangu"
"nakuambia hivi mizigo yenu hio"
"weeeeeee kwani kazaa mwangu ishia hapo hapo... Mmeshindwa kumlea mtoto wenu vizuri mnakuja kusema nini"
Wamama hao walikuwa wakitupiana maneno ya hapa na pale kwa kile kilichotokea,..

Ghafla mwai kazinduka baada ya dawa aliopewa ya kulala kuisha nguvu...
"mamaaaaa.... Mama nimebadilishiwa watoto mama"
Kila mtu alishangaa kuskia hivyo... Kuwa mwai kabadirishiwa watoto..
"wala... Anachoongea ni uongo... Hawa watoto ni wakwake"
Aliongea sheby baada ya kusikia mwai anawakataa watoto hao,...
"malipo ni hapa hapa duniani... Nisikilize mama mkwe... Hii mimba haikuwa yakwangu japo mimi ndio mumewe, mimi nilijua hio mimba sio yangu na ndio maana sitishiki kuwaona hao watoto... Kwanza mtoto wenu mlinilazimisha nimuoe wala sio idhini yangu kuoa mtu mzima kiasi hiki...... Mzeee... Kama ni laana mniachie tu nasema hivi mke kwa sasa sitaki... Nyie ndio mlisababisha nioe nasema hivi sitaki mke wa aina hiii"
Sheby leo hakutaka kuogopa kabisa yaani kamwambia mpaka baba yake kama ni laa amwachie tu...
"Weeeee hawa watoto baba yao nani kama we ukimwacha mama yake"
Aliuliza mama yake mwai huku akitaka kumzuia sheby asiondoke...

"muulize mtoto wako... Aliompa mimba ni nani... Afu akisha kili, hao watoto nitawalea mimi kama baba.. Lakini aseme ukweli hawa watoto baba yake nani"
Wakati huo mwai analia tu hana la kusema juu ya hilo
"we mwai sema ukweli tujue"
Kabla mwai hajaanza kusema ghafla kuna sauti ilitokea kwa nyuma...
"mimi nitasema ukweli wote"
Kila mtu aligeuka, japo wengine hawamjui na wapo wanaomjua mtu huyo....
Alikuwa ni mary akiwa na rose...
"ni akina nani hawa"
Aliuliza mama yake sheby huku akiwaangalia
"ni rafiki zake na huyo mwai"
"sasa hawa wanaujua ukweli gani hawa"
"mi sijui"
Akina rose na mary kumbe walisikia yote yaliokuwa yakiongelewa hapo wodini, na wanajua kila kitu kwasababu mwai alikuwa akiwaambia ukweli wa ndoa yake, kuwa hata hio mimba sio ya mume wake
"ni kweli hio mimba haikuwa ya huyu kijana...."
Aliongea Rose na kuwaacha kila mmoja mdomo wazi,...
"we umejuaje"
"huyu ni rafiki yetu... Hatufichi kitu chochote katika ndoa yake... Siku ana mimba sisi ndio wa kwanza kujua, na alituomba ushauri mana mimba hio kaipata ndani ya ndoa yake na mbaya zaidi hajawahi kulala na mumewe toka wafunge ndoa... Mimi nikampa ushauri akaenda kwa mganga ili alale na huyu mume wake mana alikuwa hataki... Mwai Alifanikiwa kulala na sheby kwa njia za uganga, lakini wakati huo tayari ana mimba ya jemsi"
"jemsi??... Jemsi ndio nani tena"
Mama mwai aliuliza
"jemsi ni mpenzi wake kabla hajaolewa na waliendelea na mapenzi yao mpaka alivyoolewa"
Mama mwai alishangaa sana kuskia hivyo... Ghafla wazee nao wakaitana pembeni

"bwana Mohamed.... Mimi nadhani mpaka hapo inatosha.. Nimekuseidia sana, kijana wangu kateseka sana, hata mimi sio kuwa nilikuwa napenda mtoto wangu aoe mtoto wako,.. Sema nilikuseidia uondoe hio aibu yako ya kuwa na mtoto asio olewa,.. Umeniseidia sana katika maisha yangu mpaka sasa nimekuwa tajiri mkubwa, ni kwasababu yako wewe... Nami nikaona nimlazimishe mtoto wangu amuoe binti yako ili kukuondolea aibu ya kukaa na binti mkubwa kiasi kile ambae haolewi... Sasa naomba tuishie hapa bwana Mohamed... Umeshindwa kumlea mtoto wako vyema mpaka sasa anagwaya hana wa kumuoa.... Naomba ndoa yao iishie hapa hapa hospitalini.. Mwanangu kateseka sana, kamaliza pesa nyingi sana kwa ajili ya mtoto wako, sasa nasema basi"

Baba yake sheby loe kaamua, na siri imeshajulikana kumbe waliozeshana kisa waliseidiana huko nyuma katika maisha yao,..
"sawa mzee rashidi... Lakini hili swala la hawa watoto linakuwaje... Kwasababu naona imekuja aibu nyingine mpya"
"wewe si umesikia yule binti alivyosema pale... Kuwa mtoto wako ana mwanaume mwingine tofauti na mumewe, na mtoto wako kamwendea mwanangu kwa mganga ili amsingizie hio mimba"
"jamani hawa watoto mbona wana balaa hivi... Mi nadhani huyu sio mtoto wangu mimi huyu"
"malezi baba.... Mumemlea vibaya mtoto wenu"
Mzee Rashidy ambae ni baba yake sheby,.. Alirudi kule wodini baada ya kuongea na mzee mwenzie... Alipofika wodini alikuta mzozo mkubwa sana baina ya mke wake na mke wa mzee Mohamed...

"eeeee ebu sikilizeni nyinyi wanawake.... Mwamuzi mkuu ni kijana mwenye mke, aamue vipi kuhusu hao watoto... Mana tayari ni binaadamu hao sioni haja ya kugombana"
Aliongea baba yake sheby, baada ya kuona wamama wamechafukwa na kila mtu anataka usahihi kwa mtoto wake, mana mama yake sheby yeye hataki ndoa iendeleee mana hakuipenda toka mwanzo, hivyo mpaka sasa familia ya akina sheby imepata chanzo cha kuikataa ndoa hio...
"sikilizeni wazee wangu... Hapa mimi namueshim kila mmoja aliopo hapa.... Suluhisho la hawa watoto,.. Mimi nipo tayari kuwalea, nipo tayari kuwatibu nchi yeyote ile mpaka wapone, kuhusu huyu kilema huyu.. Hata viungo vya bandia atapewa.. Na huyo kipofu japo kazaliwa na hali hio lakini tutajaribu kuznguka dunia kama atapona, ila kuhusu malezi yao niachieni mimi... Na nitayafanya hayo yote kama mama yao atawakubali.. Na pia nitayafanya hayo yote ila huyu sio mke wangu tena..aishi kwao na watoto wake, mimi nitawalea kwa kila kitu.. Mana kwa roho za sasa hivi hata baba yao haqezi wakubali... Sasa hivi tumetawaliwa na roho za kinyama... Ila ulemavu wa hawa watoto umesababishwa na nyinyi wenyewe"

Maneno ya kijana sheby yaliwapa imani kila mmoja na kujiona ana makosa, yaani licha ya watoto ni vilema lakini kazidi kuwapenda na kuwalipia kila kitu katika maisha yao
"sisi tulisababisha kivipi... Mbona unataka kututusi we kijana"
"unakumbuka siku ile mnawafukuza vilema wa watu mlangoni kisa sherehe yenu ya kitajiri.. Wewe ulikuwa kipau mbele kuwafukuza wale vilema... Mwanao huyo ndio yuko pale kwenye jukwaa anapiga tu kelele watolewe,.. Kisa ni pesa zenu, tena kwenye nyumba yangu.. Ivi ni jinsi gani mlimchukiza mungu.."
"alaaaaaa ivi ilikuwa hivyo"
Baba yake mwai nae anashangaa kuskia hivyo,....
"we mama mwai, ni ya kweli anayoongea huyu kijana"
"lakini ile sherehe ilikuwa ni ya kitajiri baba mwai, sasa wale wangetia aibu"
Mzee huyo hakutaka kuendelea kukaa hapo, aliondoka zake... Mara baba yake sheby kamuita mtoto wake
"sikiliza baba... Wacha mimi niwahi kazini wewe maliza mipango yote hapa ila sitaki tena ndoa iendelee, na kuanzia leo tafuta mwanamke umpendae mwanangu... Ile nilifanya hisani tu kwa bwana Mohamed lakini nilikuwa naumia kukuona unateseka vile"
"usijali mzee yote yatakwisha"

Basi kijana sheby alirudi pale wodini na kumaliza kila kitu, aliwachukuwa na kuwapeleka nyumbani kwao kabisa, kisha huyo akawa anarudi zake kazini akiwa na saidi pamoja na akina rose
"boss.... Kumbe ulikuwa na tatizo kubwa la kifamilia na ulikuwa kimya tu"
Aliongea saidi huku akiwa anaendesha gari
"saidi.. Katika dini yangu ya Kiislamu hua hairuhusu mwanandoa yeyote kutoa siri ya kifamilia... Na ndio mana nilikuwa msiri sana"
"kumbe ndio mana kila mara ulikuwa na mawazo kazini"
"aahhh yote ni maisha tu.. Na kikubwa ni kwamba nashukuru kila mtu keshalijua hili"
Sheby na wafanyakazi wake walifika kazini na kuendelea na kazi, ikiwa ni bado mapema sana....
"enheee tuendelee na maongezi yetu boss"
Alikuwa ni saidi akiwa na boss wake ofisini,
"ivi tulikuwa tunapiga story gani vile"
"ahahahah mambo ya wake"
"aahhh tuachane nayo hio mada... "
Sasa wakiwa bado wanaendelea na stori, ghafla simu ya sheby ikaingia meseji, akatoa simu mfukoni kisha akaifungua ile meseji, ilikuwa inatoka kwa mke wake...
"sheby mume wangu... Siwezi kuishi na hawa watoto... Ni aibu kubwa sana nimeona bora nife nao pamoja, ni watoto wangu wacha nife nao.. Usikose kuja kutuzika"
Heee sheby alitoa macho baada ya kusoma hio meseji...
Mara moja alimpigia simu,... Lakini simu iliita mpaka ikakata. Akarudia tena kwa bahati nzuri ikapokelewa
"halooo mwai, unataka kufanya nini"
"ndio hivyo... Siko tayari kulea vilema... Naomba uchague moja.. Niwapeleke hawa watoto kwa baba yao, afu nirudi tuendeleee kuishi kama kawaida... Au nife na watoto wangu uje kutuzika tu"
 
MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 38..... MWISHO

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp


Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"boss.... Kumbe ulikuwa na tatizo kubwa la kifamilia na ulikuwa kimya tu"
Aliongea saidi huku akiwa anaendesha gari
"saidi.. Katika dini yangu ya Kiislamu hua hairuhusu mwanandoa yeyote kutoa siri ya kifamilia... Na ndio mana nilikuwa msiri sana"
"kumbe ndio mana kila mara ulikuwa na mawazo kazini"
"aahhh yote ni maisha tu.. Na kikubwa ni kwamba nashukuru kila mtu keshalijua hili"
Sheby na wafanyakazi wake walifika kazini na kuendelea na kazi, ikiwa ni bado mapema sana....
"enheee tuendelee na maongezi yetu boss"
Alikuwa ni saidi akiwa na boss wake ofisini,
"ivi tulikuwa tunapiga story gani vile"
"ahahahah mambo ya wake"
"aahhh tuachane nayo hio mada... "
Sasa wakiwa bado wanaendelea na stori, ghafla simu ya sheby ikaingia meseji, akatoa simu mfukoni kisha akaifungua ile meseji, ilikuwa inatoka kwa mke wake...
"sheby mume wangu... Siwezi kuishi na hawa watoto... Ni aibu kubwa sana nimeona bora nife nao pamoja, ni watoto wangu wacha nife nao.. Usikose kuja kutuzika"
Heee sheby alitoa macho baada ya kusoma hio meseji...
Mara moja alimpigia simu,... Lakini simu iliita mpaka ikakata. Akarudia tena kwa bahati nzuri ikapokelewa
"halooo mwai, unataka kufanya nini"
"ndio hivyo... Siko tayari kulea vilema... Naomba uchague moja.. Niwapeleke hawa watoto kwa baba yao, afu nirudi tuendeleee kuishi kama kawaida... Au nife na watoto wangu uje kutuzika tu"

ENDELEA.......

Kijana sheby alishtuka sana kuskia hivyo, na pia alihisi labda ni utani wa mwai, na asingeweza kufanya hivyo katika maisha yake hivyo hata sheby kushtuka kwake ni kwamba anamjua mwai kwa jinsi anavyo yapenda maisha ya kidunia, ni ngumu kufa na wale watoto
"wewe mwai wewe usifanye hivyo.. Na duka lako la lipstick utamwachia nani"
"sheby mume wangu, naomba usilichukulie jambo hili kuwa mzaha, mimi sipo tayari kulea watoto wa aina hii... Mimi nimekamilika itakuwaje marafiki wa familia yangu wakigundua mimi nimezaa vilema"
"lakini ni watoto wako hao.. Muite baba yao mkae chini myajenge, na kama hana uwezo wa kuwatibia au kuwalea, mimi nitawalea hao watoto, kikubwa tu akubali"
"na akikubali mimi narudi kwenye ndoa yangu,.. Mimi bado ni mke wa mtu"
"kama nitakuwa na akili finyu we rudi, lakini kama akili zangu ni timamu, basi kuendelea na wewe kuwa mke wangu sahau"
Sheby aliongea hivyo kisha akakata simu,...

Wakati huo sasa huku kwa mwai baada ya sheby kukata simu, mwai katafuta jina la jemsi na kumpigia, mana anajua hawezi kuruhusiwa kutoka na hali ya uzazi aliokuwa nayo, alimpata jemsi mwenye hao watoto kisha akawa anaongea nae kupitia simu
"baby... Hivi una taarifa gani wewe"
"taarifa.... Sina taarifa yeyote ile"
"beibeee... Una watoto wawili mapacha"
"Weeeeeee, acha utani baby"
"heeee njoo home uwaone"
"heeeee nije kwenu? Na wazazi wako watanionaje"
"heeeee jemsi, ama kweli wewe huna taarifa,.. Mimi nimeshaachana na yule bwege, na sasa hivi wazazi wangu wanajua kuwa baba wa watoto ni wewe,.. Na licha ya hivyo wenyewe wanatamani wakuone"
"weweeeeee mwai acha utani lakini"
"we njooo... Tena njoo sasa hivi"
"sawa basi nakuja"
"ok poa... Usije ukaacha kuja mana hawa watoto wakikuwa afu wazazi wangu hawakujui hutokaa kuwaona na usijijue kama una watoto kwangu"
"nakuja mama watoto wangu"
Jemsi alifurahi sana kuskia mpenzi wake kajifungua watoto mapacha,.. Sasa kumbe mwai kacheza tu kamchezo cha kumuita aje amshikishe watoto wake,
"mama... Yule mshenzi anakuja, naomba akiingia tu milango ifungwe apewe watoto wake"
Aliongea mwai huku akiwa na watoto wake tena kawafunga vizuuuri kabisa wanaonekana sura tu, hivyo hata jemsi akija hawezi kujua chochote kile juu ya watoto hao
"ivi mwai mwanangu, we ulizani ni rahisi mtoto wa kiume kukaa na watoto wadogo kiasi hiki"
"mama atajua mwenyewe huko... Mimi akija hapa nampa watoto awabembeleze huku tukitoka nje, akitoka tu tufunge geti"
"hapana, kwa hali hii hawa watoto hawatokuwa... Kiukweli hata mimi roho ya imani imenijia, na najuta ni kwanini nilowafukuza wale vilema siku ile... Kweli waswahili walisema usitukane mamba ingali hujauvuka mto,.. Tuliwafukuza wale vilema ingali we una mimba..."
"lakini mama, ile sherehe ilikuwa haiwahusu, walifuata nini na ile sherehe ni watu wenye hadhi yetu, mimi bado sijaona kosa lolote lile"
"ivi unajua kuwa sheby mume wako ndio aliwaleta wale watu"
"ati nini"
"tena baada ya kuwafukuza yeye aliwapeleka hotelini na kuwapa mikuku"
"lakini yeye kawatoa wapi"
"si huko barabarani"

Baada ya siku hio kupita, leo ni siku nyingine tena, kijana sheby akiwa nyumbani kwao na wazazi wake wakiwa wanashauriana jambo fulani,
"kiukweli mwanangu nakupa pole sana kwa yaliokukuta ndani ya ndoa yako, nisamehe sana baba"
"lakini baba, kwanini ulifanya hivyo na kunifanya nikose raha siku zote hizo"

"mwanangu sheby.... Huijui siri kubwa ya maisha yangu ila leo wacha nikuambie ili ujue sababu ya kukulazimisha umuoe binti wa Mohamed,... kabla hujazaliwa wewe mimi nilikuwa maskini wa kutupwa,.. Nikiwa na mama yako huyu, na dada yako huyu akiwa kadogo sana,... Mtoto anahitaji kula, mimi sina kazi wala kibarua chochote nilichokuwa nategemea,.. Nilikuwa natamani nipate hata kazi ya kulipwa elfu hamsini kwa mwezi, lakini pia nilikosa ningelipata wapi,.. Miaka hio niliadhilika sana baba yako nikiwa katika jiji hili hili la Arusha... Kwa bahati nzuri bwana Mohamed alihamishwa kikazi kutoka jijini Dar es Salaam kuja arusha,.. Na kazi aliokuwa akifanya ni kazi ya heshima na alikuwa akilipwa kiasi kikubwa cha fedha, mimi nilikuwa simjui hata chembe, lakini siku anahamishwa mimi ndio nilikuwa pale stendi nikizurura tu... Ndio nikapata kazi ya kumbebea vitu vyake vya ndani vyote na mkokoteni,.. Na hapo ni mtu mzima haswa... Yule bwana alinipatia kiasi cha elfu 50, baada ya kumaliza kazi yake,.. Pesa niliotamani kulipwa kwa mwezi leo nimeipata kwa masaa... Kipindi hicho kupata elfu 50 ni kazi na pia ilikuwa kubwa sana,.. Hapo ndipo nilipojua kuna matajiri duniani,.. Lakini bwana Mohamed hakuishia hapo alipenda hata kuja kumtembelea mana mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake niliemseidia vitu vyake,.... Nakumbuka kuna siku nilikutana nae njiani akiwa na gari yake, ndani kuna mtoto wake wa kike na mkewe,.. Wakati huo wewe hujulikani utatungwa lini, nilikuwa na mtoto mmoja tu ambae ni huyu dada yako rehema,.. Bwana Mohamed alinipa lifti mpaka nyumbani kwake, nilipofika tu kwake kanikaribisha vizuri hata kuingia nilikuwa Naogopa sana mana alikuwa akifanya kazi serikalini ni mtu mkubwa sana... Kwakua mimi nilikuwa na shida na kazi, aliniambia nimtafutie kijana wa kutengeneza gadeni hapo nyumbani kwake,.. Sikuweza kufanya hivyo badala yake nikaitaka mimi ile kazi mana hata mimi nilikuwa nina shida.. Nakumbuka bwana Mohamed aliniambia hii kazi ni ya vijana wadogo, sio sisi watu wazima.. Subiri mimi nitakufanyia mpango kwenye kampuni yetu ya kifamilia ufanye kazi... Kiukweli nilishukuru sana kwa hisani alioifanya,.. Kweli nilimtafuta yule kijana wa gadeni, kisha baada ya wiki nikapelekwa kwenye kampuni yao, mana hata wao walikuwa na pesa kwenye familia yao..... Sasa kwakuwa nilipelekwa na boss mkubwa, yaani kwenye hio kampuni bwana Mohamed ndio mkubwa wao... Nilipewa nafasi ya juu sana kwasababu nililetwa na mkubwa wao.. Nililipwa kiasi cha shilingi laki tatu kwa mwezi, ambapo kwa malipo ya sasa ni kama milioni 3 za kitanzania,... Japo humo humo kina wanaolipwa zaidi ya hio yangu.. Lakini lakini tatu kwangu nilikiona ni kipato kikubwa sana.. Na hapo ndipo safari yangu ya maisha mazuri ikaanzia hapo.. Kila nikihitaji mkopo wa laki tano ambayo ni kama milioni tano kwa sasa, bwana Mohamed alikuwa akiniongezea laki tano nyingine,.. Jumla ninakuwa na milioni moja ambapo kwa sasa ni sawa na millioni kumi za kitanzania.... Hapo ndipo nami nikaacha kubweteka, nikawa bahali ili na mimi niwe kama yeye.... Nakumbuka siku namwambia mafanikio yangu, alifurahi sana, nilipomwambia nami naandaa kampuni yangu ya usafirishaji... Alifurahi sana tena akaniuliza katika kampuni yako kuna kitu kimepungua.. Nikamjibu hapana... Kiukweli mzee mwenzangu alinipenda sana.... Na sikuwa na cha kumlipa chochote zaidi ya kutoa shukrani zangu kwake..
Ndipo juzi hapa sasa ndio kanijia na kutaka wewe umuoe binti yake, na aliniomba kwamba nimtolee aibu mana wazee wenzake wote wameozesha mabinti zao, lakini wakwake haolewi kwa tabia za mtoto wake,.. Aliniambia kabisa tabia za mtoto wake ni mbaya sio za kupata mume kabisa, hivyo kaniomba kama mzee mwenzie nitumie sauti ya ubaba naye atumie sauti ya ubaba ili muoane wewe na mtoto wake.. Nikikumbuka fadhila alizonifanyia miaka hio, kiukweli sikuwa na pingamizi juu ya hilo japo moyo ulikuwa ukiniuma kwa hilo.. Lakini nikaona wacha nilipe fadhila alizonifanyia huyu bwana.... Ndipo mkaoana kwa lazima na kuishi kwa lazima...... Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwanangu nisamehe, ubusara wangu ndio uliokutesa mwanangu.. Nisamehe sana baba yako..."

Mzew Rashidy aliongea mengi sana mpaka kila mmoja alichoka, lakini mama anayajua hayo yote, lakini sheby yeye hayajui mana pesa kazikuta hivyo hajui mateso alioyapitia baba yake.... Sasa sheby ndio kujumlisha na ile picha alioiona kule kwenye kabati la baba yake siku ile... Walipiga picha pamoja lakini baba yake alionekana kuchoka sana yaani alikuwa hana mbele wala nyuma, kumbe hivyo ndivyo ilivyokuwa...
"sasa wazee mimi ngoja nitoke kidogo mana kichwa hakijakaa sawa"
Sheby aliaga kihivyo lakini mama yake alimzuia
"wewe... Sasa hebu tuambie una mchumba, mana hatutaki tena uzoee maisha ya kibachela"
"ndio ninae"
Aliposema tu anae, baba kadakia
"sasa kama unae unasubiri nini, au huna pesa za kutosha baba"
"lazima nimwangalie tabia yake kwanza"
"ina mana humjui"
"namjua.. Na hata wewe unamjua ila humjui"
"mmmhhh sawa lakini mimi nisingetaka uishi bila mtu kwa sasa"

Basi kijana sheby alitoka hapo mpaka ofisini kwake....
"saidi vp"
"aaahh poa boss... Hujaonekana toka asubuhi hapa"
"aahhhh si unajua pilika pilika hizi"
"enhee niambie"
"ebu washa gari tukatulie mahali kwanza turefresh mind kidogo"
Saidi anavyopenda kutoka na boss, haikuchukuwa hata dakika gari imeshawashwa mpaka kwenye restaurant moja hivi hapo jijini na kuagiza vibaiti vidogo vidogo.... Sasa wakiwa wanaendelea kula ghafla shadi akatokea maeneo hayo, lakini hakuwaona ila saidi ndio kamuona shadi,... Sasa saidi kwa akili yake akajua sheby alimdanganya ile ishu ya yeye kiwa na mahusiano na mke wake ambae ni zaituni, hivyo akamwonyesha sheby kama anamjua shadi, mana kama hamjui basi ni mwongo lakini kama anamjua basi ni kweli...
"boss, unamjua yule dada"
Sheby kumwangalia vizuri alimjua ni shadi, rafiki yake na zaituni
"ina maana hata wewe humjui mshenga wako"
Aliongea kijana sheby huku akimwangalia saidi
"una maana gani kusema mshenga"
"we ulifikiri bila huyu ungempata zai"
Saidi hapo ndio kajua kweli boss wake hakumdanganya hata kidogo
"kweli boss leo ndio naamini kweli zaituni alikuwa mpenzi wako... Siamini kama nimeoa mtu uliekuwa nae Kimapenzi"
"kwanza zaituni sijawahi kumwingilia kimapenzi, japo nilikuwa namwogesha mwenyewe lakini sijawahi"
"acha kunidanganya boss, yaani uogeshe mwanamke mtu mzima na wewe ni kidume rijali afu uniambie hujalala nae"
"ndio.... Zaituni alikuwa kipofu, na niliapa kutokumgusa mpaka nitakapomuoa"
"aahhhhh kweli sijaona mwanaume kama wewe aiseee......... Shadi... We shadi"
Saidi alimwita shadi aliokuwa kaketi meza ya jirani
"haaaaaaa saidi kumbe upo hapa"
Shadi alikuwa bado hajamuona sheby mana alikuwa kajiinamia kwenye meza, hivyo hakufanikiwa kumwona sura, ila anajua saidi yupo na rafiki yake...
"mambo shem"
Alisalimia shadi huku akimpa mkono saidi..
"safi tu hali yako mtoto mzuri"
"waapi mzuri mkeo..... Mwaya kaka mambo"
Shadi alimsalimia sheby huku akinyoosha mkono wake lainiii... Sheby akainua kichwa na kuupokea mkono, lakini shadi alipomwona kumbe ni sheby alirudisha mkono na kuanza kuongea
"kumbe ni wewe.... Yaani siamini kama kweli kuna wanaume makatili kiasi hiki"
"shem vp tena, mbona umebadirika ghafla"
Aliuliza saidi huku akimsihi akae
"huyu ndie alienipa kazi yake ya kumshawishi zai awe malaya ili ajue kama anampenda,... Mimi nilifanya juu chini ile kazi iende sawa mana hata mimi nilikuwa nampenda huyu kijana kutokana na uchapakazi wake, lakini kumbe nae ni tajiri alitudanganya wote,.. Nikaimaliza kazi yake vizuri,.. Nikamwambia sheby mimi nakupenda na hali yako hio hio ya kuuza viazi, lakini akasema ngoja nifikirie mana alikuwa ana mawazo juu ya kumkosa zai... Nikaona wacha nimuache hizi siku mbili tatu... Heeeeeeee, kwani toka siku hio nilimuona.. Mpaka nikajikuta nayatamani maisha anayoishi zaituni, nami nikaingia huko huko aliko zai.. Roho inaniuma sana, nimemfanyia mwenzangu ukuadi mpaka kaolewa afu mimi nimebaki nahaha na wanaume tu.. Yaani namlaani sana huyu mtu"

Shadi aliongea mengi sana lakini sheby alimtuliza...
"Samahani sana kwa hilo shadi... Lakini hata mimi nilikutafuta sana, kila nikikupigia naambiwa simu inatumika... Nikaona wacha nikuache utanitafuta kama ulivyonitafuta mwanzo na kuniambia unanipenda,.. Ni bahati mbaya tu, naamini utapata mume bora"
"sio rahisi sheby... Mimi nilikupenda wewe na ndio maana nikafanya juu chini zaituni awe malaya ili uwe na mimi... Lakini kumbe malipo yangu ni hapa hapa duniani"
"pole sana... Ila kama unaendelea na kazi hio naomba uache.. Nitakupa mtaji ufanye biashara, achana na hio kazi"
Shadi kuskia mtaji kidogo hasira zikamtua....
"lakini boss, kweli ulichokifanya kwa zai sio kizuri... Mimi naamini zaituni angelikuwa mke wako sema tu hukumfanyia fea"
"aahxxxhhh saidi tuyaache hayo... Mi naona tuondoke hapa"

Baada ya wiki mbili kupita, sheby akiwa nyumbani kwake anapoteza muda kwa kumwagilia mauwa katika bustani yake... Ghafla mlango ulisukumwa na mtu kuingia...
"we vp, umefukuzwa huko kwenu"
Aliongea sheby huku akimsogelea, na hakuwa mwingine bali alikuwa ni mwai,..
"Si nimerudi kwa mume wangu"
"heeeeeeee ehehehehe halooooo.... Ahhh umeacha nimecheka kicheko cha kike kwa ujinga wako... Kwanza kabla ya yote watoto wakuwapi mana sijawahi hata kusikia matumizi wiki ya tatu hii sasa inaisha"
"watoto kawachukuwa baba yao"
"una uhakika kawakubali"
"ndio"
"ok sawa... Vp una njaa upikiwe"
"nikapike mwenyewe au nipikiwe"
"heeeeeeeee ivi kumbe hujui... Aahhhh nakumbuka kadi ziliisha hukupewa kadi wewe... Kiukweli nina siku ya nne sasa toka nioe"
"whaaaat... "
"ohoooo.... Unashngaa tena... Mimi nimeshaoa... We mama chidi"
Sheby alimwita mkewe atoke ili aamini kweli kaoa.... Laaaaa Haulaaa mwai kabaki mdomo wazi kwa mke aliomuona....
"mary.... Yaani umethubutu kuolewa na mume wangu mary"
"Eh eh samahani we mwanamke... Naitwa hadija bibie... Mimi sio mary.. Mary bado hajaolewa, naitwa hadija.. Mwanamke ninaejua thamani ya ndoa.. Wanawake wenzio wanaitafuta ndoa kwa udi na uvumba we waichezea nyoooo..... Wanaume wenyewe wa kuoa wako wapi?? Leo upate afu uchezeee... Eti zoba, zoba kwako, kwangu mume huyu"

Mary au hadija kwa jina ndoa aliongea kwa nyodo kali kumlingishia rafiki yake kipenzi kuwa sasa ni mume wa mtu
"mary yaani unanifanyia hivi kweli.. Mimi... Nani kawaleta kwenye huu mji"
"i Know ni wewe, lakini umeichezea ndoa mwenyewe... Wanaume wachache dunia hii... Umempata afu wamchezea loooo unalo ilo"
Ghafla mlango ukasukumwa na mtu mwingine kaingia, alikuwa ni rose...
"habari zenu jamani... Poleni kwa maumivu ya kupoteza ndoa wengine poleni kwa furaha ya kupata ndoa... We bibie mpoteza ndoa.. Unasubiriwa na askari hapo nje.. Naskia umeuwa"
"kauwa??"
Sheby kashangaa kuskia mwai kauwa
"ndio.... Vile vitoto kaviua"
"astakafilu lah jamani mwai.... Haya kisa ni nini"
"lakini hayupo peke yake.... Yupo na jemsi wake, wapo nae hapo nje kajaa pingu ngwi"
Rose alikuwa akiongea kwa mbwembwe nyingi sana mana maisha ni yao kwa sasa...
"rose kwanini hamkumbuki fadhila zangu lakini"
"heeeee we mfungwa vipi, ebu nenda uko... Umeyachezea mwenyewe sasa kayachezee mavi huko gerezani"
Rose alikuwa akitoa maneno shombo.. Ghafla geti likagongwa,.. Alikuwa ni askari
"afande, mwanamke mwenyewe ni huyu hapa"
"kamata huyo atatoa maelezo kituoni"
Sheby alitaka kuingilia kati anagalao kumtetea mwai, lakink alizuiwa na rose
"shem.. Hii kesi haikuhusu.. Tulia uifurahie ndoa yako..... Hadija mdogo wangu, nakuomba sana itunze ndoa yako mama... Ukiachwa utajiju... Mpaka sasa mimi mwenzio tayari nina mchumba na dini nabadirisha na mimi... Nami ndani ya ndoa mama.. Staki utani"
"unaolewa lini dada rose"
"wiki hizi hizi..."
Sheby akaingilia kati juu ya swala hilo
"mmeo anajiweza kuusu harusi... Mana kama hajiwezi niigharamikie mimi hio ndoa yenu"
"kiukweli shem hata yeye kashiba.. Sio mbaya na nadhani unamfahamu"
"ni nani huyo"
"jamali"
"heeeeeeeee na yule bwege nae anaoa"
Jamali ni mfanyakazi wake, ambae wanafanya nae kazi kampuni moja, nae kumbe kamuona rose kuwa kama mkewe...
"hadija... Binafsi kwa mimi namuomba mungu anifanye nitulie kwenye ndoa yangu.. Sasa hivi sitaxki starehe yeyote, sasa nafuata njia zako hadija... Sasa nimeamua kutulia, naomba tutulie hadija... Dunia hii haina wanaume.. Ukimpata mama tulia mlee watoto....... Shem"
Rose alimwita sheby
"ndio shem"
"nilikuja kuwatembelea tu.. Na kuwaonyesha hawa askari sehemu alipokimbilia mwai... Wacha nirudi si mnajua leo wikiende mume wangu yupo nyumbani... Naombeni niende"
Rose kabadirika sana kutoka kwenye maisha ya kidigitali mpaka kwenye maisha ya kidini, huezi amini rose sasa ni mtu wa hijabu hataki tena mambo ya sherehe....
"rose... Binafsi hata sisi tunakuombea ndoa njema... Nasi hatukuzuii mana unakwenda kuwa mke wa mtu"
"nashukuru sana... Nanyi muishi kwa amani"
Rose aliondoka zake tena alikuja na gari ya mchumba wake ambae ni jaxxmali.... Sheby kamuoa mary tena unaambiwa siku ya ndoa hata mary alikuwa hajui, kaenda kiburuzwa tu ofisini mpaka ukumbini na kukutana na shela la harusi.. Unaamniwa baada ya ndoa mary alizimia, mana alihisi ni ndoto kwake....
"ivi umepika wewe umekuja kuskiza umbea tu hapa nje"
Aliongea sheby kwa kumwambia mkewe
"heeeeeee mume wangu.. Chakula karibia kinapoa sasa"
"wacha bwana"
Sheby alimbeba mkewe mpaka ndani katika meza ya chakula...

MWISHO..........

JAMANI DADA ZANGU PUNGUZENI NYODO... DUNIANI KUNA PINGILI TATU ZA MAISHA... (1) KUZALIWA.... (2) KUOLEWA (3) NA KUFA.... KWAHIO JUA NI LAZIMA UOLEWE, SASA KWANINI ULETE NYODO MAMA... WANAUME NI WACHACHE SANA KWENYE HII DUNIA.. UKISKIA KASEMA ANATAKA KUKUOA, KAZANIA MANA NDOA USHACHANGULIWA HIVYO... ACHENI TAMAA ZA MAISHA.. TAFUTENI ZENU MZIFURAHIE SIO UTAMANI KUOLEWA NA TAJIRI WAKATI KAZITAFUTA MWENYEWE... ATAKUNYANYASA SANA MANA PESA ZAKE UMEZIKUTA... PUNGUZENI NYODO JAMANI KUOLEWA NI SHERIA TENA NI LAZIMA NA SIO OMBI.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom