Makapuku Forum

Makapuku Forum

0883e9da020f0fa9b2c5c5f506e870a6.jpg
 
Jihadharini na manabii wa uongo watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa undani ni mbwa mwitu wakali

Mtawatambua kwa matunda yao. Je watu huchuma zabibu katika miiba au tini katika mibaruti?

Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda na mti mwovu huzaa matunda mabaya

MATHAYO 7:15-17

Muwe na asubuhi iliyo njema kwenu na mbarikiwe sana
 
Baada ya chakula cha roho kutoka kwa mpenzi wangu shunie kipenda roho ...tuone Uf ...ila tuanze na mr x ...

Asha alijitahidi kuificha hali ile ya mstuko wake machoni lakini Cj4 alimgundua vizuri sana na kwake yeye hakuonesha mstuko wowote machoni zaidi ya kumsogelea na kumpa pole kabla hajaanza kumuuliza maswali ambayo Asha alibaki kama bubu asijue aanzie wapi kuyajibu.
"Hebu nambie unajua nini zaidi kuhusu mr X, wala usinifiche ila nataka unijuze mr X alikupa neno gani la mwisho pindi ulipoasi?"
Aliuliza Cj4 kwa sauti ya chini sana lakini iliyosikika vizuri masikioni mwa Asha na kubaki anababaika aanzie wapi na hapo ndipo Cj4 alipomuachia kikaratasi cha namba za mawasiliano kisha akatoka taratibu na kumuacha Asha ametumbua macho kwa taharuki.
("Khaa! huyu si ndio yule Afande wa Chalinze? kajuaje kama niko hapa? kajuaje mambo yangu na Mr X?")
alijiuliza maswali haya Asha ambayo alijua fika kuwa hakuna mtu wa kumfata moja kwa moja akampa majibu yale bila yeye mwenyewe kuyatafutia ufumbuzi kupitia yule yule mtu.

Baada ya masaa mawili Kamishna Shebby nae alifika pale hospitali na kufanya utaratibu wa kuwatoa na kuwapeleka kwenye makazi mapya aliyowatafutia.
"Mama kwa sasa mtakuwa hapa kipindi tunafanya taratibu za kumaliza hili suala la ndoa, nataka Mungu akitujaalia tulifanye hata wiki ijayo"
"Wiki ijayo?"
"Eeh mama"
"Atakuwa kashapona vizuri kweli!?"
aliuliza kwa mshangao yule mama kutokana na kuona mambo yamekaa jilani sana tofauti na alivyodhani baada ya Asha kupatwa matatizo
"Kwa hilo usijali mama, kama yeye alivyoniuguza na tukakaa wote hadi kuwa wachumba basi nami nitamuuguza tukiwa wote kama mtu na mkewe, naamini Mungu ndie anayetupangia tukutane aktika vipindi vigumu vya mataaizo kama hivi"
aliongea Shebby maneno ambayo Zena aliyaelewa na kukubali
"Lakini naomba mjitahidi baba asijue kama ana mshono mwanae mtamchanganya"
aliwakumbushia nao walikubali jambo lile na Hussein bubu hakuambua kujua ukweli juu ya kilichompata Asha zaidi ya kujua makazi mapya na kuingojea hiyo siku ya kumuoza mwanae kwa udi na uvumba.

Kwa upande wa Asha ilikuwa ngumu sana kwa kumtazama tu ukagundua kuwa ana jeraha mwilini mwake kwa jins vile alivyokuwa anajichangamsha na kujiweka lakini kuna kitu kimoja kilimuumiza akili zake na kuufanya usiku ule wa kwanza kwenye yale makazi mapya kuwa mgumu sana upande wake na si kwa sababu ya kufikiria juu ya ndoa bali ni kwa sababu ya ule ujio wa askali ambae anakumbuka alionana nae siku ile aliposababisha ajali iliyopelekea kifo cha mzee Cypilian.
Alishangaa kila alipomuangalia Shebby hakuonesha dariri zozote za kumstukia zaidi alipowahi kumuuliza juu ya mshono kule hospitali nae alijibu aliwahi kweli kufanyiwa upasuaji mdogo wa kidole tumbo (appendex) wiki za karibuni na alifanya siri ili asimtie hofu mamaake na uongo huo Shebby aliuamini kabisa.
Usiku huo Asha hakuwa na jinsi ilibidi amtafute hewani yule askali na kweli alipopiga tu zile namba Cj4 alipokea na baada ya kujua anayeongea nae alimuuliza swali lile lile na Asha hakuwa na jinsi ilibidi aongee yote anayoyajua na kumpa lile neno la mwisho aliloambiwa na mr X ambalo lilikuwa sawa kabisa kama alilowahi kuambiwa amwambie Shebby.

* * * *

Mipango ya ndoa ya Kamishna Shebby na Dokta Asha ilizidi kushika kasi kwenye vichwa vya wanafamilia ambapo kwa upande wa mzee Mwinchande na mkewe ilikuwa ni zaidi ya furaha na walifanya utaratibu na kuongea na sheikh mkuu wa jiji la Dar ndie aje kuwa mfungishaji Ndoa hiyo ambayo Mwinchande alipania kuifanya iwe ya kipekee sana japo mipango yake ilikuwa ni ya muda mfupi.

Na hatimae baada ya maandalizi yote kukaa katika mstari (kuwa sawa) Kamishna Shebby alikutana tena kwa siri na Cj4 siku moja kabla ya ndoa kwa maongezi maalum.
"Sikia Shebby, kesho ni siku kubwa sana na muhimu katika kujua muelekeo wa Mr X"
aliongea Cj4
"Kivipi kiongozi"
"Kumbuka neno la mwisho la mr X uliloambiwa na yule Ninja."
"Yap nakumbuka lile fumbo"
"sasa kwa kuwa kesho kutakuwa na wageni wengi kwenu wanaokutambua nina wasiwasi kutakuwa na ugeni wa Mr X pia kwa kuwa anakutambua. Na hii ndio inanifanya na mimi kuja kwenye hiyo sherehe lakini hakuna atayejua kama nimekuja zaidi yako lakini pia nawe hutoniona kama nimekuja lakini nitakuja."
alichanganya maneno Cj4 na kumfanya Shebby akubali lakini asijue maana halisi ya maneno yale zaidi alipata picha kuwa kuna uwezekano kweli mr X akahudhulia hiyo sherehe au akatuma mtu wake kwaajili ya kuwamaliza katika hiyo sherehe ya harusi iliyotarajiwa kufanyika kesho yake.

"Kitu chengine Shebby umepangaje kuhusu Hussein akitoka hapo hotelini?"
aliuliza Cj4
"Nimepanga nikamnunulie nyumba sehemu salama."
alijibu Kamishna Shebby kauli iliyopingwa na Cj4
"Hapana Shebby, hakuna nyumba iliyo salama kwa Hussein kabla ya kifo cha Mr X"
"sasa Unanishauri vipi kiongozi"
"Inabidi ukae na wazazi wako uwaombe waishi na Hussein pale kwenu kidogo hiyo itakuwa salama kwake"
"Kwa hiyo unananambia Hussein akaishi nyumbani ndo itakuwa salama?"
"Ndio hivyo nionavyo"
"Sio kama nitasogeza maadui wanaomuinda nyumbani?"
"Hapana Shebby, hiyo ndio njia ya msingi"
"sawa kiongozi"
Kamishna Shebby alikubali tena swala la pili lililotolewa na Cj4 na kuagana huku wakitakiana kila la kheri hiyo kesho yake ambapo Cj4 atakuja kwa ngazi maalum ya kuwachunguza wageni wataofika ili apate kumtambua Mr X.


Wageni na viongozi mbalimbali waliendelea kumiminika katika ukumbi maalum uliokodiwa kwa niaba ya sherehe za kuwapongeza bwana Shaaban Mwinchande na bibi Asha Hussein kwa muungano wao wa kimwili na kuwa kitu kimoja kama ilivyo katika maandiko yaani mke na mume.

Ilikuwa ni majira ya saa kumi jioni mara baada ya ndoa iliyofungwa majira ya saa nne asubuhi katika Msikiti mkubwa kabisa jijini chini ya Sheikh mkuu.
Ilikuwa ni furaha sana kwa kila mtu hususani Hussein yeye muda wote alikuwa na leso akifuta machozi kwa kutoamini kama leo amefanikiwa kumuoza mwanae kwa mtu ambae alitokea kuwa chachu ya yeye kutolewa jera.
Ilikuwa ni furaha kwenye sherehe ambayo kweli ilikuwa ya kipekee na wageni walikuwa wengi sana kuanzia viongozi wastaafu waliokuwa na urafiki mkubwa na mzee Mwinchande miaka hiyo pamoja na viongozi wa usalama hususani jeshi la polisi na magereza.
Bila kusahau wageni wengine tu waalikwa ambao wao hawakuwa na wadhifa wowote nchini.

Akiwa amekaa upande maalum kulipotegwa kwa wazazi wa kiumeni na wale wa kikeni Hussein muda mwingi alikuwa na furaha lakini kila anapogonganisha macho na mamaake Kamishna Shaaban alijikuta anapata mshtuko muda mwengine ambao hakujua unatokea wapi lakini alikuwa anaupotezea.
Kuna wakati hasa ule wa kula keki na kupiga picha ndio kabisa Hussein alizidi kuushangaa moyo wake kuongeza mapigo kila anapoangaliana na yule mama hasa wakati walipokaa pamoja na mzee Mwinchande, Zena na yule mama Shaaban alijikuta kama anatamani kumuuliza kitu lakini hakujua ni kitu gani na kuishia kujichekesha tu.

kulikuwa na wapiga picha waalikwa tofauti tofauti kwenye ule ukumbi na mmoja wapo kati ya wale wapiga picha alikuwapo Cj4 ambae ilikuwa ni vigumu sana kutambulika kwa mtu yeyote aliyekuwa anamjua hapo kabla kwa ule muonekano alioingia nao pale.
Hata Shebby alipokaa na mkewe jukwaa kuu kusikiliza nasaha za hapa na pale kutoka kwa wazazi na watu wengine, macho yake muda mwingi yalikuwa yanaangaza huku na huko ndani ya ukumbi kwa lengo la kumuona Cj4 lakini hakufanikiwa kumgundua japo alikuwa jilani nae muda wote kwani wapiga picha walikaa mbelembele ya eneo la tukio ili kuweza kuchukua na kupiga picha vizuri.

Muonekano wa Cj4 siku hiyo alikuwa na Mustachi mkubwa tu sambamba na miwani ambayo kwa nje ni kama ya macho lakini haikuwa hivyo na hata mustach aliokuwanao ulikuwa wa bandia.
Alichokuwa anafanya kwa kutumia ile kamera Cj4 ni kurekodi video huku akiwachukua karibu wageni waalikwa hususani wale wastaafu wote nia na madhumuni pindi atapoondoka akirudie kuikagua kwa umakini ile video apate kumjua mr X kwani aliamini kivyovyote mr X lazima angekuja mwenyewe sehemu ile ya ukumbi na iwapo atakuja basi amani itatawala lakini iwapo mr X asipokuja aliamini kuna tukio lolote lingeweza kutokea hivyo muda wote alikuwa makini kwa hayo yote mawili Cj4.

Kwa jinsi mambo yalivyoenda vizuri pale ukumbini hakukuwa na aliyegundua wala kuhisi kama yule bibi harusi ana jeraha la mshono tumboni na hiyo ilibaki siri ya watu wachache tu japo wengi walisikia tukio la kuungua kwa nyumba ya Dokta Asha.

* * * * *

Sherehe ziliisha majira ya usiku sana na kutokana na sababu maalum fungate la Shebby na Asha lilipangwa kufanyika palepale kwenye Jumba kubwa la kifahari la mzee Mwinchande.
Nyumba ile nyengine aliyokodi Shebby ililipiwa na kukabidhiwa Zena kuwa nyumba yake huku kwa upande wa Hussein bubu alijumuika pamoja na wazazi wa Kamishna Shebby kwaajili ya makazi ya muda pale kwenye jumba la Mwinchande kipindi ambacho Kamishna Shebby atapokuwa anamtafutia makazi rasmi ya kudumu.

Alfajiri na mapema ndani ya jengo la mzee Mwinchande kwa mara ya kwanza Hussein bubu alijiona kweli yuko huru mara baada ya kulala katika chumba kikubwa chenye mandhali ambayo hajawahi hata siku moja kulala tokea kuzaliwa kwake mpaka pale alipofikia.
Usiku huo alimshukuru sana Mungu kwa yote yaliyoendelea na aliendelea kumuomba kama ilivyokuwa kawaida yake kuwa amsaidie aweze kumtendea muujiza alipe kisasi kwa kumuua Mr X kwa mikono yake.
Japo kwa akili ya kawaida ilikuwa ni kazi ngumu na ni kitu kama cha kufikirika tu kutokana na wengi waliokuwa mashupavu na uwezo wa vita kushindwa walau kumjua mr X sembuse Hussein ambae kashaanza kujiishia umri umemtupa mkono harafu aweze kumuua?
Lakini kwa Mungu Hussein aliamini hakuna linaloshindikana aliamini kabisa imani thabiti na kumuomba kila siku japo alijua kuua ni dhambi lakini kwa dhambi ya kumuua Mr X aliiomba na kuikubali kwa moyo mmoja kuliko kumuacha hai.

"Aslaam alaykum"
alisalimia mzee Hussein asubuhi ile pindi alipotoka na kumkuta Mzee Mwinchande upande wa sebuleni ambapo alikaa kwenye mswala akisoma qur'aan baada ya kusali sala ya alfajiri.
"Waaleikum salaam warahma tullah wabarakatul"
alijibu kiurefu kabisa Mzee Mwinchande kwa rafudhi maridhawa ya kiarabu kuonesha jinsi gani dini imelala kwenye ubongo wa Mzee Mwinchande.
Moyoni Hussein alijisikia faraja sana kukutana na familia ya wacha Mungu kama ile na akiwa maeketi kwenye moja ya sofa akimtazama babaake Kamishna Shebby akisoma qur aan kwa utulivu kabisa na kumliwaza Hussein japo alikuwa hajui tafsiri yake na alipata imani ya kumuelewa vizuri Kamishna Shebby kwanini kawa mtu tofauti mwenye roho nzuri, kumbe kwa sababu amelelewa na watu wenye imani na kuishika dini.
Akiwa ametabasamu pale sebuleni mara alimuona kwa mara nyengine mamaake Shebby ambae rich ya kwamba nae umli kidogo ulisogea lakini pindi anapokutanisha nae macho moyo wake unastuka sana na hadi muda mwingi alipuuzia na hakujua kwanini lakini safari hii asubuhi mara tu aliposikia sauti ikimsalimia na kuinua kichwa chake kuitikia huku akimtazama akili yake ilimletea picha iliyomfanya apigwe na bumbuwazi hadi yule mama alishangaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom