Makapuku Forum

TOP TEN
Unampenda mwanamuziki gani?
Mimi kwa bongo namkubali Albert Mangwea a.k.a Ngwair mzee waDakika 3 na kama vipi msikilize kwenye Mitungi,blant,mikasi naamini jamaa ni zaidi ya Kiba na Diamond ila hakuwa na nidhamu ya kukitumia kipaji alochojaaliwa na Mwenyezi Mungu mwisho akafa akiwa teja na maskini
Kwa mamtoni huniambii kitu kwa 20ac Umar Shakur huyu wimbo ambao umenigusa ni Dear Mama wengine ni Michael Jackson mzee wa Thriller bila kumsahau mfalme wangu wa muda woteBob Marley na song lake la I'll shot a shariff....twende sasa
.
Nakuletea wakali kumi waliotikisa dunia
Ni kalist ambalo nimeokotezaokoteza hivyo sitaweza kumridhisha kila mtu
Karibuni
.......
 
10/Pink Floyd
Ni kundi la muziki la miaka ile ambayo kijana kuvaa suruali ya bwanga na maviatu kama skuna ndio ilikuwa fasheni ya kijanja
Ni kundi la wanamuziki watano yaani David Gilmomour,Syd Berrett,Nick Mason,Roger Waters na mmoja hivi nimemsahau
Walitamba na vibao kibao kama vile The Dark Side Of The Moon ambacho kulibamba
Kingine ni Astronomy Domine ila utapenda pia The Happiest Days Of Our Lives
.......
 
kibongo bongo namkubali fid q.. mamtoni ni jay z na marehemu wako jako
 
9/Fela Kuti
Ni mwanamuziki mwenye asili ya Nigeria
Alizaliwa mwaka 1938 na kufariki dunia mwaka 1997...kwa mujibu wa Mwanafalsafa nasikia jamaa Alikufa kwa ngoma kutokana na tabia yake ya kupenda starehe na vidosho kupitiliza
Alitamba na ngoma kibao ila kwa uchache tu zitafute Teacher Don't Teach Me Nonsense hapa sijui alilenga nini kuhusu walimu wetu wale...
Ila pia kaimba Shakara na mwingine uitwao Water No Get Enemy
Alikuwa mkali wa Afro--Beat
......
 
8/Madonna
Ni mwanamuziki wa Kimarekani aliyezaliwa Agosti 16 1958 yaani tayari ni bibi
Alikuwa na vituko kumzidi huyu Lady Gaga yaani kamzidi kwa kila kitu kuanzia kukaa uchi hadi vituko stejini na maisha binafsi achilia mbali mkwanja...anapenda pia kujirusha na viMario
Alitamba na Like A Virgin, Like A Prayer kisha akakandamizia na Vogue bila kusahau Hung Up
....
 
 
7/Led Zeppelin
Ni bendi ya muziki wa rock kutoka London huko kwa Malkia Elizabeth iliyoanzishwa mwaka 1968
Iliundwa vijana wafuatao Robert Plant,Jimmy Page,John Paul Jones & John Bonham....hivyo jamaa wakakunguta vyombo na kuimba na kuishika dunia
Ngoma zao chache ni kama vile Stairway To Heaven,Whola Lotta Love ukivisikiliza na usielewe basi una gundu
Pia kuna Kashmir na Immigrant Song
.....

 

Mazishi ya Bradley Lowery: Maelfu wafika kumuaga shabiki aliyegusa nyoyo za wengi....

.........Maelfu ya watu walijitokeza katika barabara za kuelekea nyumbani kwa Bradley Lowery, shabiki wa klabu ya Sunderland FC ya Uingereza, kutoa heshima zao za mwisho.

..


Ibada ya wafu ilifanyika katika kanisa la Mtakatifu Yusufu kijijini mwao, wengi wakimsifu sana mvulana huyo kwa ukakamavu wake na sifa alizojilimbikizia....

Maandamano yalikuwa sio ya nchii hiii..




Jermain Defoe aliyeonekana kutekwa na hisia, alikuwa amevalia jezi ya England yenye jina la Bradley




Meneja wa zamani wa Sunderland David Moyes alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri katika soka waliohudhuria mazishin hayo





Barabara za kuelekea kanisa la Mtakatifu Yusufu zilipambwa kwa puto na mabango yenye ujumbe wa kutoa heshima kwa Lowery.

Wengine waliacha ujumbe nje ya uwanja wa Sunderland wa Stadium of Light.

Waombolezaji walifika kwa wingi kanisani, hivi kwamba wengine walikaa nje.

Jamaa za Bradley walivalia jezi za soka, kukumbuka upendo aliokuwa nao kwa mchezo huo.

Mamake Gemma aliambia waliohudhuria mazishi hayo: "Alikuwa na tabasamu kubwa na la kupendeza hivi kwamba lilikuwa lingeangaza chumba chochote kile. Ni shujaa mwenye ujasiri, ametuacha.

"Aligusa nyoyo za wengi - aliwatia moyo watu wengi. Mwana wetu mpendwa, ndugu - nyota ya kupendeza.

"Ingawa wakati uliokuwa nasi ulikuwa mfupi, ni lazima una kazi ya kufanya huko mbinguni na malaika kwani Mungu amekuchagua wewe.

"Kwa sasa, mtoto wangu kwaheri, Hatu tutakapoonana tena shujaa wetu huko juu mbinguni."...


Ila kiukweli watu wameonesha upendo wa kiwango cha hali ya juu....zicheki picha watu walivoamua kufanya. .

Karibia kila barabara mtaani zilitumdikwa pichaa.
...moyes alikuwepooo

upendo uliojeee.....





Pumzika kwa amani kipenzi chetu....
 
6/Bob Marley
Kama humkubali Robert Nesta Marley kisa tu alikuwa akipuliza moshi wa bangi basi kajinyonge tu kwangu mimi ndo Mfalme wa kweli wa muziki ...aliimba karibu kila kila kitu kuhusu maisha
Alizaliwa mwaka 1945 na jufariki mwaka 1981 akiwa na miaka 36 tu
Sababu ya kifo chake ni saratani liliyosabishwa na kidole alichoumia wakati akicheza soka na kukataa ushauri wa madaktari kukiondoa sababu tu ya imani ya kirastafarah
Alizikwa kaburini pamoja na kipisi cha bangi,gitaa lake na biblia iliyofunguliwa ikurasa wa Zaburi 23(kuhusu ukurasa sina hakika km nipo sawa)
Wimbo wake wa One Love umekuwa kama kauli mbiu tukufu dunia nzima
Vipi kuhusu I Shot A Sheriff ?
......
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…