Makapuku Forum

Makapuku Forum

098578c01d506c98a9a464efedbc1be7.jpg



Pole
Pole ya nini mkuu?
 
Muziki: Bila Makeke

Makeke ina tafasiri nyingi sana na kutegemea na nini na wapi unataka uitumie. Kila mmoja wetu humu, yes, sisi makapuku ana makeke yake, tunaoanza na kusalimia, wapo wanaooga kwanza ndo wanaingia hapa na wapo wanaoingia hapa wakiwa wamejipodoa wakapodoka na wapo wale sasa kama anko wangu ambao wanaingia hapa wakiwa tingasi, tilalila kwa hangouver za jana. na uzuri wake wa haya makeke ni nini, wote tunabaki kuwa Makapuku waheshimika na kwa namna hiyo ninakusalimia.

Mawazo yetu tunaweza kuyaweka katika sehemu tatu kama alivyowahi kusema Socrates, kuna mawazo ya utu, uhalisia na tamaa. Kwenye uhalisia ni pale unapowaza ukiwa na facts ili kufanya maamuzi, mawzo ya utu ni yale ya kiungwana na kuna yale mawazo ya kutamaa (desiring). Hakuna asiyetamani na kutamani sio kosa sema husuda ndo kosa (ukikijua kiswahili raha sana). Kutamani unatamani bila kuwa na wivu ila husuda huzaa wivu na mawazo ya unyang'anyi na hiki si kitu kizuri kwa afya yako na ya mwingine. Tufanye yale tunayoyaweza na tusiache kusaidia pale tunapohitajika iwe kwa kuombwa au kutoombwa (tafadhari usitoe 'o'moja kwenye kitenzi changu cha kutoombwa).

Muziki sasa, leo sijui anko wangu kaenda wapi maana nimemtafuta kwenye simu sijampata na ujue damu nzito kuliko maji, huyu ni anko wangu kabisa na ninadhani leo ana majukumu ya kikazi, akimaliza atanijulisha. halafu leo sina baya hata moja la kumuhusu anko wangu, au hiki kipengele sijaandika mimi? Burudika na muziki

Anaitwa Oumou Sangare, toka Mali mshindi wa tuzo ya Grammy 2011, mwanaharakati anayepinga ndoa za utotoni na ndoa za mitala (hapa anko wangu lazima ampinge tu) na ni mwanamama mjasiriamali aliyeingia ubia na kampuni la China kutengeneza magari yenye jina lake.

 
Muziki wa Mdhamini

Ni chaguo la aunt yangu Shunie ambalo sina hakika kama anataka kumdediketia anko wangu au anataka kuutupa tu hewani sandakalawe kwa kila kapuku afurahie na nitajipa benefit of doubt kwamba anataka tuusikilize na kuufurahia kwa sababu yeye anafurahi.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom