Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mungu Baba muumba wa Mbingu na nchi, ktk jina la Yesu Kristo. Tunaliinua jina lako kwa utufu wako, tukisema ahsante Baba kwa kuwa tulilala kama wafu. Lakini wewe usiye lala usiku wala mchana,umetuma Malaika wako wakakesha wakitulinda dhidi ya nia ya adui ya kutuangamiza. Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu, Yehova Mungu wetu ndilo Jina lako. Tunasema ahsante kwa wema na fadhili zako zote, ahsante kwa ulinzi na uponyaji wako. Tunajikabidhi tena mikononi mwako siku hii ya leo, ukatuongoze kwa Roho wako Mtakatifu ktk ibada zenye kuabudu ktk Roho na kweli,Ukijidhihirisha Mwenyewe kwa ule Utukufu wa milele Bwana.
Ukaponye na kuokoa kwa Mkono wako ulio hodari.
Wafuatilie pia walio wagonjwa na wenye shida mbalimbali.
Wakiwepo wasafirio leo, basi ukawafuatilie kwa ulinzi wako.
Tunaziombea mamlaka mbalimbali za tawala kote ulimwenguni Palipo na ukatili na zuio la utukufu wako ukatume utiisho wako ili wakujue Wewe wa pekee.
Nimeomba na kushukuru haya yote ktk jina la Yesu Kristo aliye BWANA na Mwokozi wetu, Aaaamin.

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA MBARIKIWE
Ameen mama barikiwa sana
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 41
ILIPOISHIA:
“Habari za saizi nesi,” Raya alimsalimia Shamila kwa unyenyekevu, jambo ambalo hakuwahi kulifanya kabla. Shamila naye akajibu kwa uchangamfu, nikabaki njia panda. Sikujua walizungumza nini muda ule mpaka wakamaliza tofauti zao. Raya akaja mpaka pale kitandani na kunibusu mdomoni, Shamila akageuka na kulishuhudia tukio hilo.
SASA ENDELEA...
Alipogundua kwamba namtazama, harakaharaka Shamila alijifanya kama hakuwa ameona chochote.
“Leo nimekupikia chakula kizuuri, naamini utakipenda,” alisema Raya huku akianza kuniandalia chakula. Nikawa nimetulia pale kitandani huku akilini mwangu mawazo mengi yakipita. Nilikuwa nimeingia kwenye mtego hatari sana ambao sasa ilikuwa ni lazime nifanye kila kinachowezekana kujikomboa.
Njia pekee ambayo ingenisaidia, ilikuwa ni kuhakikisha baba yake Shenaiza na kundi lake lote wanafikishwa mbele ya sheria na mamia ya watu ambao maisha yao yalikuwa hatarini, wanaokolewa kutoka kwenye shimo la mauti.
Ni jambo hilo pekee ndiyo lingenifanya niwe na amani kwa sababu bila kumdhibiti baba yake Shenaiza, maana yake ni kwamba angeendelea kunisaka kwa lengo la kuniua, akiamini tayari kuna siri zake nyingi nazijua, lakini pia maana yake ni kwamba baada ya kunimaliza mimi, angefuatia Shenaiza na baada ya hapo, angeendelea na kazi yake haramu ya kuteketeza maisha ya watu bila huruma.
“Mbona unaonekana kama una mawazo mengi, nini kinakusumbua?” swali la Raya ndilo lililonizindua kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Akaacha kuandaa chakula na kunisogelea, akaniinamia pale kitandani na kunibusu kwenye paji la uso, akawa ananiuliza kwa upole kinachonisumbua.
Mpaka muda huo, Raya hakuwa akielewa chochote kilichokuwa kinaendelea, zaidi ya kufahamu tu kwamba nilikuwa hospitalini nimelazwa baada ya kuvamiwa na majambazi ambao almanusra wayakatishe maisha yangu. Hakuwa anajua ‘connection’ iliyokuwepo kati ya matukio yaliyokuwa yananitokea hata kidogo.
“Kuna jambo linanisumbua sana kichwa changu.”
“Jambo gani mpenzi wangu, si unajua sipendi kukuona ukikosa raha?”
“Najua mpenzi wangu, mambo yamenifika shingoni,” nilimwambia Raya, akazidi kunidadisi ambapo nilimwambia aniandalie kwanza chakula mengine tutaongea baadaye.
Kwa jinsi hali ilivyokuwa, sikuona sababu ya kuendelea kumficha Raya, nilitaka nimueleze ili naye akae akiwa anaelewa kuhusu kipindi kigumu nilichokuwa napitia ili kama kuna msaada wowote anaweza kunisaidia afanye hivyo.
Baada ya kumaliza kuandaa chakula, alinisogezea na kuanza kunibembeleza nile. Kwa jinsi alivyokuwa amepika chakula vizuri, nilikula chote mpaka nikamaliza, jambo ambalo lilimfurahisha sana.
“Enhee, haya niambie sasa,” alisema baada ya kumaliza kutoa vyombo, kama nilivyokuwa nimedhamiria kutoka ndani ya moyo wangu, nilianza kumueleza ukweli wa kila kitu. Jambo pekee ambalo sikumueleza, kama ilivyokuwa kwa Shamila, ni kile kilichonitokea baada ya kupoteza fahamu. Nilihisi naweza kumjaza woga moyoni akaanza kunitazama kwa macho yasiyo ya kawaida.
Nilimficha pia suala la mimi na Shamila kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, nikamwambia kwamba alitokea kuguswa na kilichonipata na kuamua kunisaidia kwa sababu hata yeye kuna ndugu yake amewahi kusafirishwa na shirika hilo na mpaka muda huo hawakuwa na mawasiliano naye. Niliamua kutumia uongo huo ili asishtuke mapema kwamba mimi na Shamila tulikuwa na uhusiano wa kimapenzi
Kiukweli Raya alishtuka sana nilipomueleza kilichokuwa kinaendelea, akawa hataki kuamini, akawa anahisi labda nimeamua kumtungia stori za kumtisha. Nilimhakikishia kwamba kila kitu nilichomwambia ni kweli na kama anataka kuthibitisha, ipo siku atajionea mwenyewe.
Nilimuona Raya akishusha pumzi ndefu, akainua shingo yake akiwa anatazama huku na kule kisha akanigeukia: “Kwa hiyo wewe ulikuwa umeamuaje?”
“Ni lazima nipambane nao.”
“Jamal, umechanganyikiwa nini? Unawezaje kupambana na watu hatari kama hao?”
“Ni lazima nifanye hivyo Raya, sipo tayari kufa kama kifaranga cha kuku mbele ya mwewe, ni lazima nipambane.”
‘Sidhani kama hilo ni jambo sahihi kwa sasa, isitoshe bado hata afya yako haijawa poa, kwa nini tusitafute sehemu nje ya Dar tukaenda kujificha huko na kuanzisha maisha yetu bila mtu yeyote kujua? Mimi nipo tayari hata sasa hivi na naamini nikiwaambia wazazi wangu watakuwa tayari kutusaidia,” alisema Raya, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama.
“Ni lazima nipambane Raya, siwezi kuwakimbia. Najua ni kazi ngumu lakini mwisho wa siku ni bora nife nikiwa napambana,” niliendelea kushikilia msimamo, raya akawa hana cha kuniambia tena.
Bado alikuwa na maswali mengi yaliyokosa majibu ndani ya kichwa chake, akawa ananiuliza kila alipokuwa anakumbuka. Aliniuliza kama watu hao ndiyo walioenda kuvunja nyumba yangu siku ile usiku, nikamjibu kwamba kwa ushahidi huo, inaonesha moja kwa moja kwamba ni wao.
Maswaliyalikuwa mengi mpaka ikabidi nimkatishe, nikamwambia anatakiwa kupeleka vyombo nyumbani ili na yeye apate muda wa kupumzika, nikamuona akisimama kwa shingo upande na kukusanya vitu vyake.
“Nimeongea na daktari, anasema naweza kuruhusiwa ndani ya siku hizi mbili kwa sababu naendelea vizuri.”
“Ooh! Itakuwa vizuri sana, sasa umepanga ukitoka ukaishi wapi?”
“Itakuwa ni siri yangu lakini kwa sasa sitakiwi kukaa pale kwangu kwa sababu najua watakuwa wananiwinda usiku na mchana.”
“Natamani sana tukaishi nyumbani kwetu, wazazi wangu wanakaribia kurudi lakini usijali ile nyumba ni kubwa, wanaweza kukupa hata vyumba vya uani, ukakaa hapo chini ya uangalizi wangu mpaka mambo yatakapotulia.”
“Ahsante sana mpenzi wangu, hivi kazini unaenda kweli wewe?”
“Kazini siendi, nimeomba ruhusa kwamba nakuuguza wewe, kwanza ukiwa kama mfanyakazi mwenzangu na pia ukiwa mume wangu mtarajiwa, kwa hiyo usijali,” alisema Raya huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, akakusanya vitu vyake, akaja kunibusu kisha akaniaga.
Akatoka na kufunga mlango, mara Shamila naye akaingia, ni kama alikuwa amekaa sehemu anasubiri aondoke tu ili na yeye aingie. Akaja uso akiwa ameukunja, nilishaelewa ni kwa sababu gani yupo kwenye hali hiyo.
“Vipi?”
“Mbona unapenda kunitesa Jamal, kwani huyo mwanamke wako huwezi kumkataza kukubusu mbele yangu?”
“Siyo hivyo mpenzi wangu, naomba kaa kwanza tuzungumze.”
“Sitaki, na kwa sababu yeye ameanza basi mimi namaliza,” alisema Shamila na kwenda kufunga mlango kwa funguo, akashusha na mapazia yote, nikawa sielewi alichokuwa anataka kukifanya.
“Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, nilishtuka kumuona akianza kufungua vifungo vya gauni lake la kazini, mara akalivua na kubaki na sidiria na nguo ya ndani tu, ukichanganya na jinsi alivyokuwa amegawanyika na kujaa sehemu za katikati, nilijikuta nikikosa cha kufanya.
“Una..ta..ka kufa...nya ni...ni,” sikumalizia kauli yangu, akawa tayari ameshafikapale kitandani, tukagusanisha ndimi zetu huku Shamila akionesha kweli kudhamiria kile alichokitaka. Hakuogopa kabisa kwamba pale ni wodini.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 42
ILIPOISHIA:
“Una..ta..ka kufa...nya ni...ni,” sikumalizia kauli yangu, akawa tayari ameshafika pale kitandani, tukagusanisha ndimi zetu huku Shamila akionesha kweli kudhamiria kile alichokitaka. Hakuogopa kabisa kwamba pale ni wodini.
SASA ENDELEA...
Nilijaribu kumzuia lakini haikusaidia kitu, alishadhamiria na kwa ilivyoonesha, alikuwa tayari kufanya chochote ili apate alichokuwa anakitaka. Tuliendelea kugusanisha ndimi zetu huku mikono yake laini ikitalii kwenye viunga mbalimbali vya mwili wangu, nikaanza kuhisi hali ya tofauti.
Unajua jambo ambalo nitaendelea kulisema kila siku, hakuna jambo baya kama kuyajaribu mapenzi. Wazee wetu waliosema kwamba mapenzi hayajaribiwi, walikuwa sahihi kabisa. Wakati naanza uhusiano wa kimapenzi na Shamila, nilikuwa najua kabisa kwamba tayari ninaye Raya ambaye ananipenda sana na tumeshaahidiana vitu vingi, tena kibaya zaidi mimi ndiyo nikiwa mwanaume wa kwanza maishani mwake.
Akilini mwangu nilijua kwamba hata nikimkubalia Shamila, haiwezi kuwa na tatizo lolote kwa sababu kiukweli sikuwa nimempenda kutoka ndani ya moyo wangu na nilipanga kumtumia kama daraja tu la kunifanya nipate nilichokuwa nakitaka kwa urahisi.
Hata hivyo, tangu Shamila alipoanza kua karibu na mimi, nilijikuta akiingia kwa kasi kwenye moyo wangu kuliko hata nilivyotegemea. Jambo ambalo sikuwahi kulijua tangu awali ni kwamba kumbe Shamila alikuwa mzuri kuliko Raya, kuanzia mwonekano, shepu, uchangamfu, uelewa wa mambo mpaka kwenye ufundi wa ‘uwanja wa fundi seremala’.
Ilifika mahali mwenyewe nikawa najiona kabisa kwamba nimeanza kumpenda Shamila kuliko Raya, jambo ambalo sikujua mwisho wake utakuja kuwa nini. Nawasihi kwa mara nyingine wanaume, hasa vijana kama sisi, hakuna kosa baya kama kucheza na hisia za wanawake wanaokupenda kwa wakati mmoja.
Basi Shamila aliendelea na mbwembwe, ‘Jamal’ wangu akachaji ile mbaya, nikajikuta mimi ambaye mwanzo nilikuwa navungavunga ndiyo nimekuwa nyota wa mchezo, kwa umakini wa hali ya juu nikajibinua, Shamila akawa chini mimi juu, tukawa tunatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana, kila mmoja pumzi zikimtoka kwa nguvu.
Sikuwa na muda wa kusubiri, nilianza kusakata kambumbu kwa mtindo wa kushambulia mfululizo, huku nikiwa makini nisijitoneshe jeraha langu la kifuani, Shamila akawa anayapokea mashambulizi yangu kwa miguno flan’ hivi ambayo ilizidi kunipandisha wazimu.
Ilifika mahali nikabadili mfumo wa kusakata kabumbu, nikawa nakimbia na mpira kwenye chaki kama Christiano Ronaldo vile, nikawa nahama pande zote na kumfanya Shamila apoteze ‘netiweki’, akaanza kutoa miguno kwa nguvu akiwa amesahau kabisa kwamba hatukuwa kwenye mazingira rafiki.
Niliongeza kasi, naye akaongeza kasi ya kunikaba, dakika chache baadaye nilitangaza kuzifumania nyavu zake lakini kabla sijamuwahi, na yeye alishatangaza kuzifumania zangu, ikawa ngoma droo!
Harakaharaka nilishuka pale kwenye kitanda changu na kuvaa vizuri nguo zangu ambazo hata sikumbuki nilizitupa saa ngapi sakafuni. Harakaharaka nikajiweka vizuri na kumsogelea Shamila ambaye eti tayari alikuwa ameanza kukoroma kwa mbali, akionesha kuchoshwa mno na mpambano ule wa kushtukiza.
Nikamtingisha kwa nguvu, akawa ananisukuma kama anayesema ‘niache nipumzike bwana’. Nilipozidi kumsumbua, aliinuka, naye akavaa magwanda yake, safari hii akiwa hataki kabisa kunitazama usoni. Akajizoazoa mpaka kwenye ofisi ya manesi ambako nako kulikuwa na kitanda, akajitupa kitandani.
Ilibidi mimi ndiyo niwe na kazi ya ziada ya kuondoa ushahidi wote eneo la tukio, nikaenda kufungua mapazia, nikafungua na milango na kuiweka kama inavyotakiwa kuwekwa, nikaongeza spidi ya feni na kurudi kitandani, nikajilaza huku moyoni nikijipongeza kwa kumtolea uvivu Shamila ambaye alikuwa akicheza na sharubu za simba.
Muda mfupi baadaye, niliona kivuli cha mtu akipita dirishani kwa nje, akaenda upande mmoja kisha muda mfupi baadaye akarudi na kusimama pale mlangoni, ilionesha kama ni mtu ambaye hakuwa na uhakika sana wa mahali anakokwenda. Kwa kuwa pale nje ya wodi za ‘private’ kulikuwa na walinzi, nilisikia wakimsemesha.
Kama kawaida yangu, nikawahi kujihami kwa kushuka pale kitandani haraka na kwenda kujibanza nyuma ya mlango ili hata kama ni miongoni mwa wale wanaoisaka roho yangu, akiingia tu niwahi kuchomoka.
Katika mahojiano yake, niligundua kwamba ni msichana, tena bado mdogo na alikuwa akitaka kuniona mimi maana niliwasikia akiwatajia mpaka jina langu. Baada ya kumhoji sana, wale walinzi walimruhusu kuingia, nadhani ni kwa sababu walishapewa maelekezo na Shamila juu ya kuwa makini na watu wanaokuja kwa lengo la kuniona. Akafungua mlango na kuanza kuangalia juu ya vitanda viwili vilivyokuwa ndani ya wodi hiyo.
“Firyaal,” nilisema baada ya kumtambua kuwa ni yule mdogo wake Shenaiza ambaye nilipewa maagizo ya kwenda nyumbani kwao kuonana naye, ambaye ndiye aliyenipa ‘hard disk’ iliyokuwa na siri nyingi kuhusu ushetani uliokuwa ukifanywa na baba yake.
“Jamal! Alisema huku akitetemeka, uso wake ukionesha dhahiri jinsi alivyokuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.
“Vipi mbona hivyo? Tulia kisha uniambie nini kinachokusumbua,” nilisema huku nikifunga mlango na kusogea naye mpaka pale kwenye kitanda changu.
“Baba anatarajiwa kurudi kesho nchini na tayari walinzi wake wamegundua kwamba kuna kitu kwenye kompyuta yake kimechomolewa, wakijua kwamba mimi na dada Shenaiza tunahusika hata sijui itakuwaje.
“Nipo chini ya miguu yako nakuomba unirudishie ile ‘hard disk’, nimefanya kazi kubwa sana kukutafuta, hospitali nzima hawajui umelazwa wodi gani,” alisema Firyaal, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama.
“Usijali Firyaal kila kitu kitakuwa sawa,” nilimwambia na kuanza kumtuliza, nikamhakikishia kwamba kabla ya hiyo kesho, ataipata ‘hard disk’ yake, pia nikamwambia kuhusu matatizo yaliyokuwa yanamkabili dada yake.
“Tusaidie kama unaweza, najua baba akija maisha ya dada yapo hatarini sana, anaweza hata kuamuru auawe, yaani sijui baba siku hizi amekuwaje,” alisema Firyaal huku akianza kuangua kilio. Niliendelea kumtuliza huku nikitafuta mbinu ya kuwasaidia wote kwani kwa jinsi ilivyoonesha, baba yao alikuwa mtu hatari hata ndani ya familia yake mwenyewe.
Nadhani mazungumzo yetu yalimzindua Shamila aliyekuwa usingizini, akakurupuka na kutoka, akapigwa na butwaa kumuona mdogo wake Shenaiza. Alimkumbuka vizuri kwa sababu hata siku niliyoenda kuichukua ile ‘hard disk’, nilikuwa nimeongozana naye ingawa yeye alibaki ndani ya teksi.
“He, vipi imekuwaje? Binti nani amekuruhusu kuingia humu?” alihoji Shamila huku akijiweka vizuri nguo zake pamoja na nywele ambazo bado zilikuwa zimevurugika. Ilibidi nimtulize na kumweleza kilichomleta pale. Kwa bahati nzuri Shamila ni mwelewa sana, harakaharaka alielewa, kwa pamoja tukawa tunajadiliana nini cha kufanya.
“Inabidi kwanza hiyo ‘hard disk’ yake irudishwe haraka kisha baada ya hapo inabidi tufanye mpango wa kumtorosha Shenaiza wodini haraka iwezekanavyo, hayo yote yanatakiwa kufanyika usiku wa leo.
“Hata wewe hapa siyo mahali salama tena pa kuendelea kukaa, ngoja kwanza nimesahau kuuliza kitu muhimu. Wewe binti upo upande upi? Unamuunga mkono baba yako au na wewe unamsimamo kama wa dada yako?” Shamila alimuuliza swali muhimu.
Msichana huyo mdogo alituhakikishia, tena kwa kujiapiza kwamba kamwe hajawahi kumuunga mkono baba yake lakini amekuwa akikosa mtu wa kumsaidia kupambana naye.
Kauli yake hiyo ilitufurahisha sana mimi na Shamila, tukawa na uhakika kwamba sasa kazi itakuwa nyepesi kwa sababu tayari tutakuwa na mtu kutoka ndani kabisa, ambaye angetusaidia kutimiza lengo letu la kupambana na mtu huyo hatari.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 43
ILIPOISHIA:
Kauli yake hiyo ilitufurahisha sana mimi na Shamila, tukawa na uhakika kwamba sasa kazi itakuwa nyepesi kwa sababu tayari tutakuwa na mtu kutoka ndani kabisa, ambaye angetusaidia kutimiza lengo letu la kupambana na mtu huyo hatari.
SASA ENDELEA...
“Kwa hiyo tunaanzia wapi?” nilimuuliza Shamila, akawa ni kama anayetafakari kitu kisha akaniambia ameshapata majibu.
“Ngoja niende kwanza na huyu binti nikampe hiyo hard disk yake,” alisema Shamila.
“Utaweza kuichomoa kwenye kompyuta?”
“Mimi naweza, nasomea Information Technology niko mwaka wa pili,” alisema Firyaal ambaye alikuwa amefanana sana na Shenaiza, yaani hata bila kuuliza ungemjua tu kwamba ni ndugu yake.
“Sijamaliza kukopi data ninazozihitaji lakini.”
“Nitakusaidia pia, ninayo ‘back up’ kubwa tu nyumbani, naweza kuhamisha data zote na kukuletea,” alisema msichana huyo, nikawa namtazama usoni kwani aliyokuwa akiyasema hayakuwa yakifanana na umri wake.
Kwa kumtazama alionekana kama msichana mdogo ambaye kwa makadirio ungeweza kudhani yupo kidato cha pili au cha tatu lakini kumbe tayari alishafika kidato cha sita na sasa alikuwa chuoni.
“Nitashukuru sana ukinisaidia dada’angu,” nilisema kwa sauti ya kiungwana, Firyaal akanitazama usoni, na mimi nikamtazama, macho yetu yakagongana, harakaharaka akakwepesha macho yake huku aibu za kikekike zikiwa zimemtawala.
“Basi usitoke kwenda sehemu yoyote, mimi ngoja niende naye nyumbani,” alisema Shamila, akanisogelea pale kitandani na kunibusu kisha harakaharaka akamshika mkono Firyaal na kuanza kutoka naye nje.
Walipofika mlangoni, nilimuona Firyaal akigeuka na kunitazama, na mimi nikamtazama, macho yetu yakagongana kwa mara nyingine. Tofauti na mwanzo, safari hii hakukwepesha macho yake, tukaendelea kutazamana mpaka walipotoka nje. Sikuelewa sababu iliyofanya awe ananitazama vile kwa sababu kimsingi hiyo haikuwa mara ya kwanza mimi na yeye kuonana.
Ilikuwa ni mara ya pili. Hata hivyo sikutilia sana maanani, nikampotezea.
Nikashusha pumzi ndefu na kutulia kitandani, mawazo mengi yakiendelea kupita ndani ya kichwa changu. Ni kweli nilikuwa bado sijapona vizuri lakini ilikuwa ni lazima niondoke hospitalini hapo kabla mambo hayajaharibika. Kutokana na sifa nilizokuwa nazisikia, nilijikuta nikimuogopa mno baba yake Shenaiza kama malaika mtoa roho.
Niliendelea kutulia pale kitandani, japokuwa Shamila aliniambia nisitoke, nilipata wazo la kwenda kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Shenaiza kwenda kuangalia anaendeleaje. Hata hivyo, nilipomkumbuka yule mtu aliyekuwa akinitazama sana kwa makini mle ndani ya wodi ya vichaa, nilijikuta nikipatwa na hofu moyoni, nikaghairi.
Kwa hesabu zangu za harakaharaka ukichanganya na maelezo niliyoyapata kutoka kwa Shamila, nilikuwa nimekaa hospitalini hapo kwa wiki mbili mfululizo, huku kati ya hizo, siku saba nikiwa nimepoteza kabisa fahamu.
Nilijaribu kuvuta kumbukumbu ya mambo yote yaliyotokea ndani ya kipindi hicho nilichokuwa hospitalini hapo, ungeweza kudhani kama nimekaa hospitalini kwa kipindi cha mwaka mzima. Kila kitu kilikuwa kikitokea kwa kasi kubwa mno kiasi cha kufanya hata akili yangu isipate muda wa kupumzika.
Kitu ambacho kilinipa faraja kubwa ndani ya moyo wangu, ni kuona jinsi wafanyakazi wenzangu pamoja na bosi wetu walivyokuwa wakinijali. Japokuwa nilikuwa chini ya uangalizi maalum ambapo watu hawakuwa wakiruhusiwa kuja mara kwa mara kunitazama, Raya alinihakikishia kwamba katika zile siku nilizokuwa nimepoteza fahamu karibu kila siku watu kutoka kazini walikuwa wakija kunitazama.
Baada ya kama dakika arobaini tangu Shamila na yule mdogo wake Shenaiza waondoke, Raya alikuja tena. Kiukweli japokuwa nilikuwa nikimuendea kinyume, Raya alikuwa akijitahidi sana kuwa karibu na mimi.
Muda wote yeye alikuwa akinifikiria mimi tu kiasi cha kumfanya kazini asiwe anaenda wala nyumbani kwao asiwe anatulia, muda wote ilikuwa ni kiguu na njia, kuja hospitali na kurudi kwao.
“Vipi unaendeleaje mume wangu,” alisema Raya kwa sauti ya chini, akionesha kuwa na mawazo lukuki ndani ya kichwa chake.
“Naendelea vizuri mke wangu, vipi mbona nakuona kama mudi yako iko chini sana, nini kinakusumbua,” nilimwambia Raya kwa upole, akajisogeza na kupitisha mkono wake mmoja shingoni kwangu, akanibusu kwenye paji langu la uso na kuanza kuniambia kwamba tangu nilipomweleza ukweli wa kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia, alikosa raha kabisa.
“Nahisi kama nitakupoteza mpenzi wangu na mimi siwezi kuishi bila wewe, hata sijui itakuwaje,” alisema kwa huzuni, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kumtuliza. Nikamwambia asiwe na wasiwasi, hakuna jambo lolote baya litakalotokea nakuhakikishia,” nilimwambia.
Kidogo kujiamini kwangu kulimfanya naye aanze kuona kwamba kumbe halikuwa tatizo kubwa mbele yetu, nikamueleza pia juu ya mipango ya kutoroka tuliyokuwa tumeipanga kwa ajili ya kumkimbia baba yake Shenaiza. Nilimuona naye akiniunga mkono, nadhani hata yeye hakuwa na imani kabisa juu ya usalama wangu hospitalini hapo.
Tulizungumza mambo mengi, Raya akawa ananisisitiza kwamba yeye amejitoa kwa asilimia mia moja kunisaidia, isije ikatokea kwamba nikamgeuka na kumuona hana maana tena. Kauli yake iliugusa sana moyo wangu kwa sababu ni kweli Raya alikuwa amejitoa kwa kila kitu lakini kwa bahati mbaya sana shetani alionekana kunizidi nguvu.
Nikawa namhakikishia kwamba asiwe na wasiwasi lakini ukweli, sikuwa namaanisha kile nilichokuwa nakisema. Akaniambia kwamba atashirikiana na Shamila kuhakikisha wananitorosha hospitalini hapo usiku bila mtu yeyote kujua, swali likawa nikishatoroshwa nitaenda kukaa wapi?
Raya alisema anataka nikakae nyumbani kwao kwa sababu pale kuna usalama zaidi, nikamwambia ni rahisi wabaya zangu kujua kwamba niko pale kwa sababu kuna baadhi ya watu walikuwa wakijua kuhusu uhusiano wetu wa kimapenzi. Nikatumia nafasi hiyo kumpigia chapuo Shamila, nikamwambia Raya kwamba amesema yupo tayari kunificha nyumbani kwake.
Nilimuona Raya akishtushwa kidogo na nilichokisema lakini nikamtoa wasiwasi na kumwambia kwamba mimi na yeye tutakuwa pamoja kwa hiyo asiwe na wasiwasi wowote. Akakubali kwa shingo upande, nadhani bado alikuwa na wivu juu ya ukaribu wangu na Shamila.
Muda ulizidi kuyoyoma, baadaye Shamila alirudi akiwa peke yake, akaniambia kwamba kila kitu kimeenda kama tulivyokubaliana, akaniambia kwamba Firyaal alikuwa mtundu sana kwenye mambo ya kompyuta na kwamba tayari alishanikopia data zote na kuziacha pale nyumbani kwake kama tulivyokubaliana, tukaanza kupanga mipango ya namna ya kutoroka usiku huku Raya naye akiwepo.
Jambo ambalo kuanzia mwanzo Raya hakuwa akilijua, ni kwamba katika mpango wetu huo ilikuwa ni lazima pia tumtoroshe na Shenaiza, akashtuka kusikia hivyo.
Bado nikaendelea kumsisitiza kwamba ilikuwa ni lazima tuondoke na Shenaiza kwa sababu bila yeye mimi nisingeingia kwenye mtego huo na kuanzia mwanzo alikuwa akinisisitiza kwamba mimi ndiye mtu pekee ninayeweza kumsaidia.
“Usiwe na wasiwasi, hawa wote wataenda kukaa nyumbani kwangu, mimi nina nyumba kubwa, hata na wewe ukitaka tukae pamoja tusaidiane kuwahudumia wagonjwa haina shida,” alisema Shamila, nikamuona Raya akishusha pumzi ndefu na kunitazama, akatingisha kichwa kama ishara ya kukubaliana na mimi.
Ilibidi Raya abaki palepale hospitalini mpaka usiku ili iwe rahisi kufanya kazi yetu, muda ukazidi kuyoyoma na hatimaye giza likaingia, ule muda tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu ukawa umewadia.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 44
ILIPOISHIA:
Ilibidi Raya abaki palepale hospitalini mpaka usiku ili iwe rahisi kufanya kazi yetu, muda ukazidi kuyoyoma na hatimaye giza likaingia, ule muda tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu ukawa umewadia.
SASA ENDELEA...
“Tunakusikiliza wewe Shamila!”
“Yaah! Inabidi mnisikilize kwa makini vinginevyo hakuna kitakachofanikiwa.”
“Tunaanzia wapi?” nilimuuliza Shamila huku mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio.
“Tulia Jamal, mbona una haraka namna hiyo,” alisema Shamila, nikashusha pumzi ndefu na kutulia, hakuna muda ambao nilikuwa nahitaji msaada wake kama huo na kubwa zaidi, sikuwa mimi tu ambaye nilikuwa nahitaji msaada wake, bali Shenaiza pia.
Shamila aliingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo, muda mfupi baadaye alitoka akiwa na gauni jingine, akampa Raya na kumuelekeza kuingia kule ndani kwenda kubadilisha nguo. Kweli akatii alichoambiwa, muda mfupi baadaye akatoka akiwa ndani ya mavazi ya kinesi, usingeweza kumtambua kwamba hakuwa nesi.
“Sasa wewe kazi yako itakuwa ni kutoka na mgonjwa mpaka nje, unaona hili faili lake, inatakiwa ulishike na kufuata maelekezo ya nitakachokuwa nakwambia. Ukikosea tu basi hakuna kitakachowezekana,” alisema Shamila wakati akimpa maelekezo Raya, akatingisha kichwa kwa utiifu kuonesha kwamba alikuwa ameelewa alichokuwa ameambiwa.
“Inabidi pia njia ambayo itatumika kukutoa wewe itumike pia kwa Shenaiza, tena kwa wakati mmoja kwa hiyo tutaongozana wote, sijui kama mnanielewa,” alisema Shamila huku akiwa amevaa uso wa ‘usiriaz’, wote tukaitikia kuonesha kwamba tulikuwa tumemuelewa.
“Mimi nitaenda kumchukua Shenaiza wakati huo nyie mtakuwa mkinisubiri hapo chini, tutatoka pamoja mpaka pale getini, mimi nitaongea na walinzi, wakituruhusu kutoka tu, Firyaal yupo nje anatusubiri na gari la familia yao kwa hiyo hakutakuwa na muda wa kupoteza, tumeelewana?” alisema Shamila ambaye aligeuka na kuwa mwalimu wa kutuelekeza, sisi kazi yetu ikawa ni kuitikia tu.
“Nifuate,” alimwambia Raya huku akinitaka na mimi nivae vizuri nguo maalum za wagonjwa.
“Kamanda, huyu mgonjwa inatakiwa akafanyiwe kipimo cha MRI kesho sasa kwa sababu mashine ya hapa hospitalini ni mbovu na kesho kutakuwa na foleni kubwa, tumeomba akafanyiwe kipimo hicho usiku huu pale kwenye maabara za Lancert zilizopo nje ya hospitali,” Shamila alimwambia mlinzi aliyekuwa nje ya wodi ile kwa sauti ya juu, japokuwa mimi nilikuwa ndani niliweza kusikia kila kitu, nikatabasamu na kutikisa kichwa kwani ama kwa hakika mbinu ya Shamila ilikuwa kali mno.
Muda mfupi baadaye, nilisikia mlango ukifunguliwa, Shamila akatangulia kuingia, nyuma yake akafuatia Raya aliyekuwa akisukuma kiti cha magurudumu (wheel chair) huku akionesha dhahiri jinsi alivyokuwa na hofu kubwa moyoni mwake.
“Inatakiwa uchangamke, ukiwa unatetemeka hivyo watatushtukia, muone kwanza,” Shamila alimshushua Raya kwa sauti ya chini, nikanyamaza kimya kama sijasikia chochote. Wakasogeza ile wheel chair mpaka pale pembeni ya kitanda changu, Shamila akaniambia anajua ninao uwezo wa kutembea mwenyewe lakini ni lazima nikubali kusukumwa kwenye kiti cha magurudumu ili isiwe rahisi kwa mtu yeyote kutushtukia.
Basi nikashuka kitandani na kukaa kwenye kitanda cha magurudumu, Shamila akamuelekeza Raya namna ya kukisukuma na akarudia kumsisitiza kwamba anatakiwa kuchangamka. Ilibidi vitu vyangu vingine vyote niviache mlemle wodini, tukatoka mpaka kwenye korido, nikamuona yule mlinzi akisimama na kutusaidia kubonyeza kitufe kwenye lifti.
Hakuwa na mawazo kabisa kwamba ndiyo tunamtoka kiaina. Nikiri wazi kwamba hilo halikuwa zoezi langu la kwanza kutoroka hospitalini kwa sababu tayari nilishamtorosha Shenaiza lakini hali haikuwa tete kama ilivyokuwa muda huo, na kikubwa kilichokuwa kikinipa hofu kubwa ndani ya moyo wangu ni kujua aina ya watu niliokuwa nadili nao; baba yake Shenaiza na watu wake.
“Inawezekana kabisa kuna watu wamepandikizwa hapa hospitalini na baba yake Shenaiza kufuatilia nyendo zako na binti yake, kwa hiyo unatakiwa kujiinamia muda wote ili mtu yeyote asikuone usoni, mtanisubiri nikamchukue Shenaiza,” alisema Shamila wakati tukiwa ndani ya lifti tukishuka chini, tukamuitikia.
Tulishuka mpaka chini, akatuelekeza kufuata korido mpaka mbele ambapo alisema tumsubiri, Raya akawa ananisukuma taratibu, yeye akaelekea kwenye wodi ya wagonjwa wa akili alikokuwa amelazwa Shenaiza.
“Im scared Jamal, I cant take it!” (Naogopa Jamal, siwezi!)
“You need to do this my love, do it for me!” (Unatakiwa kufanya mpenzi wangu, fanya kwa ajili yangu) Raya alinisemesha kwa Kimombo si unajua tena yeye alikuwa akitoka familia bora? Nikawa naendelea kumpa maneno ya kumtia nguvu, tukawa tunaendelea kutembea taratibu kwenye korido huku Raya pia akiwa na faili langu.
“Hivi akitokea mlinzi hapa na kutuuliza tunaenda wapi usiku huu tutajibu nini?”
“Tunaenda kufanyiwa kipimo cha MRI pale nje kwenye maabara za Lancert kwa sababu mashine za humu ndani zimeharibika,” nilijibu kwa kujiamini, nikaona hofu ikipungua ndani ya moyo wake.
“Maelezo haya inabidi wewe nesi ndiyo uyatoe, sio mimi mgonjwa,” nilisema kwa msisitizo, Raya akawa ananiitikia lakini jambo ambalo bado hakuweza kulidhibiti, ni hofu iliyokuwa ndani ya moyo wake.
Tulifika mpaka pale Shenaiza alipotuambia kwamba tumsubiri, tukasimama na kuanza kuangalia uelekeo wa wodi ya wagonjwa wa akili alikokuwa ameelekea. Hata hivyo, hakutokea haraka kama tulivyodhani, muda ukaanza kuyoyoma mara dakika tano zikakatika, kimya! Tano nyingine zikakatika bila Shamila kurudi, tukaanza kuingiwa na hofu.
Pale tulipokuwa tumesimama, wauguzi na ndugu za wagonjwa mbalimbali walikuwa wakitupita lakini hakuna aliyekuwa na habari na sisi kwani walijua tupo kwenye taratibu za kawaida za tiba.
“Tunavyozidi kusimama hapa ndivyo tunavyozidi kujiweka kwenye hatari zaidi, wanaweza kutushtukia.”
“Sasa tufanyeje?” nilimuuliza Raya lakini kama bahati, kwa mbali tuliona mlango wa wodi ya wagonjwa wa akili ukifunguliwa, Shamila akatoka akiwa anasukuma kitanda cha magurudumu kama kile nilichokuwa nimekalia, wote tukashusha pumzi ndefu na kumshukuru Mungu kwani tulishaanza kuchanganyikiwa.
Kwa mbali akatuonesha ishara kwamba tuendelee kusonga mbele, naye akawa anakuja huku akikisukuma kile kitanda ambacho hata bila kuuliza, niligundua kwamba aliyekuwa amekaa pale alikuwa ni Shenaiza.
Akazidi kutukaribia na muda mfupi baadaye, tayari alikuwa ametufikia, tukawa tunatembea bila yeyote kati yetu kumsemesha mwenzake. Kwa watu ambao hawakuwa wakielewa kinachoendelea, wangedhani kwamba ni manesi walikuwa wakiwapeleka wagonjwa wao kupata matibabu ya kawaida.
Kwa mbinu ile ilikuwa vigumu sana kwa mtu yeyote kutushtukia, tukazidi kusonga mbele huku nikijitahidi kuibia macho pembeni na kumtazama Shenaiza ambaye alikuwa amekaa kwenye kiti cha magurudumu akiwa haelewi chochote kilichokuwa kinaendelea.
Nguo maalum aliyofunikwa upande wa kichwani, ilifanya iwe vigumu kwa mtu yeyote kumtambua, tukaendelea kusonga mbele mpaka tulipofika kwenye geti la kutokea nje ya hospitali, hapo tukakumbana na kipingamizi ambacho hakuna aliyekitegemea, mapigo ya moyo wangu yakawa yananienda mbio kuliko kawaida.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Seven Days ih Hell (Siku Saba Kuzimu)- 46
ILIPOISHIA:
“Ulisema unasomea IT, hebu chukua ile laptop pale uje hapa unisaidie kitu,” nilimtega, naye ni kama alikuwa akiisubiri nafasi hiyo, harakaharaka aliinuka pale alipokuwa amekaa, akaenda kuchukua laptop ya Shamila na kuja nayo kwenye lile kochi nililokuwa nimekaa, akaja kukaa karibu kabisa na mimi kiasi cha kunifanya niwe nalisikia joto la mwili wake, lililonakshiwa kwa manukato mazuri aliyokuwa amejipulizia.
Mara mlango wa jikoni ukafunguliwa.
SASA ENDELEA...
“Vipi?” Shamila aliuliza huku akiwa ni kama ameshtuka f’lani hivi kuniona nikiwa nimekaa jirani namna ile na Firyaal.
“Kuna kazi namuelekeza anisaidie.”
“Ooh! Tena huyo atakufaa zaidi, si amesema anajuajua mambo ya IT?”
“Ndiyo japo bado sijathibitisha,” nilisema huku nikijifanya kumkandamiza Firyaal ili kuua soo, naye ni kama alijua kilichokuwa ndani ya akili yangu, akatulia kiasi cha kufanya iwe vigumu kwa Shamila kuelewa kilichokuwa kikiendelea kati yangu na msichana huyo mdogo lakini mrembo.
Akaenda kwenye friji na kuchukua baadhi ya vifaa kisha akarudi jikoni, akaniacha nikiwa bize nikijifanya namuelekeza kitu Firyaal ambaye naye alikuwa akiitikia kwa umakini, alipoingia jikoni tukatazamana.
“Hapa siyo sehemu sahihi, watatushtukia sasa hivi,” nilimnong’oneza, harakaharaka akanikubalia kwa kutingisha kichwa. Nikamwambia anisaidie kutafuta majina ya watu wote ambao walikuwa ‘wamesaidiwa’ na Shirika la Black Heart lililokuwa likiongozwa na baba yake kwenye zile data tulizoziiba kwenye ile ‘hard disk’ aliyonipa.
Akahama pale alipokuwa amenifuata na kurudi kwenye kiti chake, akajiinamia kwenye laptop na kuanza kufanya ile kazi niliyomuagiza. Shamila alitoka tena jikoni na alipoona kweli Firyaal amejiinamia na kompyuta, wala hakuhisi jambo lolote baya, akawa ananitazama kwa macho fulani hivi ambayo nilimuelewa alichokuwa anamaanisha.
Firyaal aliendelea na kazi, Shamila na Raya nao waliendelea na kazi, mimi nikawa nimekaa zangu pale kwenye kochi nikiwa naendelea kuwaza hili na lile. Nikiri wazi kwamba kabla ya matatizo hayo hayajaanza kunikumba, sikuwa napenda kukaa karibu na wasichana kabisa, yaani kama ungekuja kwangu, kama usingenikuta natazama ‘movie’ basi ungenikuta nacheza gemu za ‘Playstation’.
Tangu nilipoanza kukutana kimwili na Raya, akili zilikuwa ni kama zimezibuka, nikawa najilaumu kwa kuchelewa kuvumbua ‘hazina’ iliyojificha kwa kipindi chote hicho. Kabla sijaendelea, naomba niliweke wazi hili kwa manufaa ya wengine. Wanaume wengi huwa wanaharibikiwa maishani kwa sababu ya kuruka vipengele fulani katika hatua za ukuaji.
Unakuta mtu ule muda ambao alitakiwa afanye mambo ya ‘kitoto’ yeye anakuwa bize na masomo au kazi. Akishaingia kwenye ndoa ndiyo anazibuka na kuanza kuona kama alikuwa anachelewa, matokeo yake ndiyo unakuta mwanaume ana mke mzuri lakini kila siku anasaliti ndoa yake kwa sababu kuna hatua ya ukuaji aliiruka.
Muda mfupi baadaye, chakula kilikuwa tayari, Raya na Shamila wakaandaa chakula, Raya akiwa hajui kabisa kwamba aliyekuwa akishirikiana naye kwa kila kitu alikuwa ni ‘mke mwenzie’, Firyaal naye akijifanya anawaheshimu sana dada zake hao kumbe na yeye alikuwa akijilengesha kwangu.
Baada ya kumaliza kuandaa, tulianza kula huku Shamila akitusisitiza kwamba tusiwe na wasiwasi kuhusu Shenaiza, akatuambia kwamba atamshughulikia na baada ya muda mfupi atarejewa na fahamu zake. Sote tulikuwa kimya kabisa, mtu pekee aliyekuwa akizungumza alikuwa ni Shamila.
Baada ya kumaliza kula, tulikaa pamoja sebuleni hapo na kuanza kupanga namna ya kukabiliana na baba yake Shenaiza. Nilimuuliza Firyaal amefikia wapi kwenye kazi niliyompa, akaniambia ameshapata majina ya watu wote waliosaidiwa na shirika hilo pamoja na anuani zao za makazi pamoja na ndugu zao waliokuwa hapa nchini.
“Basi naomba uunganishe na yale majina ambayo nilishayapata kuanzia mwanzo,” nilisema, Firyaal naye akaitikia kwa adabu kabisa, watu wote wakazidi kutuamini kwamba kweli tulikuwa kikazi zaidi.
Bado ule mchezo wake wa kunitazama kwa kuibia hakuwa ameuacha lakini kwa kuwa sasa Raya na Shamila walikuwa pale sebuleni, nilijifanya sijui chochote kinachoendelea kwa sababu nilihofia wanaweza kutufuma tukitazamana halafu wakatufikiria vibaya.
Tuliendelea kupanga mipango yetu na mwisho tukakubaliana kwamba kwa kuwa ushahidi wote tayari tulikuwa nao, twende tukatoe taarifa polisi ili watusaidie kupambana na genge hatari la baba yake Shenaiza.
Kilichonipa moyo kwamba kila kitu kitafanikiwa, ni jinsi Firyaal alivyoonesha kuchukizwa na vitendo vya baba yake, akatuhakikishia kwamba japokuwa anajua baba yake anaweza hata kufungwa, yupo tayari kwa chochote mpaka tufanikiwe.
Wazo hilo lilipitishwa, tukakubaliana kwamba usiku ule Shamila anatakiwa kurudi kule hospitalini ili kuhakikisha hakuna anayeshtukia kama mimi na Shenaiza tumetoroshwa hospitalini, na asubuhi na mapema ya siku inayofuatia, mimi nitaongozana na Raya mpaka kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya kwenda kutoa taarifa.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeshaenda, Shamila alimwambia Firyaal amrudishe mpaka hospitalini kwa kutumia gari lake kisha arudi nyumbani kwao, Kurasini ili asije akashtukiwa lakini msichana huyo alikataa katakata, akasema alishamuaga mama yake kwamba anakwenda kwenye ‘birthday’ ya rafiki yake na kwamba hatarudi mpaka asubuhi na aliruhusiwa.
“Twende nikupeleke wewe kazini mi nitakuja kulala hapahapa na dadaa’ngu Shenaiza,” alisema, Shamila na Raya wakamkubalia bila kujua kwamba kuna kitu alichokuwa anakifuata.
Raya naye alipoulizwa kama atarudi nyumbani kwao, naye alisema atakaa na mimi mpaka asubuhi ya kesho yake. Shamila alikubali ingawa nilimuona kama wivu unamsumbua sana, akainuka na kwenda kuanza kuandaa mazingira ya sisi sote kulala.
Mimi aliniandalia kwenye chumba cha peke yangu, Firyaal akamwambia atalala na dada yake kwenye chumba cha wageni na Raya atalala kwenye chumba chake, wote tukamkubalia kwani kwa wakati huyo yeye ndiye aliyekuwa bosi wetu.
Alienda kuoga na kuanza kujiandaa kisha akatuaga na kututaka tuwe makini, hasa mimi, akatoka na Firyaal kuelekea hospitali huku akiniachia maagizo kwamba Firyaal akirudi, nikamsaidie kufungua geti aingize gari kisha baada ya hapo, nifunge milango yote na kuzima taa zote za ndani na nje, nikamkubalia.
Walipotoka, ndani nilibaki na Raya tu ambaye ilionesha alikuwa na hamu kubwa ya mimi na yeye kubaki wawili tu. Alipohakikisha wameshaingia ndani ya gari na kuondoka, harakaharaka alinifuata na bila kuzungumza chochote, alianza fujo zake akitaka nikamalizane naye fasta kabla Firyaal hajarejea.
Hata hivyo, kwa kuwa tayari nilikuwa na ratiba nyingine kichwani, nilimdanganya kwamba siku hiyo nilikuwa nimechoka sana na jeraha langu lilikuwa likima kwa sababu ya purukushani za kutwa nzima, nikamuomba kama hatajali, tukapumzike kwanza mpaka baadaye.
Nilimuona akikubali kwa shingo upande, akaenda kuoga na kuniacha niko pale sebuleni najifanya niko bize na laptop. Baada ya kumaliza kuoga alinifuata tena, nikaendelea kumsisitizia kwamba hali yangu haikuwa nzuri, akaniomba basi tukalale kitanda kimoja ambapo pia nilimkatalia na kumwambia nitamfuata usiku sana wakati Firyaal ameshalala ili tusije kuonesha picha mbaya.
“Basi naacha mlango wazi,” alisema, nikatingisha kichwa kuonesha kumkubalia, akaondoka kwa shingo upande na kwenda kulala. Kutokana na uchovu aliokuwa nao wa pilikapilika za kutwa nzima, hakuchukua raundi, akapitiwa na usingizi mzito.
Nusu saa baadaye, alikuwa akikoroma, hata niliponyata na kwenda kumchungulia, alionesha ameshalala fofofo, moyoni nikawa nachekelea. Harakaharaka nilienda kwenda chumba nilichopangiwa kulala, nikaingia bafuni na kujimwagia maji kupunguza uchovu kisha nikatoka na kwenda kukaa sebuleni nikimsubiri Firyaal kwa shauku kubwa, nikiwa nimejifunga taulo tu! Shetani wa mahaba alikuwa amenizidi nguvu.
Dakika kadhaa baadaye, nikasikia honi ya gari, harakaharaka nikatoka na kwenda kufungua geti, alikuwa ni Firyaal, aliponiona nimejifunga taulo tu, alijifanya kushtuka kisha nikamuona akitabasamu, akaingiza gari na kulipaki, nikafunga mageti kama Shamila alivyoniagiza, tukaingia ndani na kwenda mpaka sebuleni.
“Dada Raya yuko wapi?” aliuliza Firyaal kwa sauti ya chini, nikamwambia ameshalala na sasa anakoroma, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kunitazama usoni, tukawa tunatazamana.
“Nataka nikalale na dada Shenaiza,” alisema kwa sauti ya kudeka huku akinisogelea na kujilaza kifuani kwangu, nikapitisha mkono wangu na kumshika kiunoni, nikamuona akiruka kama aliyepigwa na shoti ya umeme.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
Seven Days in Hell (Siku Saba Kuzimu)- 47
ILIPOISHIA:
“Nataka nikalale na dada Shenaiza,” alisema kwa sauti ya kudeka huku akinisogelea na kujilaza kifuani kwangu, nikapitisha mkono wangu na kumshika kiunoni, nikamuona akiruka kama aliyepigwa na shoti ya umeme.
SASA ENDELEA...
“No! Usifanye hivyo,” alisema Firyaal huku akinitoa mkono kwa staili ya ‘sitaki nataka’, nikamvutia kwangu na kusababisha tuwe tunatazamana katika umbali usiozidi nchi tano, kiasi cha kila mmoja kuwa anazisikia pumzi za mwenzake.
“This is not the right time,” (Huu siyo muda muafaka) alisema huku akiipitisha mikono yake na kunishika shingoni, kwa mara nyingine nikamshika kiunoni, akashtuka tena, safari hii kwa nguvu zaidi na kufumba macho yake mazuri, tukagusanisha ndimi zetu na kuanza kuwaiga njiwa wanavyoyalisha makinda yao.
Jambo la ajabu lilitokea kwenye hisia zangu, nikawa nahisi kama nipo kwenye ulimwengu mwingine wa tofauti kabisa, tuliendelea kugandana kama ruba kwa sekunde chache, kelele za kitasa cha chumba alichokuwa amelala Raya ndizo zilizotushtua.
Harakaharaka nikamuachia Firyaal na kumuonesha kwa ishara kwamba aende chumbani alikokuwa amelala dada yake, kweli alifanya hivyo, akakimbia kwa kunyata wakati mimi nikienda kumfungulia Raya.
“Vipi?” nilimuuliza baada ya kumfungulia mlango ambao ni mimi ndiye niliyemfungia kwa nje ili nipate nafasi nzuri ya kuwa na Firyaal.
“Wewe ndiyo ulinifungia mlango kwa nje?”
“Mh! Saa ngapi tena mpenzi wangu? Itakuwa labda mlango ulijiloki,” nilimwambia.
“Kwani ulikuwa hujalala mpaka saa hizi?”
“Nilikuwa namsubiri Firyaal arudi ndiyo nifunge geti, amesharudi na nafikiri muda huu ameshalala na dada yake na mimi nilikuwa najiandaa kulala,” nilijenga mazingira ya kujitetea. Nikampachika swali jingine:
“Mbona umeamka wakati ndiyo kwanza ulikuwa unaanza kulala?”
“Nimeota ndoto mbaya sana mpaka nimeshtuka,” alisema Raya huku akijinyoosha.
“Ndoto gani tena?”
“Inatisha sana, please Jamal mi siwezi kulala peke yangu, nakuomba tukalale wote,” alisema Raya huku akinikumbatia, nikashusha pumzi ndefu kwani niliona ananiharibia sana ‘taiming’ zangu. Hata hivyo sikuwa na namna zaidi ya kukubaliana naye, nikamshika mkono na kuelekea naye kwenye kile chumba ambacho Shamila alinipa mimi nilale.
Hata hivyo, moyoni nilishajiapiza kwamba sitafanya chochote na Raya hasa ukizingatia kwamba tayari nilishampa udhuru mapema kwamba hali yangu haikuwa nzuri. Baada ya kuingia chumbani, kwa sababu muda ulikuwa tayari umeenda sana, hatukuwa na cha ziada zaidi ya kupanda kitandani na kulala.
Japokuwa Raya alikuwa pembeni yangu, akili zangu zote zilikuwa kwa Firyaal, ni kama nilikuwa nimepandwa na pepo ndani ya kichwa changu. Nilikumbuka kila kitu kilichofanyika muda mfupi uliopita, nikawa nazilaumu ndoto za Raya kwani kama asingeota na kushtuka kama mwenyewe alivyosema, huenda tayari ningeshakuwa naelea kwenye ulimwengu mwingine tofauti kabisa.
Wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa ni je, Firyaal akija kunigongea usiku huo itakuwaje? Sikupata majibu. Kwa kuwa Raya alikuwa amechoka sana, nilipomkumbatia tu, hakuchukua muda, akaanza kukoroma tena, akiwa amelala fofofo. Niliendelea kutafakari mambo mengi na hatimaye usingizi ukanipitia.
Mlio wa simu ya mezani ndiyo ulionishtua kutoka kwenye usingizi mzito, nikamsogeza Raya pembeni na kuamka, nikatoka mpaka sebuleni na kwenda kuipokea simu hiyo.
“Haloo!”
“Haloo Jamal, umeamkaje mpenzi wangu?”
“Ooh! Shamila, ni wewe? Nimeamka salama, vipi wewe huko?”
“Huku kuna matatizo mpenzi wangu, nimekupigia kukwambia kwamba inawezekana nikawa sipatikani hewani, ishu imeshtukiwa huku na imebainika kwamba nimehusika kuwatorosha wagonjwa wawili, wewe na Shenaiza, hIvi ninavyoongea na wewe tunaingia kwenye mkutano wa dharura na viongozi wetu pamoja na polisi.”
“Mungu wangu, kwa hiyo itakuwaje?”
“Nimekupigia simu kukutaarifu kwamba hapo nyumbani kwangu hapafai tena, kuna uwezekano mkubwa polisi wakaja kufanya upekuzi kwa hiyo nakuomba muondoke haraka iwezekanavyo. Chukua kalamu na karatasi, andika namba hii nitakayokutajia,” alisema Shamila na kunifanya mapigo ya moyo wangu yawe yananienda mbio kuliko kawaida.
Nikachukua kalamu na karatasi.
‘Tayari nimeshachukua,” nilimwambia Shamila baada ya kuuinua tena mkonga wa simu, akanitajia namba hiyo ya simu na kuniambia kwamba ni ya mama yake mdogo anayeishi Kimara Temboni.
“Nimeshampigia na kumwambia kila kitu, yupo tayari kuwasaidia, mpigie sasa hivi,” alisema Shamila kisha akakata simu. Nilipoweka mkonga wa simu chini, nilitazama saa ya ukutani iliyokuwa inaonesha kwamba ilikuwa ni tayari saa kumi na mbili asubuhi, harakaharaka nikaelekea kwenye chumba alichokuwa amelala Firyaal na Shenaiza ambaye bado hakuwa amerejewa na fahamu zake.
“Firyaal, Firyaal,” nilisema huku nikigonga mlango wa chumba hicho, nilipoona kimya nikanyonga kitasa, kumbe hata hakuwa amefunga mlango, nadhani alijua kwa vyovyote usiku ule nitamfuata tena.
Nikaingia na kutupa macho kitandani, Firyaal alikuwa amelala kihasarahasara, akiwa amejifunga khanga moja tu huku dada yake, Shenaiza akiwa amelala kwenye kitanda kingine maana ndani ya chumba hicho kulikuwa na vitanda viwili.
Nilishusha pumzi ndefu kwani nikiri kwamba Firyaal alikuwa akiyafanya mapigo ya moyo wangu yaniende mbio sana, hasa kutokana na hali niliyomkuta nayo, mwenyewe akiwa hana habari ameuchapa usingizi.
Taratibu nilimsogelea, nikainama pale kitandani na kumbusu kwenye paji la uso wake, akafumbua macho na kunitazama, akaachia tabasamu hafifu na kunishika mkono wangu, joto la kikekike likazidi kunifanya nisisimke mno.
“Mbona umechelewa kuja Jamal wangu, hata mlango sikufunga kwa ajili yako,” alisema huku akinivutia pale kitandani ili na mimi nilale.
“Kuna tatizo Firyaal,” nilimwambia, kauli yangu ikamfanya ayakodoe macho yake mazuri ambayo yalikuwa yamelegea sana kwa sababu ya usingizi.
“Tatizo gani tena mpenzi?” aliniuliza kwa sauti iliyojaa shauku.
“Shamila amepiga simu anasema huko kazini kwao kimenuka, wamemshtukia kwamba yeye ndiye aliyetutorosha na hivi tunavyoongea wameingia kwenye kikao cha dharura, anasema inabidi tuondoke hapa haraka iwezekanavyo,” nilimwambia.
“Mungu wangu,” alisema huku akikurupuka pale kitandani, akasimama huku akinitazama kwa wasiwasi, mkono mmoja akautumia kuirudisha ile khanga yake ambayo alipoinuka ilifunuka upande na kusababisha niyaone tena maungo yake ambayo ama kwa hakika yalikuwa yakimuamsha shetani wangu wa mahaba.
“Kwa hiyo itakuwaje?”
“Inabidi tujiandae tuondoke, oga fastafasta kisha muandae mgonjwa, ngoja na mimi nikamuamshe Raya,” nilisema, akatingisha kichwa huku akiendelea kunitazama kwa macho yake mazuri, nikageuka na kutaka kutoka, akanishika mkono huku akiliita jina langu.
“Nambie,” nilijibu kwa upole, akanisogelea hadi mwilini na kunikumbatia kwa nguvu.
“Nakupenda Jamal,” alisema kisha akanibusu kwenye shavu langu la upande wa kushoto, mwili wote ukasisimka tena, nikakosa hata cha kujibu zaidi ya mimi kumkumbatia pia na kumbusu, uvuguvugu wa joto la mwili wake ukanifanya nitamani niendelee kumkumbatia lakini nilipokumbuka mtihani mzito uliokuwa mbele yangu, nilimuachia, nikatoka haraka na kwenda kumuamsha Raya, harakaharaka tukaanza kujiandaa.
Je, nini kitafuatia?
 
KUTUBU KWANGU (MY REPENTANCE)- 1 AZIZ HASHIM
Naitwa Flaviana Joel, mwanamke mwenye umri wa miaka ishirini na nane. Nilibahatika kuolewa miaka kumi iliyopita, nikiwa bado msichana mbichi katika umri wa miaka kumi na nane tu.
Niliolewa na mume wangu kipenzi, Ibrahim au Ibra kama mwenyewe nilivyozoea kumuita ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye benki moja maarufu ambayo sitaitaja jina kwa sababu maalum, iliyopo hapa jijini Dar es Salaam.
Kabla Ibra hajanioa, tulidumu kwenye uchumba kwa kipindi cha takribani mwaka mmoja, kipindi hicho nikiwa nasoma chuo kimoja cha uhasibu kilichopo Posta, katikati ya Jiji la Dar es Salaam, nikiwa ndiyo kwanza nimeanza mwaka wa kwanza.
Baada ya ndoa, mimi na Ibra tulihamia Mbezi Beach kwenye nyumba yetu ambako tuliishi pamoja mpaka tulipokuja kutengana kwa sababu ambazo ndizo hasa zilizonifanya nitafute nafasi hii ya kutubu hadharani na kukiri kwa kinywa changu yote niliyowahi kuyafanya.
Nimesukumwa kuja kusimulia mkasa wangu huu kwa sababu nataka watu wajifunze kupitia maisha yangu na Ibra. Najisikia aibu sana, najikaza tu kwa sababu nataka wanawake wenzangu waelewe kilichonitokea na kamwe wasifuate njia kama ambazo mimi nilipita. Pia iwe funzo kwa wanaume, hasa wale ambao wapo ndani ya ndoa.
Nasikitika kwamba nimekuwa kikwazo kikubwa katika maisha ya Ibra, mwanaume niliyetokea kumpenda kwa moyo wangu wote lakini kwa sababu ya mapungufu ya kibinadamu ambayo nitayaelezea, nikageuka na kuwa mwiba mkali kwenye maisha yake.
Nilisema tangu awali na nitaendelea kusema kwamba sijawahi kutokea kumpenda mwanaume kama nilivyompenda Ibra ila hata sielewi ni kitu gani kilichosababisha haya yote yatokee.
Najisikia uchungu sana ndani ya moyo wangu hasa nikiwatazama wanangu Joel, James na Mahiza ambao bado walikuwa wakihitaji malezi ya baba na mama lakini kwa kukosa akili kwa mama yao (mimi) leo wanateseka mno.
Siwezi kumlaumu Ibra kwa sababu alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kufanya yale ambayo mwanaume anapaswa kuyafanya katika ndoa yake ingawa pia alikuwa na udhaifu mkubwa ambao ndiyo uliosababisha leo hii nipate nguvu ya kuja kutubu hadharani na kuwa sauti ya wengine ambao waume zao wana matatizo kama aliyokuwa nayo mume wangu Ibra lakini hawana pa kusemea.
Naamini kutubu kwangu na kueleza ukweli wa kila kitu kwenye maisha yangu, kutakuwa chachu ya mabadiliko katika nyumba nyingi na kutaokoa ndoa nyingi.
Ukimya unaua, naamini kuna wanawake wengi sana ambao wanakufa taratibu kwa sababu hawataki kuyasema matatizo ya ndoa zao hadharani, matokeo yake wanazalisha matatizo mengine kwa waume zao ambayo mwisho wake ni kama huu ulionitokea.
Kama kujiua isingekuwa dhambi, hakika ningeyakatisha maisha yangu lakini naogopa nitakachokutana nacho siku ya kiyama. Naamini kwa kuyasimulia haya, angalau kidogo nitapunguza mzigo unaonielemea ndani ya nafsi yangu.
Nawaomba radhi wote mlioumizwa na matendo yangu na mtakaoumizwa na ushuhuda huu, hasa kipenzi changu Ibra, watu wote wanaotufahamu na kubwa zaidi kwa mama yangu ambaye matendo yangu yamemfanya adharaulike na kila mtu kwani inaonekana alishindwa kunilea katika maadili mema.
Pia naomba Mungu wangu anisamehe na nitaendelea kumlilia kila siku kama nilivyofundishwa na mtumishi wa Mungu, Mchungaji Mwakatobe ambaye ndiye aliyeniongoza katika sala ya toba.
***
April 8, 2003
Dar es Salaam.
Ilikuwa ni asubuhi yenye mvua kubwa ambayo ilisababisha hali ya taharuki kwa wakazi wengi wa Jiji la Dar ambao tulikuwa tukitegemea usafiri wa daladala. Nakumbuka vizuri ilikuwa ni tarehe 8 ya mwezi wa nne, mwaka 2003. Naikumbuka vizuri tarehe hii kwa sababu ambayo baadaye nitaielezea.
Nilikuwa nimebeba begi langu begani na kujikunyata pembeni ya kituo cha daladala cha Morocco, kwenye makutano ya Barabara za Ali Hassan Mwinyi na Old Bagamoyo Road, nikisubiri usafiri wa kuelekea chuoni, Posta.
Daladala siku hiyo zilikuwa za taabu sana kwa sababu ya hali ya hewa iliyosababisha foleni kubwa karibu kwenye barabara zote za Jiji la Dar es Salaam. Kama ujuavyo Jiji la Dar mvua ikinyesha kidogo tu basi barabarani hakupitiki kutokana na foleni.
Ilikuja daladala ya kwanza iliyokuwa inaelekea Posta lakini ilikuwa imejaza mno kiasi cha watu wengine kuwa wananing’inia mpaka mlangoni. Nikashindwa kupanda. Ikaja ya pili nayo ikiwa katika hali hiyohiyo, ikanibidi niendelee kusubiri.
Mvua nayo ilikuwa inaendelea kunyesha, safari hii ikiambatana na upepo uliosababisha wote tuliokuwa tumejibanza pale kituoni kuanza kulowa. Nilitamani kurudi nyumbani kwani ukiachilia mbali kero ya mvua, muda nao ulikuwa umeenda sana.
Nikiwa najishauri cha kufanya, gari dogo aina ya Toyota Carina lilikuja na kusimama pale kituoni, jirani kabisa na pale nilipokuwa nimesimama. Kioo cha upande wa kushoto kikashushwa kisha tukamsikia dereva akituambia kuwa kama kuna wanaoenda Posta, anataka kuwabeba watu wanne tu kwa sababu daladala zinasumbua.
Mimi nilikuwa wa kwanza kulifikia gari hilo dogo lakini zuri, nikawahi kufungua mlango wa mbele na kujitoma ndani. Abiria wengine wengi wakafuata na kuanza kugombania lakini kwa sababu gari lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria wanne tu, watatu nyuma na mmoja mbele, ilibidi wengine wabaki.
Nilijiona kuwa na bahati kubwa, nikamgeukia dereva na kumsabahi huku nikimshukuru kwa msaada wake. Abiria wengine nao walifanya hivyohivyo, akaondoa gari na safari ya kuelekea Posta ikaanza. Kwa kuwa sote tulikuwa tumelowa, hakuna aliyekuwa na stori na mwenzake, kila mmoja akawa anajifuta maji.
Safari iliendelea taratibu kutokana na foleni na baada ya muda mrefu, hatimaye tulifika Posta. Kila mmoja alifungua nauli na kutaka kumpa dereva lakini mwenyewe alikataa na kutuambia kuwa ametusaidia tu kwa hiyo tusimlipe.
Tulimshukuru sana, sote tukashuka na kila mmoja akaendelea na hamsini zake. Baada ya lile gari kuondoka, nilikumbuka kuwa nilikuwa nimesahau begi langu lenye madaftari, vitabu na vifaa vyangu vingine vya kusomea. Nilijikuta nikichanganyikiwa ghafla, nikawa najilaumu kwa uzembe nilioufanya.
Ilibidi nianze kulifukuzia lile gari kwa nyuma lakini tayari nilikuwa nimechelewa, lilishajichanganya na magari mengine, hali iliyonipa wakati mgumu kulitambua kwani kulikuwa na magari mengi aina ya Carina Posta, tena yote yakiwa yanafanana.
Nilitoa simu yangu mfukoni lakini nilishindwa kuitumia kwa sababu sikuwa nikizijua namba za dereva. Nikajikuta nikiishiwa nguvu kabisa. Safari yangu yote haikuwa na maana tena kwa sababu nisingeweza kwenda chuo nikiwa sina vifaa vya kusomea.
Kwa kuwa bado mvua ilikuwa ikimwagika, nilisogea kwenye korido ndefu za Posta Mpya na kujibanza hapo pamoja na watu wengine wengi waliokuwa wamejisitiri mvua. Nikiwa bado najiuliza cha kufanya, simu yangu ilianza kuita. Nilipotazama namba ya mpigaji, ilikuwa ngeni kwangu.
Sina kawaida ya kupokea namba za simu nisizozijua lakini siku hiyo niliipokea haraka ilipoita mara moja tu.
“Halloo!”
“Haloo, nani mwenzangu.”
“Samahani, unamfahamu Flaviana Joel?”
“Ndiyo namfahamu, kwani vipi?”
“Kuna watu niliwapa lifti kwenye gari langu muda mfupi uliopita sasa kuna mmoja amesahau begi lake la vitabu, nilipopekua ndiyo nikaikuta hii namba imeandikwa nyuma ya kitabu kimoja. Naomba umpe namba yangu mwambie anitafute au nipe yake nijue namna ya kumfikishia mzigo wake,” alisema dereva wa ile Carina kwa sauti ya kiungwana mno.
Nilishusha pumzi ndefu na kuachia tabasamu, nikamwambia kwamba mimi ndiyo Flaviana, nikamsikia akicheka kidogo kisha akaniuliza nipo wapi kwa wakati huo. Nilipomuelekeza, aliniambia nimsubiri hapohapo anakuja.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom