Makapuku Forum

R.I.p nimemeet na "tiger wood"kitaani
 
hiyo kweli
 
6/Night Monkey
Hawa ni nyani wachawi maana wanaonekana zaidi muda wa usiku kama popo
Wanapatikana zaidi huko nchini Panama na baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini
Waswahili husema nyani haoni kundule hivyo usiendekeze masimango kwa hawa nyani kuhusu tabia yao ya kulala ovyo wakati weewe hapo ulipo hupo kotandani na smartphone yako ....nyanyuka kwanza

Kea siku hulala masaa 17
................,.................
Zitaendelea baadaye
 
Kila siku huwa najiuliza: How did we survive as a specie hasa hapo mwanzoni mwanzoni kabla ya kugundua moto na silaha za kujilinda?
 
5/Python
Kwa kiswahili sanofu cha TUKI ni chatu
Kuna aina za chatu zaidi ya 30
Ni jamii ya nyoka wakubwa duniani nafikiri hata Anaconda ni chatu tu ila imi sio mtaalamu wa qanyama
Chatu ni reptilia wakubwa kwa urefu
Uzito wao huweza kuwa zaidi ya Kilogramu 150
Chatu wanapatikana barani Afrika,Asia na Australia
Kwa hapa bongo wafugaji ndio wanajua zaidi tabu ya hawa chatu maana huvizia ifugo na kuimeza bila kubakisha hata kwato
Samtaimu humeza watu !!....Kama. Unakaa porini huko Singida chunga sana mwanao

Kwa siku hupiga usingizi masaa 18
.........
 
4/North American Opossum
Opossum wanapatikana barani Amerika ya Kusini na Kaskazini
Kuna aina zaidi ya 100 za hawa wanyama
Sasa hapa nawaongekea wale wa Amerika Kaskazini kama jina lao lilivyo
Wanapatikana katika nchi za Mexico na kule kwa Mzee Donald Trump
Hawa nao wanafanana na panyaau sumgura sasa kama umezoea kuwinda sungura pori ipo siku unaweza kukutana nao na bila kujua ukaewageuza kitoweo

Kwa siku hulala masaa 18
......
 
3/Giant Armandillo
Wanafanana na kakakuona
Wanapatikana huko Amerika ya Kusini katika nchi ya Argentina hivyo kama unabisha kamuulize Messi
Hawa ndio Armandillo pejee wakubwa walio haimaana wengine wameshatoweka kwenye uso wa dunia
Licha ya kuitwa jina lenye heshima la giant ila hawa jamaa wanalala sana hivyo bora tu wajiite weak armandillo wanatia aibu tofauti na jina lao

Kwa siku hulala masaa 18.2
............
 
2/Brown Bat
Popo ni ndege au ni mnyama ?
Mtabishana siku nzima naana jamaa ana manyonyo kama ng'ombe halafu anaruka kama kunguru
Hapa namzungumzia popo wa kahawia sio uliowazoea wewe
Sasa ukisikia team popo ndio uekewe kwamba ni watu wanaokuwa macho mida ya usiku kuliko mchana
Humu nfani binamu Obe labda ndoye popo wetu

Kwa siku hulala masaa 20
....................................................................
Achana na popo kuna mnyama mwingine bwege aitwaye Sloth yaani huyu ukimwangalia tu sura utaelewa

Kwa siku nae hulala masaa 20
.....................
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…