Zaburi 146
1 Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.
2 Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.