Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 44,001
- 150,526
Muziki: Furahiday, Usivunje Madaraja
Ninakusalimia Kapuku mheshimika, na leo Ijumaa sijui huwa ni kwa nini huwa najikuta napenda ukiacha bakulutu basi muziki wa reggae na matawi yake huwa unanikosha sana na kunifanya niwe na furahiday nzuri sana. Najua nawe una 'ulevi' wako wa muziki siku na siku. Siku ambayo ninapenda kusikiza taarabu nitakuambia maana sio leo.
Asante sana shululu kwa magazeti, shukrani sana mpendwa wangu wa ukweli husna muba kwa kuwa super sub kipengele cha historia, niseme nini kwako BlessedHope kwa sala na maombi ya kutwa mara tatu, back up ya Lyon Lee imekaa poa sana. Hamjui tu ninyi wadau mnaifanya kapuku forum kuwa sehemu bora kabisa ya kuwepo. Usiseme nimesahau wadau wa ukweli makaveli10 , Tumosa , dumejeuri , SHIMBA YA BUYENZE , dingimtoto , mzeewakungoa , Mndali ndanyelakakomu , Shunie , moneytalk , shedede , Jimena , Mussolin5 , Clkey , Nyagei , genius aka Mond, Transcend , Sakayo , Madame S na wewe mdau unayenisoma sasa hivi.
Muziki sasa, reggae ina siasa nyingi sana na kibao hiki cha Shaggy akishirikiana na mwenzake Chronixx kimenivutia na kunikumbusha nikuambie kuwa katika maisha ni bora kujenga daraja na si kulibomoa lililopo na kwa wanasiasa wetu wa leo wanajitahidi sana yale wanayoamini (wishes) wanadhani ndo tunayaamini na matokeo yake badala ya kutuunganisha na kufanya limited objective ili kutuaccomodate wetu na differences zetu zinazotuunganisha wanajifanya wao wako sawa na sisi hatuko sawa.
Utaipenda reggae na hasa ukiangalia kuna jamaa kashika gitaa zito la bass nyuzi 6, ni lazima urukeruke na hukatazwi kurusha mikono hewani. Wikend Njema Kapuku mwenzangu
Asante anko
MAUTI NA UZIMA ZIPO KATIKA UWEZO WA ULIMI.




