Makapuku Forum

Amina
 
ENDELEA..........



Kama tunavyomjua kijana sheby tabia yake katika simulizi zilizopita hua hapitwi na matamanio ya kimapenzi, katika hisia za kijana sheby yeye hata ukae uchi, hisia zake hazitopanda kwa kasi kama ilivyo katika nguo ya ndani ya kike, yaani kila mtu anajua nini kinachompa hisia za kimapenzi,.. Kuna mtu mwingine akimuona tu mwanamke kavaa dera anachanganyikiwa mpaka basi, mwingine akiona hata wigi kichwani anaweweseka halali usiku kucha, mwingine hata akiona unyayo wa mwanamke yaani anafanya kutetemeka,... Hivyo kwa huyu kijana yeye hisia zake ni hizo, akiona nguo ya ndani tu hata kama ipo wapi yeye hali yake inabadirika na kujikuta anatamani mwanamke.....
Sheby alizidi kuiangalia chupi hio iliokuwa imetundikwa katika tendegu la kitanda,.. Hisia za mapenzi zilimpanda ingali yupo ugenini kwa watu... Yule dada aliona sheby kaangalia wapi, lakini hakuta kumshtua kuwa kwanini alikuwa akiiangalia sana nguo yake,..
"karibu ukae kaka"
Yule dada aliongea hivyo ili hata kumshtua kijanja janja, mana anashindwa kumwambia asiangalie nguo yake,..
"Ahsante dada angu"
Sheby alikaa katika makochi yaliochakaa sana, yaani hata vitambaa vyake vimechanika afu yeye ni fundi,.. Mana hawezi kumaliza faida anayopata kwa ajili ya kushona vitambaa vya makochi yake,
"ok ahsante dada yangu.... Aaaahh Samahani sana, nikiwa naendelea kumsubiria baba mwenye nyumba, kuna jambo nataka tuliongee mana umeshakuwa jirani yangu sasa"
Aliongea kijana sheby huku nae akiwa na busara zake, sema busara hupotea pale anapoona nguo za kike,
"sawa tuongee haraka nirudi kazini"
Aliongea dada huyo huku akiwa kweli ana haraka ya kutoka hapo..
"lakini bado hatujajuana hata kwa majina mama"
 
mmhhh.. Mimi naitwa Shadya ukipenda niite Shadi"
"waoooo jina lako limeanza kama jina langu vile"
"kwani we jina lako nani"
"mimi naitwa Sharbiny, ni mtoto pekee kwenye familia ya kita... Nooo... Kwenye familia ya kimaskini"
Sheby alitaka kukosea neno akajikuta anataka kuongea eti yeye ni tajiri... Basi shadya alipata kucheka kwa kigugumizi alichokipata sheby wakati wa kujitambulisha kwa Shadi (Shadya)...
"unanicheka si ndio"
"No, unajua nini? Ulitaka kujitambulisha hali za wenzako na wakati hali yako inaonyesha tu ulivyo"
"kwani mi nipoje"
"ulivyomalizia kujitambulisha ndivyo ulivyo, na ndivyo unavyoonekana"
Shadi alimaanisha kwamba sheby alionekana maskini kabisa, lakini weeee heeeee balaa tu, pesa zimelala hapo..
"sasa shadi, kuna kitu cha muhimu dana nahitaji kukuomba,.. Binafsi nahisi utanikubalia ombi langu"
"mmmhh kaka unanitisha, kwani ni ombi gani unalotaka kuniomba"
Maongezi yao hapa ndipo yanapoanza,

Siku hio ilipita lakini hatukujua maongezi ya akina Shasha (Sharbiny na Shadya).. Ilionekana kuna siri kubwa tumefichwa baina yao,..
Sasa sheby akiwa ndio anatoka kazini mida ya saa 11 hivi akielekea kwa akina mary, kama unakumbuka ana kazi ya kuwafundisha wadada hao ili wapate kazi katika kampuni yao,.. Mana vyeti vyao havina sifa ya kupata kazi popote pale labda viwandani,. Sheby alipiga honi nje ya geni lakini sio kuwa alitaka kuingiza gari, ila alikuwa anawaita waje wafungue mlango mdogo,.. Mana nyumba wanayoishi ni nyumba ya kupanga,... Haikupita muda mrefu akina mary na rose walitoka na kumpokea sheby, mana alikuwa ana laptop na kibegi chenye madocoment ya kumfunzia mfanyakazi,.. Na jukumu hilo baba yake halijui kabisa, ni sheby mwenyewe ndio kajitolea kufanya hivyo,...
"karibu boss"
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…