BlessedHope
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 7,988
- 32,649
MAUTI NA UZIMA ZIPO KATIKA UWEZO WA ULIMI.Mithali 18:21.
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
Hapa

hugharimu wengi bila kujua au muovu kutumia sana nafasi hii kuwaangamizia wanadamu...Mfano mzazi anamtukana mwanawe kwa maneno makali sana kutamkika na kumlaani...au mume na mke wamegombana maneno makali wakatamkiana yaliyo ya maangamivu....basi hapo watakuwa wamebeba yaliyo ya mauti....bali tukitamka ya baraka....mfano mzazi anamwambia mwanawe mtoto wangu Mungu akubariki utakuwa kichwa daima...uwe baraka kwa ulimwengu...Mungu na akupe kibali popote uendapo...
Kwa kutamka mabaya au mazuri yanajiandika kwenye ulimwengu wa Roho na kufuatilia kwenye maisha ya mtu...
Kwa hayo utakula matunda ya ulichotamka ikiwa ni mbaya mauti yapo ujue...
Ikiwa ni mazuri basi kuna uzima...
TUSILE MATUNDA MABAYA YATOKANAYO NA NDIMI ZETU,MAANA ULIMI UMEBEBA UZIMA NA MAUTI...
BALI TUCHAGUE UZIMA NA TUKATAYE LAANA..
Kwa ndugu zetu...jirani yako...mtoto wako.....mume...mke...wako..mama.....baba...marafiki,wapenzi na jamii kwa ujumla..


MBARIKIWE WANA WA BABA ..LOVE YOU
