Makapuku Forum

Chelsea Vs Bayern Munich (2-3) All Goals & Extend…:
 
Reactions: Lee
TOP TEN
Wadau kama kawaida kumi kubwa ni muda wa jioni
Halafu leo nimefurahi uwepo wa Linamo na Sakayo...ni jambo jema wadada wamerejea ila Mama Mchungaji bado haonekani(tumemmiss)
Leo tuangalie wezi/vibaka au matukio 10 ya wizi maarufu yaliyowahi kutokea tena kwa mafanikio
Karibuni
.......
 
10/2010 Credit Lyonnais Paris Burglars Mwaka 2010 wezi waliotukuka walifanikiwa kuvunja na kuiba kijanja katika Benki ya Mikopo ya Lyon iliyopo katikati ya jiji la Paris na kuiba viboksi vya kutunzia vito na pesa vyenye thamani ya mamilioni ya Euro pamoja na pesa taslimu.
Walifaniliwa kuingia kupitia mbinu za kijanja na kuvuruga mifump yotee ya ulinzi ma hivyo kuiba kiulaini bila kushtukiwa
Pia mwaka 2011 genge hilo lilifanya kufuru nyingine
Hadi sasa umekosekana ushahidi wa kiwezesha kuwashtaki
........
 
9/French "Vacuum" Gang Kuanzia mwaka 2006 huko Ufaransa liliibuka genge la Kihalifu lisilofahamika la vibaka wajanjawajanja ambao waliimba na kusafisha kabisa Supamarket kwa kutumia kifaa maalumu walichokibuni cha fagio la vakyumu
Waligundua udhaifiu katika utunzaji fedha wa Supermarket ya Monoprix na hivyo kutumia fursa vizuri kwa kubuni fagio hilo la kuiibia kwenye vacuum tubes za itumzaji fedha
Hadi kufika 2011 walikuwa washaiba USD 800,000 kwa kutekeleza matukio 15 yenye mafanikio mkubwa
Kamera za CCTV ziliambulia kuona watu waliovaa mask tu
Hawa jamaa walikuwa wakiiba usiku
............
 
8/Carl Gugasian Jamaa ni maarufu kwa jina la The Friday Night Bank Robber
Huyu ni kibaka maoni mwenye Shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania huko nchini Marekani ambaye aliamua kutumia usomi wake kufanikishia matukio ya kijambazi yenye weledi
Alipohitimu tu akaanza kuiba magari katika casino 8 tofauti na kuyatumia kwenye matukio yake ya kihalifu
Aliprmdelra zaidi kuiba kwenye mabemki siku za Ijumaa na alifika dakika 5 kabla ya benki kufungwa na kutumia dk 3 tu kubeba mpunga na kusepa zake bila kukamatwa ambapo alienda kuzihifadhi pesa na vitendea kazi kwenye handaki porini kisha kusepahadi mambo yakipoa anarudi kuzichukua
.........
 
7/Paris Modern Art Museum Barglary Mwezi May 2010 wezi alivunja Makumbusho ya sanaa ya Paris na kuiba kazi za kisanii kama vile za Picasso and Matisse ambazo zilikuwa na thamani ya Euro milioni 100
Wizi huo ukaja kugundulika keshowe asubuhi muda wa saa 1 na kuaminika kwamba vitu vilivyoibiwa vinaerza kufika thamani ya Euro Milioni 430
Hadi kufikia mwaka 2012 hakukuwa na mtu yoyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo
........
 
6/Derek 'Bertie' Smalls
Huyu alikuwa ni mwizi aliyebobea huko Uingereza katika miaka ya 1960
Kabla ya miaka ya 1970 alikuwa ni mwizi mwenye jina kubwa kwenye mitaa ya jiji la London
Mwezi Februari 1970 aliongoza genge liitwalo Wembley Mob kuvamia na kuiba pesa kiasi cha Pauni 240,000katika benki ya Barclays kiasi ambacho ni rekodi kwa kipindi hicho
Kisha akapanda treni na kutimkia jijini Paris kusikilizia upepo na kuponda raha
Baada ya juahidiwa kupewa kinga na mwendesha mashtaka iwapo atakubali kuelezea wizi ulivyofanyika kwaajili ya faida ya Polisi siku zijazo alikubali kurudi na kutoboa siri ambapo genge zima lilipigwa mvua ya miaka 100 jela ila yeue akasamehewa
Huyu jamaa ni mfano halisi wa Yuda Eskarioti
.............
 
Huyu yuda kweli

策熬失控了惡奧
 
Wewe ndio yuda maana umenikalisha hapa hata kuendrlea huendelei . Unazingua madenge..
Mdau na mimi binadamu kama ww siishi kwenye server za Jf bali kitaa hivyo samtaimu mambo yanabana
Mgano nilikuwa nazungumza na shemeji yako
Ila nitazimaliza baada ya muda
.....
 
Mdau na mimi binadamu kama ww siishi kwenye server za Jf bali kitaa hivyo samtaimu mambo yanabana
Mgano nilikuwa nazungumza na shemeji yako
Ila nitazimaliza baada ya muda
.....
Sasa U yuda wangu uko wapi..?
Acha uongo ujue ulikua unakimbizana na bata sio shem wala nini!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…