*

TUOMBE*
Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu Muumbaji. Tupo mbele zako asubuhi hii ya leo kukushukuru kwa kutufikisha siku hii ya leo. Sifa, heshima na Utukufu ni kwako.
Tunakuomba tutakase maovu tuliyo tenda kwa kujua na kutokujua. Mungu tuongoze tuweze kufikia kusudi letu maishani na kuliishi kusudi. Mungu wetu Tunaombea Taifa letu,wajane,yatima, waliofungwa kwa hila za mwovu shetani,wagonjwa,Uchumi wetu,Wanafunzi hasa wanaofanya mitihani. Tunaarika Nguvu,Mamlaka na Utawala wa Roho Mtakatifu viwe pamoja nasi katika Jina la Yesu tumeomba Amina.