Zaburi 144
1 Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana.
2 Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu.
3 Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue? Na binadamu hata umwangalie?
4 Binadamu amefanana na ubatili, Siku zake ni kama kivuli kipitacho.