Makapuku Forum

....hata kwa mama Said yule mpika chapati bonge bonge waiti uko tayari. Maana huyu waiti ni mrembo na ni fundi kweli sina hakika anatokea wilaya gani tanga. Si unajua mimi mgeni humu sijui mengi
Kote nitamsindikiza binamu yangu usijal
 
5/Hippo
Kiuhalisia kiboko ni herbivorous yaani anakula majani kama ng'ombe tu ila mara kibao tu keshabambwa akijichana na kitoweo a.k.a nyama
Wanapatikana kwa wingi barani Afrika ambayo huotwapia River horse yaani farasi wa mtoni
Silaha yake kuu ni meno(jaw) na Mara kibao hujeruhi na kuua watu
.....
 
...kwa kweli anko wangu umenifumbua macho, yaani nafurahia kuwa na wewe anko, umenifungua macho. Yaani naiona talaka inaniita kwa furaha.
Sasa nifanyeje anko, si unajua wewe ndo mshauri wangu mkuu ninayekutegemea
Uachweeee tu hakuna namna binamu
 
Baba D acha uchochezi


Mjomba wangu sio mchochezi, mimi kwa vitumbua kwa kweli utanisema tu vibaya, navipenda kweli kweli, tena wakivitia na mayai basi ni kujinoma kutwa mara tatu. Sisi watu wa mchele tunajijua, asubuhi vitumbua, mchana biriani na usiku wali nazi. Asubuhi tunapasha kipora
😀
 
Hivi upo upande upi binamu jamaan kwa mpendwa wako au kwa mama mchuchu

...yaani nitakuapa majibu kama ya Yesu, .....ya kaisari...na ya Mungu ..... Jiongeze, wengine tuko tofauti mama ni mmoja tu baba mbalimbali
 
Hapo kwa ras simba binamu ndio penye uchochezi ujue
 
4/African Lion
Simba mnyama anatisha ....achana na yule mchovu wa pale Msimbazi anayesumbuliwa na Vyura
Silaha yake kubwa ni kasi,mbinu na meno makali
Kitu kibaya zaidi ni kwamba huku Bongo kuna simba hukaa hadi juu ya miti
......
 
Ninafurahi umekuja salama, vipi una mpenzi?


Taarifa: Hili swali sijauliza mimi, msije mkaanza maneno yenu ya kuniharibia masuala yangu muhimu. Sasa hivi niko mahakamani naapa kuwa sijauliza mimi
Ana mume huyo binamu humu anaitwa Bailly5
 
Kwa nn talaka?? Kaeni muyamalize msiachane

Madame S


...,hakuna shida kati yetu, talaka nilikuwa naiongelea ya mjomba wangu anataka kupewa talaka. mimi penzi bado jipya sana yaani tunaitana honey na sweet , mara sugar , dearest na mengine kama hayo, tukianza kuitana majina yetu ya kuzaliwa ujue talaka inakaribia
 
Kuna ukweli wowote juu ya Papa akiona viganja na unyayo hakuachi?


...sijui kama ni kweli, na wengine wanasemaga eti ukiogelea uchi kabisa (skin dive) huyu papa anabaki kukushangaa tu anaanza kutafuta kioo na yeye ajiangalie kama mnafanana. Haya ni maswali huwa tunaulizana kwenye kahawa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…