Wale wa mr x twende sawaa.....
.........Ashaaaa!!! Ashaaaa Ashaaa Mwananguuuu Jamaaaaniii msaadaaa...
Motoooo Moootoooo"
alipagawa Zena huku akimbuluza Asha kwa nje kumtoa pale alipodondokea na kwa bahati nzuri alidondokea kwenye Sofa huku ule mlango uliofatuka kwa mlipuko na kurushwa sambamba nae ukiwa umedondokea sakafuni na hapo ndipo moto ulianza kukamata zuria pale chini taratibu.
"Jamani msaaadaaaaaa aaaaaah"
alipiga yowe Zena lakini kumbe mlinzi pale getini alishatimua mbio muda mrefu mara baada ya kishindo kizito kilichosikika upande ule wa juu ya nyumba chumbani kwa Asha sambamba na fungu la moto lililofumuka angani mithili ya wingu na kushuhudia hadi vigae vilivyokuwa upande ule vikifumuka kwa mlipuko ambao uliwatisha hadi majirani na wapita njia waliokuwa karibu na eneo lile.
Akiwa anahangaika mwenyewe Zena kumvuta Asha huku akiogopa hali ya usalama mule ndani mara baada ya moshi kuanza kutanda hususani na ule moto ulioshika zuria kuzidisha kasi yake ya uwakaji, alizidi kuchanganyikiwa Zena na kulia kama mtoto mdogo hasa kila alivyomtazama Asha alikuwa kalegea mwili mzima hasemi wala hatazami.
"Ashaaaa mwaanaaanguuuu Ashaaaaa amkaa mamaaaa"
hakuweza kum beba kutokana na umli na nguvu chache alizokuwa nazo Zena lakini hakuweza kumuacha pia alijitahidi kumnyanyua sehemu za juu na kumbuluza vivyo hivyo kuelekea mlango wa kutokea nje mara baada ya kuona msaada umeenda kombo.
Lakini mara ghafra mlango ulifunguliwa kwa nguvu na mwanaume aliingia huku akiwa kachanganyikiwa mno haamini kile alichokuwa anakiona.
"Ashaaaaaa ASHA Wanguuu"
alitoa ukelele wa maumivu na mshangao Kamishna Shebby mara baada ya kuingia na kumkuta Zena akimkokota Asha aliyekuwa katika hali mbaya huku sehemu zake za chini ya tumbo kukionekana damu kumvuja kwa wingi.
"Mama Tangulia haraka nje kabisa Usishike hilo geti la mlangoni niachie mimi"
alinena Shebby na kutoa tahadhari ile huku akimnyanyua Asha mara baada ya kuona cheche zikizidi kwenye socket za umeme mule ndani na ule moto wa kwenye zuria ulianza kudaka masofa na mapazia makubwa yaliyokuwa Dirishani pale Sebuleni.
Alinyanyuka huku akiwa kam beba Asha Kamishana Shebby na kutoka nae haraka haraka na kuelekea alipopaki gari kule nje na kumkuta Zena akiwa kasimama huku ameeka mikono kichwani.
"Mama ingia kwenye gari twende mamaaa"
aliongea Shebby kwa sauti ya kazi zaidi kutokana na uchungu aliokuwa nao na kumfanya Zena afungue mlango wa nyuma na kutangulia kukaa pindi Shebby alipomuingiza Asha na kumlaza huku mapajani mwa Zena, ndipo baada ya kuufunga mlango Shebby alizunguka upande wake haraka na kuingia ndani ya gari kuondoka eneo lile ambalo tayari moto ulianza kuwa mkubwa kule kwenye ile nyumba na watu walianza kuzongea huku wengine wakipiga simu sehemu za usalama wa zimamoto kitu ambacho Zena na Shebby hawakukikumbuka wala kujali zaid walichanganyikiwa na hali aliyokuwa nayo Dokta Asha.
("Mr X MR X lazima nikuue lazima nikuue na Ninja wako malaya wako unayemtumia lazima nae Nimuueee Lazimaaa damu ya mchumbaangu ilipwe hata kama atabaki hai..")
aliwaza moyoni Shebby huku akiendeesha gari speed kuwahi hospitali kuokoa maisha ya mchumbaake kipenzi, mkewe mtarajiwa, thamani ya moyo wake hasa alipokuwa anakumbuka alivyotibiwa mguu wake, mwanamke aliyeamini ndie mke bora wa kumuoa kutokana na sura yake ya bashasha, upole na upendo wa dhati aliomuonesha kipindi anamtibu.
Nae si mwengine ni Dokta Asha ambae mpaka muda huo Shebby hakujua kuwa yule ndie Ninja wa kike aliyekuwa anatumiwa na Mr X.
* * * *
Kelele za watu pamoja na ving'ora vya polisi vilivyokuwa vinasikika upande wa chini ya jengo la Hoteli ile ndio zilizomsababisha Hussein bubu aamke alfajiri ile na kuelekea usawa wa dirisha la chumba chake kile alichopangiwa na Shebby kwenye ile hoteli.
Alishangaa sana mara baada ya kuona umati wa watu wengi sambamba na polisi wakiwa eneo la bustani kubwa iliyokuwa nyuma ya ile hoteli usawa wa vyumba vile vya upande aliokuwepo.
(He!! Nini tena kimetokea?")
alijiuliza mwenyewe kimoyo moyo baada ya kuona kuna ambulance iliyokuwa inapakia miili ya watu wawili iliyokutwa imeuawa mahala pale pa bustani alfajiri ile hali iliyomstua zaidi Hussein na kuamua kuvaa nguo zake harakaharaka ili apate kwenda kule chini akajionee mwenyewe kilichokuwa kinaendelea.
"Nini kimetokea hapa?"
alimuuliza swali bwana mmoja baada ya kushuka chini na kupenya penya kwenye jopo la watu mpaka alipofika nyuma ya yule bwana aliyekuwa amesimama sehemu za mbelembele kulipozungushiwa warning tape za police kutoruhusu mtu yeyote kusogea eneo lile la tukio zaidi ya wana usalama waliokuwa wanafanya kazi yao ya upelelezi na utafiti wa kina kujua kilichowasibu wale maiti waliokutwa pale.
"Kuna walinzi wameuawa hapa"
alijibu yule bwana
"Walinzi...!!"
alitaharuki Hussein
"Eee, bwana walinzi wamevamiwa na watu wasiojulikana na kuchomwa na vitu vya ncha kali shingoni kila mmoja"
"Kwani walikuwa wangapi?"
"wawili"
"na walinzi wengine je?"
"Wengine walikuwa upande wa mbele kule naona hawajasikia wenzao wlipokuwa wanauawa"
"Duh! kwa hiyo hao majambazi wamefanikiwa na kuiba?"
"Dah! ndugu yangu hata mimi mwenyewe mpita njia tu sio msemaji wa hoteli wala polisi we sikiliza tu fatilia utajua kila kitu"
Alijibu yule bwana mara baada ya kuona maswali ya Hussein yanazidi kuwa mengi.
Aliangalia huku na huko Hussein huku akiwa na maswali ya wale watu waliovamiwa upande ule wa nyuma ambao ulinzi ulikuwa mchache kutokana na kutoonekana kuna thamani kubwa ya kuchukua zaidi eneo lile lilikuwa kama la kupumzika wageni tu, tofauti na eneo la mbele ambapo pia kulikuwa na parking kubwa ya magari na ndio kulikuwa na mashine za ATM na milango ya kuingilia mule hotelini.
("sasa hawa majambazi gani wamevamia na kuua watu upande huu huku kukionekana hakuna madhara menggine yoyote upande wa mbele? Mh! itakuwa visasi tu hivi sio bure")
aliwaza Hussein huku anaangaza macho huku na huko na mara alipogeuka kwaajili ya kuondoka pale kuna mtu alimuona upande wa pili aliyemstusha kidogo macho yake.
("Haa!..!>>!)
alipigwa bumbuwazi huku akiwa haamini kama mtu anayemtazama pale ndie au sie na kuanza kusogea haraka ili avuke barabara eneo lile la upande wa pili kumuwahi kabla hajaondo kwani ni mtu ambae alikuwa anamkumbuka vizuri sana na alipomuona moyo wake ulistuka na kubadilisha mapigo kwani hakuwahi kufikiria kama atamuona tena mtu yule ambae sasa alikuwa mita chache tu mbele ya macho yake......
Alikuwa ni Cj4 nae alishamuona Hussein muda mwingi tu japo alijifanya
kutomuona na katika hali ya kumzuga na kumpoteza maboya alisubiria roli
moja ambalo lilikuwa linapita pale barabarani pindi lilipowaziba tu baina
yao alizunguka haraka na kuingia kwenye ile nyumba ya wageni ambayo ndio
alikuwa amefikia na kupandisha juu chumbani kwake mpaka dirishani na kuanza
kumuangalia Husein ambae sasa alionekana kutamtafuta.
("Mh!! kaendea wapi sasa yule kijana!!?")
alijiuliza Hussein kipindi akitafuta na kutomuona Cj4 ambae alichokuwa
anakumbuka yeye ni kwamba alikuwa mfungwa mwenzake kule gerezani ambae nae
alikuwa na mkasa kama wake na hata alipoingia gerezani kwa mara ya kwanza
alikuwa na maneno kama yale yale aliyoyaamini yeye kuwa Wanawake ni Wauaji
lakini kilichokuja kumshangaza baada ya kuzoena nae alikuja kutoweka kwa
kutoroka jera na jitihada zilifanywa za kumtafuta lakini hadi anatoka
gerezani alikuwa hajapatikana wala hata dariri za kuonekana kwake.
("Mh! mbona maajabu haya, au mzimu!!)
alijisemea moyoni Hussein mara baada ya kuona hakuna hata dariri ya uelekeo
wa yule mtu aliyekuwa amekusudia kumfata pale na kuamua kugeuza kurudi tena
kule hotelini.
Lakini wakati wote huo Cj4 alikuwa anamtazama Hussein na kumfanya atabasam
kw vile Hussein alivyoonekana kuhaha kwa kumtafuta yeye bila kujua
ameelekea wapi wala kutambua kama yuko nae pale kila siku.
* * * *
Kwa speed ya hatari yenye umakini wa ajabu Kamishna Shebby aliweza
kuiingiza gari mpaka hospitali kuu ya Jeshi la polisi Kilwa road na pindi
gari iliposimama walikuja watu wa machera haraka haraka kutokana pia na
kuitambua gari ile ilikuwa ya nani na aliposhuka tu ndio kabisa huduma za
kumtoa Asha garini zilifanywa haraka sana na kwa umakini mkubwa.
Alionekana kudata Kamishna Shebby huku akiwa anazunguka zunguka wodini
pindi Asha alipoingizwa chumba cha upasuaji bada ya kutolewa taarifa kuwa
alirushwa na mlipuko hivyo madaktari walihisi huenda pia kuna vyuma au
vibati vimeingia mwilini mwake hususani sehemu ya tumbo kulipooneaka kuvuja
damu kwa wingi.
("Ama zako ama zangu.. ama zako Ama zangu..")
alirudia rudia Shebby maneno haya huku akiimaliza korido na kurudi mwanzo
akifika mwisho anarudi tena mwanzo huku kichwa kakiinamisha wakati huo Zena
alikaa kwenye viti vya kusubiri wagonjwa akilia kwa uchungu.
Baada ya nusu saa alitoka Dokta mmoja kwenye chumba cha upasuaji.
"Vipi Dokta?!"
aliuliza Shebby kwa mshtuko huku akiwa na shauku ya kujua kilichoendelea
kwenye kile chumba cha upasuaji.
"Usijali mkuu, maendeleo ni mazuri tu inaonesha zaidi alipata mshtuko wa
moyo uliosababisha presha kuwa chini sana lakini hana majeraha makubwa wala
mwilini mwake hakuna kipande chochote cha chuma au chenye ncha kali, kwa
sasa wanarekebisha mshono aliokuwa nao ambao ndio ulifumka na kumsababishia
damu nyingi kuvuja"
majibu ya yule Dokta yalishusha presha aliyokuwa nayo awali Shebby kwa
kiasi kikubwa na ndipo alipomfata na mama (Zena) kumuelezea lile na kumtoa
wasiwasi kisha alimuachia kiasi cha ths laki moja kwa niaba ya dharula
yoyote itayojitokeza pale nae aliahidi kurudi baada ya muda mfupi ujao.
Alitoka na kuingia kwenye gari huku mawazo yake kichwani yakiwa kwenda
kukutana na Cj4 ambae alizidi kumuona mchawi wa mbinu kwa kugundua vitu
ambavyo yeye hakuvifikiria.
Lakini akiwa njiani alikumbuka vizuri maelezo ya yule daktari pindi
alipotoka chumba cha upasuaji na alipoyafikiria vizuri maneno yake kuna
kitu kimoja kilianza kumchanganya na kutoelewa.
("Mshonooo, mshonooo. Mh!! mbona sikumbuki kama Asha aliwahi kuwa na
mshono. mshonooo!!.. mshono gani tena huo?!!")
aliwaza Shebby na kujiuliza mwenyewe pindi alipokuwa njiani baada ya
kukumbuka vizuri maelezo ya yule daktari.
* * * *
"Huwezi amini Cj yaani kabla hata sijafika kwenye ile nyumba kwa macho
yangu nilishuhudia mlipuko upande wa juu na nilipoingia sikuamini hali
niliyomkuta nae Asha .. Daaah!! Mr X naamini nitapomuua nitapata thawabu
Dah!"
aliongea Shebby mara walipokutana kwa siri na Cj4.
"Kwa hiyo mchumbaako vipi?"
"Mungu amesaidia nimemuacha hospitali kwa matibabu zaidi ila kuna kitu
sijakielewa"
"Kipi hiko?"
"Nimeambiwa jeraha lililokuwa linavuja damu tumboni kwa Asha ni la mshono.."
aliongea Shebby kauli ambayo Cj4 aliichekecha harakaharaka na kupata
uhakika sasa kua mtoto wa Hussein ambae ni mke wa Kamishna Shebby ndie yule
Ninja aliyemsaidia usiku baada ya kuchomwa na kisu cha kininja tumboni
hivyo alijua mshono unaozungumziwa pale laima atakuwa amejishona mwenyewe
usiku uliopita na kutokana n msukosuko wa bomu umefumka.
"Sasa neno Mshono limekuchanganya nini? mbona mi naona kawaida."
alijibu Cj4 kwa kumzunguka Shebby kwani hakutaka kabisa agundue mapema
mchumbaake ni nani.
"Sikia Cj, sijawahi kumuona na mshono Asha wala hajawahi kunambia hiko
kitu."
"hahahaha, tatizo Shebby unapanik mapema, nataka ukumbuke kuwa mshono
unamaanisha sehemu ambayo iliwahi kufumka ikazibwa upya. sasa unajuaje kama
kipindi cha nyuma mchumbaako aliwahi kufumka sehemu hizo?"
"Mh! sasa ndio uachie na kuvuja damu?"
"Inawezekana kishindo kilikuwa kikubwa.. Ila mi nataka nikushauri kuwa
fanya jitihada mapema tu umuoe Asha"
"Mh! Cj mi naona kwanza tumalize hili la mr X"
"Hapana, unajua mr X anatumia akili na mambo yake mengi aliyaeka kwenye
mipango kabla hayajatokea. sasa ili akuchanganye anataka kudili kwanza na
watu uwapendao. Ndio maana nakwambia muoe kwanza Asha mueke jilani harafu
hapo sasa hata mr X mwenyewe utakuwa umeshamzunguka"
Ushauli wa Cj4 hakuutarajia kabisa Kamishna Shebby lakini hakutaka kuupinga
kwani moyo wake tayari ulikuwa unamuamini sana Cj4 na kumkubali hivyo
aliongea na wazazi wake ambao walikubali lifanyike hilo jambo haraka
hususani mzee Mwinchande limpongeza mno mwanae kwa maamuzi aliyofikia
lakini kwa kile kilichotokea kwa Asha Shebby alizificha taarifa zile
nyumbani kwao kwa kuogopa kuwatisha pia kwa kuzingatia ushauri wa awali
aliopewa na Cj4 na hata Hussein babu bubu hakuambiwa kilichompata mwanae
zaidi ya kuja kusikia habari za nyumba kuwaka moto huku akidanganywa ni kwa
shoti ya umeme kipindi ambacho wakazi wote (Zena na Asha)
hawakuwepo pale nyumbani.
* * * * *
Siku ileile masaa machache baada ya Shebby kuondoka Asha alirejewa na
fahamu wakati huo tayari madaktari walikuwa wamemaliza kumshona vizuri
sehemu ile ya chini ya tumbo kulipoachia.
Kutokana na kupungukiwa damu ililazimika kuongezewa chupa nne za damu na
usiku huo alilala pale wodini huku upande wa Shebby alihaha na kufanikiwa
kuwakodia nyumba nyengine nzuri maeneo ya jilani na ile hoteli aliyopngiwa
Hussein kwa kujua kuwa pale amewaeka kwenye usalama kwa uwepo wa rada za
Cj4.
Baada ya kila kitu kuwa sawa upande wa Cj4 siku hiyo asubuhi na mapema
alitoka kinyemela pale alipokuwa anaishi pasi na kumuarifu Shebby na
alielekea kule hospitali akiwa amevaa sare zake za kipolisi
zilizomtambulisha kama Inspecta na kufanikiwa kuingia wodini kumuona
mgonjwa ambae siku hiyo ndio ilikuwa siku yake ya kuruhusiwa.
Hakukuwa na vizuizi wala maswali mengi pindi alipotaka kukutana na yule
mgonjwa, ila kukaibuka mstuko na taharuki kubwa kutoka kwa yule mgonjwa
ambae ni Asha pindi alipokutanisha macho na Cj4 ambae nae alistuka kidogo
baada ya yale macho kuyakumbuka vizuri siku ile ya ajali ya kule chalinze
ambayo ilipelekea kupoteza kwa maisha mtu muhimu aliyetakiwa kuhojiwa juu
ya upelelezi wa kum baini Mr X.