NUKUU YA LEO
Change will not come if we wait for some other person or some other time. We are the ones we've been waiting for. We are the change that we seek.
Mabadiliko hayatokuja kama tukisubiri watu wengine au muda mwingine, sisi ndio tumekuwa tukisubiriwa, sisi ndio mabadiliko yaliyokuwa yanatafutwa
Haya maneno yamewahi kutamkwa na mwanasheria, mwalimu wa sheria na Rais wa 44 wa Taifa la marekani Bw. Barack Hussein Obama.
Barack Obama alizaliwa tar. Kama ya leo 4/8/1961 Katika mji Honolulu-Hawaii miaka 2 baada ya kuwa jimbo la 50 kuwa ndani ya muungano wa majimbo ya marekani.
Barack obama amekuwa rais wa kwanza mmarekani mweusi kukaa na kufanya kazi ndani ya ofisi maarufu ya oval office na white house kwa ujumla.
Obama amezaliwa na mama mzungu na baba mwafrika kutoka kenya barack obama sr.
Obama atakumbukwa kwa kuwa na utawala wenye mafanikio na kurudisha taifa la marekani katika nafasi yake baada ya kuporomoka kiuchumi kutokana na vita vya mashariki ya kati.
Utawala wa obama umefanya mengi katika ulinzi wa marekani ikiwa ni pamoja na kumuuwa mtu walieamini ni gaidi no 1 duniani Osama bin Laden.
Obama amechukuwa Tuzo ya Nobel mwaka 2009 "peace prize" kwa kutengeneza na kujenga diplomasia ya kimataifa na ulimwengu kwa ujumla.
Obama ana mke mmoja ( michelle ) na mabinti 2 ( malia na sasha) .
Obama alikuwa role model wangu toka nimemfahamu hadi leo hasa namna ya kudeliver speech na audience confidence. The man is good in every aspect you know in politics..
Out of politics; he's also a caring dady of two applaudable daugheters..
Kuna mengi ya kuandika kuhusu obama lakini muda hautoshi....
Happy born day BO