Liverpool na Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, ambaye thamani yake ni pauni milioni 65. (Sun)
Kipa wa Manchester United David de Gea, 26, anataka kujiunga na Real Madrid msimu huu na amemuambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake. (Don Balon)
Chelsea watakamilisha usajili wa kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kutoka Monaco kwa pauni milioni 39.7 katika saa 24 zijazo, ingawa mchezaji huyo atakosa mechi kadhaa za mwanzo kutokana na kuwa majeruhi. (Daily Express)
Barcelona wameacha kumfuatilia beki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, baada ya klabu hiyo ya Uhispania kufikia makubaliano ya kumsajili Nelson Semedo, 23 kutoka Benfica. (London Evening Standard)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka uhamisho wa Kyle Walker, 27, kwenda Man City uharakishwe ili wapate fedha za kusajili wachezaji wengine. (Daily Mail)