MKE JEURI
(The Wife's Tyrant)
Sehemu Ya 16
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Simulizi hii inakujia kwa udhamini mkubwa wa #km_music
#KM _MUSIC INAWAKARIBISHA WASANII WOTE KUFANYA KAZI NAO NA WANAFANYA AINA ZOTE ZA MUZIKI.PIA KAMA UKO MKOANI NA UNAHITAJI BEAT KALI WASILIANA NAO KWA SIMU NA +255743761268
#kmmusic_____music for life
OFA!!! OFA!!! KABAMBE KWA WAKAZI WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA
KWA MAHITAJI YA SOFA BORA ZA KISASA NA ZA KILEO USIACHE KUMTAFUTA #ADAM_KIM HUYU NI FUNDI WA UHAKIKA ANAKUJA SEHEMU YOYO
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
"lakini mpenzi aliompata sasa hivi wala hana hela kama wale wa mwanzo"
Aliongea neema na kumfanya Zainabu kushtuka
"weeeeeeee, tena sasa hivi ndio kapata tajiri haswa.. Yaani yule mkaka ana pesa"
Sasa kumbe zaituni alikuwa akizisikia zile story.. Mana dirisha lilikuwa wazi, na yeye alikuwa chumbani kwake...
"mmmmhhhh mwanaume yenyewe hata nguo hajui kuvaa yule, yaani katika hasara ya wanaume aliowapata ndugu yako, huyu ni hasara"
"neema wewe hujui... Yule mwanaume mimi ndio mtu wa kwanza kukutana nae"
"ulikutana nae wapi wewe"
"nilikutana nae supamaketi akiwa na mdogo wake wa kiume,... Gari wanayotumia ni gari ya pesa haswa"
"we Zainabu muongo mmmhhh sikuezi"
Sasa zaituni ndio kwanza anatega skio vizuri...
"sasa sikia... Unaiona hii nyumba yetu"
"ndio"
"yeye ndio kainunua, na yeye ndio kaikarabati upyaaa"
Sasa huku ndani zaituni ndio anafungukwa na masikio, kumbe mpenzi wake ni tajiri kiasi hicho afu anaishi kwenye kibanda kina matundu kila kona..
Zaituni bila kuchelewa alimfuata mama yake na kumuuliza
"mama, ina maana kukosa kwangu kuona ndio hata ukweli hutaki kuniambia"
"una nini zai mwanangu, kwani mimi nimekudanganyia nini"
"nani kununua hii nyumba.. Na kama ni huyu mchumba wangu mbona ni muuza viazi, au ni jambazi afu mnanificha, kwahio mnataka niolewe na jambazi si ndio mama"
ENDELEA........
Katika maisha ya hapa duniani, kuna viungo ukivikosa basi wengine husema bora ufe tu, japo wengine hutamani kuishi, wakati zai akiwa kipofu alikuwa haoni vitu vingi vizuri na vibaya, alikuwa akisikia tu lakini kukiona kwake ni ngumu, uhusiano wake wa yeye na sheby ulianza kipindi akiwa kipofu, hivyo hajui sheby ana kazi gani, lakini kwa kuelezewa aliweza kujua kuwa sheby ni muuza viazi, na hata alipokuja kupona pia alimwona kweli sheby ni muuza viazi, lakini alishangaa sana kumsikia ndugu yake Zainabu akisema kuwa kijana alienae kwa sasa ni tajiri kuliko hata wale waliopita,... Sasa zaituni baada ya kusikia hivyo, ikabidi amfuate mama yake na kumuuliza kama ifuatavyo
"nani kununua hii nyumba.. Na kama ni huyu mchumba wangu mbona ni muuza viazi, au ni jambazi afu mnanificha, kwahio mnataka niolewe na jambazi si ndio mama"
Aliongea zai huku akiwa mkali kwa mama yake, mana haelewi chochote kinachoendelea kuhusu kijana huyo
"zai mwanangu, nani kakuambia ujinga"
"si nimewasikia akina zai wanaongea huko nje"
"we kweli akili huna wewe, yaani unatekwa kiakili na Zainabu, huyo zai kamjulia wapi huyu kijana kama sio uongo, unatekwa kiakili wewe tulia na mchumba wako ndoa sio kitu cha mchezo mchezo"
Sasa zaituni akafikiria kweli toka akiwa kipofu alisikia kazi ya huyu mtu, mpaka leo anaona na anamuona anauza viazi kwa mkokoteni tena anatembeza mtaani, sasa kwanini adanganyike kuwa ana hela,... Zaituni aliona kweli huo ni ujinga.. Ila kitu anachokililia zai ni kwamba, kama sheby ana hela sasa kwanini anaishi kwenye kile kibanda,.. Basi zaituni alitulia lakini mama anajua ukweli wote kuwa sheby yu hali gani,..
Mida ya jioni huku kwa sheby akiwa ndio anatoka kazini lakini hana hata raha yaani toka lile swala litokee basi amekuwa mtu wa mawazo tuuu mwanzo mwisho,.. Alipanda gari yake na kutaka kuondoka lakini rose alimsimamisha
"Samahani boss, naomba utuache pale kona"
"sawa pandeni"
Rose alikimbilia kukaa mbele, na ile nafasi ya kukaa mbele mary alikuwa anaitamani kuliko maelezo, lakini kwa bahati mbaya kawahiwa na rose, maskini mary ni mpole na vitu vyake havina haraka,.. Basi safari ilianza lakini sasa mary alijikuta anafuraha kwa nafasi ya kukaa nyima, mana alikuwa ana nafasi nzuri ya kuongea na sheby hata kwa macho tu,.. Kwahio rose akajikuta kumbe mbele kakimbilia bure tu lakini siti ya nyuma ndio ilikuwa ishu... Sasa mary akawa anamuona sheby kupitia kile kioo cha pele mbele ya dereva, kile ambacho dereva anaweza kumuona abiria wa nyuma,.. Sheby akipiga jicho anakutana na macho makubwa ya mary, kijana anarudisha macho kwa aibu,... Mary akaona bora ampe pole mana alikuwa anaumwa,... Unacheki sasa mambo yanavyonoga yaani rose kabugi step,.. Mary aliandika ujumbe flani kwenye karatasi kisha ile karatasi akaibandika kwenye paji la uso wake,... Sheby kucheki kioo akakutana na ujumbe kwenye maji la uso wa mary..
"niliskia unaumwa na ndio mana nilikuja mbio pale ndani... Pole sana boss"
Sheby alikisoma kisha akashusha macho chini kana kwamba tayari keshakisoma
"ahsante"
Aliongea sheby huku kaangalia mbele mana yeye ndio dereva mwenyewe, sasa rose akashangaa mbona boss kasema asante na hakuna mtu aliokuwa anaongea nae, rose akiangalia simu ya boss wake, wala haikuwa ikiita wala nini, lakini kasema Ahsante... Rose akamwangalia mary, akamkuta mary kanyamaza kimyaa kama vile hajui kitu, na wakati huo karatasi keshaitoa kwenye paji lake la uso,. Hivyo kakakuka kau....
Rose hakutaka kuendelea kudadisi sana kwanini boss wake kasema Ahsante,...
Mary kaandika karatasi nyingine na kuiweka katika paji la uso, kisha kijana huyo akaisoma
"boss napenda ufurahi muda wote"
Sheby alisoma ujumbe huo kisha akasema
"sawa usijali, ni mawazo madogo madogo tu wala hakuna shida"
Na Wakati huo sheby anaongea sio kuwa anamwangalia mtu, hapana bali macho yake mbele huku anaongea, mana aligundua kuwa mary hakua akihitaji mtu ajue, hivyo hata sheby alikuwa akijibu na mtu hajui anamjibu nani...
"boss unaongea na nani"
Rose kavunja ukimya baada ya kuzidi kumsikia boss wake anabwatuka tu, bila kujua mary ndio chanzo,... Rose akimwangalia mary anamkuta kakaa kimya katulia tulii kama vile hajui..
"we acha tu rose, ni mawazo tu yananiandama"
Aliongea sheby huku wakikaribia nyumbani kwao kwa akina rose...
"mmmhhh pole sana boss"
"ahsante"
Sheby anasimamisha gari na kuwashusha abiria wake,..
"Ahsante boss... Mungu akubariki boss wetu"
Kila mtu alitoa shukrani zake za dhati kwa kijana huyo aliokuwa mpole wa ajabu...
Sheby aliondoka zake na kupotelea huko... Wakati huku wakina rose wanaulizana
"we mary, ivi ulimsikia boss kwa makini"
"ndio, hata sijui kapatwa na nini maskini ya mungu"
"mmmhhh boss ana shida, tena sio ndogo, yaani mpaka anaongea mwenyewe"
"we acha tu rose"
Mary nae alijifanya hajui chochote kilichokuwa kikiendelea, kumbe yeye ndio sababu ya boss kubwatuka kwa ujanja aliokuwa nao...
Basi siku zilizidi kwenda na leo ni siku ya Jumamosi, hata kijana sheby hakwenda kazini, karibia familia yote haikwenda kazini kwasababu kuna maandalizi ya harusi ya mtoto wake, haswa mzee ndio alikuwa bize sana, harusi ilioandaliwa kitajiri sana, mana inakwenda kufanyika katika mijumba ya kifahari huko mjini,.. Shamra shamra zilikuwa nyingi mno, wakati huo kijana sheby yupo ndani katulia tuliii anasubiri kinachoendelea
Siku hio ilikwisha na leo ni siku ya Jumapili ambayo ndio siku ya kufunga ndoa kwa kijana sheby,.. Wakati huku kwa akina mary waliokuwa wakijiandaa kwa ajili ya harusi ya rafiki yao mpendwa mwanadada mwai, tena walikuwa wana furaha sana kwa rafiki yao kupata mume, lakini sasa mary na rose hawajui kwamba mume wa mwai ndio huyo huyo boss wao,.. Walikuwa wameshonesha sale zao wao wawili kwa jinsi wanavyopendana ila kwenye mapenzi ndio chuki huanzia hapo, lakini kwa kupendana kawaida, sio haba upendo wanao..
"nakwambia mary nina hamu ya kumwona huyo mume wake mana alisema sintokaa kuolewa na janaume la ajabu ajabu, sasa nataka nimjue huyo janaume lenyewe"
"mimi pia nina hamu ya kumuona we acha tu"
Walikuwa wakiongea hivyo huku wakiendelea kujiandaa....
Huku kwa kijana sheby akiwa yupo na baba yake ndani
"sheby mwanangu... Nakuomba sana usije ukanieibisha"
"nikuaibishe na nini tena"
Aliongea sheby kuonyesha sura ya kupenda jambo hilo lakini linamla ndani kwa ndani,..
"hutakiwi kugombana na huyo mwanamke, mpe matumizi yote, akikukosea njoo twende kwa wazazi wake lakini sio kumpiga mtoto wa watu, kuwa makini sana na ndoa yako"
Sasa sheby anashangaa mbona baba yake anamwambia vitu kama hivyo kwanini, yaani mwanamke hata akimkosea amuache,.. Ghafla mama yake katokea
"mama... Mama"
"abee baba"
"mbona baba simuelewi"
"kwanini"
"nasema huyo mwanamke hapigwi"
"ni kweli mwanangu, huyo mwanamke ni mgonjwa, anaanguka kifafa, ukimgusa kwa ngumi umeuwa baba... Huna budi kumuacha"
"sasa mke wa aina hio ni wa nini mimi"
"baba yako ndio kuniambia nije kukwambia"
"mungu wangu, kwahio hata akinitukana nimuache"
"njooo unipe taarifa"
Sasa tukija huku kwa akina zaituni akiwa katulia katika kibanda chake, tena kwa sasa ana kasimu chake,.. Maskini zaituni alikuwa akila viazi vya kuchemsha mana ndio kazi ya mchumba wake atafanyeje,... Ghafla anaingia shadya FUNDI CHEREHANI
"mambo zai"
"safi tu shadi, karibu tule"
"mmnhhh Ahsante"
Lakini kwa muonekano wa shadya alikuwa kang'aa sana, alafu mkononi kashika pesa nyingi sana sasa sijui kazipata wapi...
"heeeeeeee shadi umependeza"
Aliongea zai huku akimuonea wivu mwenzie
"yes, ni mambo ya kujiachia tu.. Nitajibana mpaka lini na wakati najitambua"
Shadya kumbe hakuwa mschana mzuri, kumbe alivaa ngozi ya kondoo na wakati kumbe ni chui,.. Huezi amini kumbe shadya ni mschana anaejiuza, na kutudanganya ni fundi cherehani kumbe ni malaya,.. Kwani hata nguo alioivaa ilikuwa ni fupi na hata yeye mwexnyewe alikuwa akiivuta vuta ili isiwe fupi sana...
"kujiachia Kivipi tena"
"mi nakushangaa unakaa na kijidume kichaafu hakina mbele wala nyuma, pesa ya kuendea kule india yenyewe kakopa sasa hivi anadaiwa weeee, utakufa njaaa"
"lakini shadi mbona sikuelewi shost"
"ona pesa hizi hapa"
"Haaaaaaaaaaaaaaa umetoa wapi pesa zote hizo"
"una sura, una umbo zuri.. Una kila kitu kwanini usipate pesa mtoto wa kike"
Huezi amini shadi kaanza kumharibu mdada wa watu, maskini zai anatamani mavazi aliovaa shadi, anatamani pesa alizonazo shadi
"nitapate sasa"
"sikia... Kuna kijidume kinakuoenda kina pesa chafu.. Vipi sema nikupeleke"
"mmhhhhh lakini shadi"
"lakini nini acha ujinga... Mimi nawagereshea tu hapa lakini nina nyumba yangu mjini"
Mara ghafla simu ya shadi ikaita, sijui nani aliokuwa akipiga
"enheee tena mwanaume mwenyewe huyu hapa anapiga... Sema nimuambieje sasa kuhusu wewe"
Zaituni alianza kujing'ata ng'ata vidole huku akiziangalia zile pesa za shadi....
Je? Zaituni atakubali au atakataa??...