Antonio Rudiger anakaribia kukamilisha uhamisho wake kutoka Roma kwenda Chelsea kwa pauni milioni 34 na mkataba utakamilika katika saa 24-48 zijazo (Sky)
Arsenal wameweka wazi kuwa hawatomuuza Alexis Sanchez au Alex Oxlade- Chamberlain kwenda katika timu yoyote hasimu ya EPL. Sanchez ananyatiwa na Manchester City huku Oxlade-Chamberlain akihusishwa na Liverpool (Daily Star)
Arsenal wameongeza dau lao hadi pauni milioni 40 kutaka kumsajili winga Thomas Lemar, 21 kutoka Monaco, baada ya pauni milioni 35 za awali kukataliwa (L'Equipe)
Meneja Antonio Conte atarejea Chelsea siku ya Jumatatu kutoka likizo na kutaka mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kushindwa kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton (Express)
Newcastle wamekuwa na mazungumzo na Middlesbrough ya kutaka kumsajili winga Adama Traore, 21 ambaye huenda akagharimu hadi pauni milioni 20 (Chronicle).