Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mzee huyu bebe mpya wa mjini alipitia mengi na kuvumilia mengi ila akivumilia ma hawa kweli ntazidi kumpa respect
fcc861e4fad325be5debd736de03a37a.jpg
 
MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 36

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp


Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"mmeo nini huyo"
Aliuliza rose huku kama wanaogopa ogopa hivi mana kwenda kubwata umbea kwenye nyumba za watu ni kitendo kibaya sana tena kwa sisi wanaume hua hatukipendi kabisa yani, mwanamke utoke kwako uje huku kuleta umbea tu, ndio uharibifu wa ndoa sema hawajui tu wenyewe.. Sasa kama kawaida ya mke wa sheby kukaa mlangoni ili tu ampokee na maneno,
"leo hujaleta hata chochote, yaani mwanaume wewe"
Mwanaheri aliongea hivyo huku sheby akishuka kwenye gari na msunyo mkubwaaa,...
"nipishe mimi"
"lakini si nimekuuliza tu"
"unaniuliza mie baba ako"
"Wwhaaaaaat"
Sasa mwai anasema What, sheby nae ndio anawaona akina mary...
"ooohhh leo kuna ugeni leo"
Sasa mary na rose ndio wanashangaa, ina maana kumbe rafiki yao ndio kaolewa na boss wao,. Sasa mwai nae anataka kutambulisha anakuta watu wanajuana siku nyingi tu,.. Mwai anashanga hawa wakina rose na mume wake wamejuana wapi...
"nyi... Nyie... Nyie mnajuana"
Mwai au mke wa sheby Aliuliza, na sheby pale pale akajibu kwa uchangamfu wa hali ya juu..
"ndio... Ni wafanyakazi wenzangu hawa.. Sasa kwanini umekuja usiku jamani"
Sasa sheby yeye anajua katembelewa yeye,...
"rose na mary, anachokisema mme wangu ni kweli mnafanya nae kazi"
"ndio.. Tena ni boss wetu huyu"
Sasa mwai kuskia hivyo akagundua jambo
"ina maana siku zoote hizo kumbe mnamgombania mume wangu rose??... Hapana kitaeleweka tu hapa"
Mwai alianza kufunga kanga kiunoni, wakati huo sheby nae anashangaa kumbe mkewe na akina rose wanajuana.....

ENDELEA........

Kwanza kabla ya yote naomba nitoe stori fupi ya hawa marafiki watatu walifikaje fikaje jijini Arusha

Hakuna kitu kibaya kama marafiki kuibiana wanaume, hata kwa wewe mtoto wa kike ambae una rafiki yako kipenzi, ebu jaribu kuwa karibu na mpenzi wake, mi nakuambia lazima urafiki ufe au utetereke,... Kwa akina rose na mwai ni marafiki wa muda mrefu sana tena wakiwa wanapendana mno,.. Mwai na familia yake walikuwa wakiishi jijini Dar es Salaam sema ule uhamishwaji wa kikazi ndio uliowafanya waje kuishi arusha, na hapo ndipo wakakutana na familia ya akina sheby,... Marafiki zake walitamani sana kuja kuishi na rafiki yao huku jijini Arusha, lakini wao hawakuwa na ndugu hata wa kufikia, lakini kwakuwa mwai kwao walikuwa wakijiweza kimaisha aliweza kuwaita rafiki zake hao na kuwapangishia chumba kila kitu wakawa wanaishi juu ya mwai... Sio chakula sio mavazi, kiukweli ni urafiki wa hali ya juu mno ambao sidhani kama upo kiukweli,... Kama jinsi ilivyo tunajua akina rose walitafuta kazi na hatmae kupata, lakini mbali na kazi walitokea kumpenda boss wao, bila kujua boss huyo huyo ndio mume wa rafiki yao mkubwa aliowaita hapa jijini, na leo mke wa mtu ndio anagundua kumbe rafiki zake ndio wanaomuibia mume wake

"rose na mary, anachokisema mme wangu ni kweli mnafanya nae kazi"
"ndio.. Tena ni boss wetu huyu"
Sasa mwai kuskia hivyo akagundua jambo
"ina maana siku zoote hizo kumbe mnamgombania mume wangu rose??... Hapana kitaeleweka tu hapa"
Mwai akiwa anafunga kanga katika kiuno, mana kwa sasa kama unakumbuka anampenda sheby kwa mapenzi ya siku moja tu.. Na wakati alikuwa hampendi kupita kiasi lakini leo anamjali mno...
"ngojaaa ngojaaa.... Yaani mimi na akili yangu nitembee na hivi vikaragosi, wasichana ambao sio hadhi yangu... Ebu jieshim wewe, siwezi kutembea na watu taipu yako"
Sheby aliongea utumbo utumbo lakini ni moja kati ya utetezi juu ya ugomvi uliotaka kuzuka kwa wakati huo

"sasa kwani huko ofisini boss ni nani? Si wewe na akitoka wewe ni baba yako haya nani mwingine"
"saidi... Jamali wote hao ni maboss kwenye kampuni yetu"
Sheby alizidi kuongeza idadi ya maboss katika kampuni yao ili tu wasichana hao wasikutwe na dhuruba ya ugomvi wa mkewe....
"eti mary anayosema ni ya kweli"
"ndio dada mwai... Sisi hatumgombanii huyu"
Ni maneno ya ujinga tu alioyaongea sheby lakini yamekuja kuonekana ni kweli hawakuwa na uhusiano na sheby, ila ni maneno tu ukweli ndio huo, mana hao wakina Saidi na jamali wote ni wafanyakazi wadogo sana, lakini mkewe kaamini kuwa ni kweli.....
"aahhh basi tusameheane jamani... Nadhani mnajua uchungu wa mume"
Aliongea mwai, na wakati huo sheby keshaingia zake ndani anaoga.... Hata akina rose hawakuwa na hamu ya kukaa eneo hilo tena.... Waliaga na mwai aliwasindikiza kwa gari yake yeye mwenyewe kisha akarudi nyumbani kwake.... Aliporudi kakaa kwenye kioo anajipaka wanja malipustiki, yaani na usiku huo yeye ni kujipaka tu wala hajui kuwa ana mume au vipi, kitumbo chake kilikuwa ni kikubwa haswa mana tayari ni miezi kama 6 hivi....

Tukija huku kwa akina rose usiku huo huo baada ya kufikishwa nyumbani kwao,.. Kila mmoja alikiwa akishangaa
"we rose, ina mana kumbe boss sheby kamuoa mwai? Au naota jamani"
"hilo swali mwenyewe nataka kukuuliza, mana siamini amini"
"kumbe mwai alikuwa anatupigia story ya mume wake alivyo mume bwege mjinga mjinga tuu zoba zoba, kumbe ni boss sheby"
"mi mwenzio nimechoka yaani we acha tu"
"sasa huo uzoba wake ni upi.... Kweli mwai haipendi ndoa yake"
Walikuwa wakiongea na kujikuta wanasahau yakwao kuwa wana ugomvi,...
"haya sasa mary, huyo ni shemu wako, bado unaendelea kumpenda"
Rose alimuuliza mary kuwa bado anaendelea kumpenda, mana keshajua ni mume wa rafiki yake...
"mimi najua hawapendani... Sheby nampenda kutoka moyoni"
"we mary wewe, lakini si unamjua mwai alivyo mkorofi"
"mapenzi rose... Yaani toka siku ile ananishika mapaja, mpaka leo nahisi mkono wake upo mwilini mwangu,.. Sheby ni mwanaume wa tofauti sana mi sijui ata nifanyeje"

Siku iliofuata sheby akiwa ofisini kwake akiendelea na majukumu yake ya kikazi, ghafla Saidi kaingia...
"za saa izi boss"
"safi tu vp"
"fresh... Ebwana jana ulikuja kwa mama mkwe pale nikasema nawe ulitaka jiko nini pale"
"aaahhh amna, yule namfahamu mno hivyo nilikwenda kumjulia hali"
"kwani alikuwa anaumwa"
"ana mtoto ambae ni kipofu, sasa nilikwenda kumjulia hali"
Sheby aliongea kama mafumbo hivi lakini kipofu ni huyo huyo mke wa saidi, sema sheby hapendi kuharibu uhusiano wao, mana ni kumkosa keshamkosa...
"mbona sisi hatujamuona na hata zaituni hajaniambia kama ana ndugu mgonjwa wa macho"
"hawezi kukuambia.. Ila usimuulize na ipo siku nitakuambia tu"
"mmmmhhh haya bwana... Ila sina hata wiki moja nafunga ndoa"
"wacha weee.. Aaahh ama kweli saidi umependa sio utani, utaki mchezo"
"nimechoka kuwa bachelor kaka.. Wacha nioe mtoto zai"
Sheby kuskia hivyo roho inamuuma sana, maana ndio alikuwa awe mkewe,...
"vp boss mbona umebadirika ghafla"
"aahhh tuyaache hayo... Nicheki baadae"
Sheby roho ilimuuma pale aliposikia mchumba wake ndio ataolewa hivi karibuni

BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA

Baada ya miezi mitatu kupita, ikiwa ni siku nyingine tena,... Sheby akiwa zake ofisini akiendelea na kazi za hapa na pale, ghafla simu yake inaita, kuangalia jina alikuwa ni mke wake
"heeeee lina nini tena hili"
Aliongea sheby huku akitaka kusita kuipokea,
"haloooo"
"Eeeeh samahani sjui naongea na mume wa mwai"
Ilikuwa ni sauti ya kike ilioongea kwa kutumia simu ya mwai
"ndio Kwani we nani"
"mimi ni daktari... Na mkeo kajifungua watoto mapacha"
"ooohhh mpe hongera zake"
Hata daktari alishangaa sana kuona mume analipokea jambo zuri kama hilo lakini haonekani kufurahi hata kidogo...
"ok sio mbaya ungefika hospitali"
"nipo bize nitakuja baadae au kama vipi tutakutana nyumbani"
Sheby alikata simu kisha akaendelea na kazi,... Unajua uzuri ni kwamba sheby anajua fika ile haikuwa mimba yake, sema kwa ajili ya familia yake kutaka kuishi na mke wa aina hio ndio maana muda wote kawa kimya lakini anajua kiwa mkewe alibeba mimba ya mtu mwingine na sio mume wake....

Ghafla aliingia saidi na kumshtua sana boss wake, mana alikuwa katika dimbwi la mawazo mazito sana
"boss vp mbona kama una mawazo hivi"
"aaahhh we acha tu, mke wangu kajifungua"
"weweeeeeee hongera sana... Ila mbona ni habari nzuri afu huna raha"
"aaahhh ni mambo ya kikazi tu"
"aahhh basi nami mke wangu katoka kupima.. Anayo"
"wacha bwana... Miezi mitatu mkeo ana mimba"
"aahhhh chezea vijana wewe"
"duuuu hongera sana saidi"
Aliongea sheby kuskia mke wa saidi ana ujauzito,...
"Ahsante sana boss, hata mimi nina furaha sana juu ya hilo"
"ila umpende... Hakikisha unampenda, isije ikatokea kama ilivyotokea kwangu"
"kwako.... Kumbe hata wewe shem alikusumbua sana"
"zaituni wako huyo"
"zaituni wangu kafanyaje boss"
"sikiliza nikuambie saidi.... Huyu mkeo alikuwa awe mke wangu mimi.. Lakini kwa tamaa zake akajikuta kashawishika na kuingia mtaani, tena nia yake yeye alikuwa ajiuze, lakini kwa bahati nzuri ukakutana nae wewe na ukaweka nia ya kumuoa na umeshamuoa"
"unajua boss mi bado sijakuelewa ujue.....ina maana wewe na zaituni huyu mke wangu mnajuana"
"haswaaa tena mi nilianza nae toka akiwa kipofu"
"whaaaaat, yaani zaituni huyu huyu alikuwa kipofu"
"ndio.. Lakini mimi nilimpenda hivyo, na upofu wake tena akiwa barabarani anaomba omba... Nikampenda na kuanza kuishi nae,... Na ndio mana kuna siku nilikuuliza ivi kwa mfano anakuwa kipofu ungefanyeje.. Ukajibu huezi kuishi nae"
"aaahhh boss.... Mbona stori nzuri afu sijui kama unamlenga mke wangu tu au"
"sikiliza saidi, kitu kilichomkimbiza zaituni katika himaya yangu ni uhaba wa maisha... Baada ya mimi kumkuta ni kipofu nikajifanya nimekopa pesa,.. Unakumbuka ile safari yangu ya india"
"ndio nakumbuka sana tu, si ile ulioenda mpaka dubai"
"ndio.... Sasa kwenye ile safari nilikuwa nae, akatibiwa vizuri kabisa mpaka akapona,.. Nikaona ili nijue kama kweli ananipenda, nikawa toka siku hio najifanya maskini wa kutupwa... Tena ilifikia hatua nakodisha mkokoteni uliojaa viazi ili ajue kazi yangu ni ya kuuza viazi.. Tena hata nyumba niliopanga ilikuwa ni mbavu za mbwa... Zaituni huyu nimeishi nae kwenye mbavu za mbwa ili ajue mie masikini... Nikaona hio nayo haitoshi nikamtumia mwanamke mmoja hivi amshawishi kuwa na tamaa ili nione ana tamaa... Kama unamjua rafiki yake huyu anaitwa shadi.... Huyo ndio niliompa kazi ya kumfanya ashawishike"
"bosiiiiiiii hivi unayoyasema ni ya kweli"
"si unamjua shadi wewe"
"ndio shemeji yule"
"muulize sasa full story atakupa... Na ndio mana nakuambia mpende mtoto wa watu"
"mungu wangu yaani siamini jamani.. Ama kweli hawa wanawake kweli pasua kichwa... Lakini boss huoni wewe ndio sababu mpaka akashawishika"
"kivipi"
"sasa mitego yote hio mungu wangu"
"kwa mwanamke mwenye akili, asingeweza kusubutu kufanya ujinga kama huo... Tena akikumbuka alikuwa kipofu na leo kaona kwa ajili ya huyu mwanaume, yaani asingetakiwa kufanya hivyo alitakiwa akumbuke alikuwaje... Lakini ndio hivyo bwana"
"kwahio wewe ulikuwa muuza viazi"
"kabisa.. Ili nisije kupendwa kwa ajili ya pesa zangu... Na unakumbuka siku ile nilikuja kwao nikakukuta"
"eeeeee siku ile ndio naikumbuka"
"nilikuja kumpa mama ukweli wa mtoto wake, lakini mama akatikisa kichwa kuwa nisiseme mbele yako ili mtoto wake asikose bara na pwani... Nyumba ile walikuwa wanadaiwa kodi chungu nzima.. Lakini nikapambana mpaka nikainunua kabisa.. Ebu angali ni jinsi gani roho isiniume saidi.. Lakini moyo wangu ulitulia baada ya kusikia ni wewe ndio unaoa.. Nikaona hakuna shida yote maisha tu"
Sasa katikati ya maongezi yao ghafla simu ya sheby ikaita, kuangalia namba ilikuwa ni ile ya mke wake...
"haloo, jamani nipo bize jamani naombeni dakika chache"
Aliongea sheby huku akipiga meza kwa hasira
"samahani baba... Mkeo analeta fujo huku hataki watoto wake"
"hataki watoto wake... Kwanini asiwatake.. Au kawa chizi"
"hapana.... Hawataki kwasababu watoto hao hawako sawa"
Sheby alishangaa kuskia watoto hao hawako sawa
"watoto hawako sawa kivipi dokta?"
Sheby aliuliza huku akiwa mpole kwa kusubiri majibu toka kwa dokta huyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom