Muziki: Futuhi, Uaminifu na Kuaminika
U khali gani Kapuku mheshimika, upande wangu nimekuwa na wakati mzuri sana, nashukuru. Leo ni Alhamisi, hilo halina siri, na ni siku nzuri ya kufurahia vichekesho, kuanzia saa moja utakutana na kina Mtanga, Masanja na saa tatu tatu hivi unakutana na kundi zuri kabisa FUTUHI na ni hapa sasa itabidi ujipange kwa vichekesho vingine vya mabingwa wa namba nne EPL, Arsenal. Ukibahatika kuviangalia vichekesho hivi vyote wewe ni muaminifu sana.
Uaminifu, ngoja nikueleze, una misingi mikuu minne, miwili ya kwanza ni wewe na tabia zako (character) na misingi miwili iliyobaki ni weledi wako na kwa ujumala yake yote unamaanisha uaminifu wako na kuaminika. Kumbuka, kuaminika na kuwa mwaminifu ni jambo zuri haijalishi unaamini katika dini au huamini. Makundi ya tabia yanajumuisha Ukweli (Integrity-honesty). Ukikosa kuwa mkweli kuaminika sahau. Kingine ni Makusudi, una makusudi gani katika maisha, mengine nitayataja tu maana muziki haupaswi kuwa chini sana, Uwezo (capabilities) na mwisho Kufikia Matokeo, je unayofanya yanakuletea matokeo chanya au hasi. Jibu unalo mwenyewe.
Muziki sasa, leo hatupaswi kucheza, ni kukaa unaburudika kwa muziki wa taratibu na hiki ndo unaenda kukipata