Kazi kwenu wapenda kope za bandia
Daktari Muhimbili aeleza jinsi KOPE ZA BANDIA zinavyofanya WAREMBO kuwa vipofu
Daktari Bingwa wa Macho na Mkuu wa Idara ya Macho katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Baruani Mtemi Sufiani amesema kuwa Kope za bandia zinamadhara makubwa sana kiafya katika macho. Bofya hapa kutazama video >>>
Dkt. Buriani amesema kope za Bandia zimetengenezwa na Kemikali ambayo husababisha muwasho katika macho kisha mikwaruzo ambayo baadaye hutengeneza vidonda ambavyo baada ya kutibiwa hubakisha makovu.
Ukubwa wa makovu hayo husababisha uoni hafifu au kushidwa kuona kabisa. Bofya hapa kutazama video >>>
Amesema kumekuwa na wadada wengi wanaoweka kope za bandika wakiona kuwa ni urembo bila kujua madhara makubwa yanayoweza kusababishwa na kope hizo, hivyo amewataka kuacha kutumia ili kujiepusha na madhara hayo na badala yake wabakie na kope zao walizoumbwa nazo.
Dkt. Buriani amesema kumekuwa na wagojwa wengi ambao wanafika katika hospitali ya Muhimbili wakiwa na tatizo hilo na amekuwa akiwashauri kuachana na kope za bandia. Bofya hapa kutazama video >>>