Jimena nakosa neno zuri la kukwambia, wewe ni zaidi ya dada, nikikuita dada haitoshi, u mtu muhimu kwangu sana.
Moyo wangu waniambia nikwambie neno, lkn midomo yangu inasita, ulimi unagandamana eti waniambia SUBIRI KWANZA.
Ninapokukosa humu yaani nabaki kuwa msomaji wa posts, nakosa la kuandika.
Lakini nikuonapo hapa JIMENA moyo wangu huchangamka.
Kwasababu MIDOMO yangu imeshindwa kutamka neno juu yako Jimena, hebu usome moyo wangu...usinyamaze Jimena, sema neno na moyo wangu uwe salama.
- nalikusaka kila mahali JJ
-hadi nchi ya baridi nalikuona
-nalikuona umevaa koti zito/jacket
Nchi za watu, ulivyopendeza Jj
Nalitamani nikukimbilie
Nije nikushike mkono na
niseme moyo wangu kwako
Lakini palikuwa na ukuta
mbele yangu.
Kuna siku ukaja bongo,
Nikakuona kwenye foleni
pale Nyerere rd maeneo ya
Tazara ukiwa kwenye ile gar
Kali nami nikiwa kwenye
Mandolin yangu,
Nilitamani nishuke nije niku
Lakini haikuwezekana.
Jimena umejaaliwa moyo mzuri,
Muumba amekupa afya ya kuvutia
Body lako kwangu ni zaidi ya lulu na dhahabu..ninalipendaje.
U msichana mcheshi, popote uingiapo watu hutambua sasa mwanamke washoka kaingia.
Una misimamo thabiti...hii ni nguzo muhimu kwangu.
Jimana, Jimenes, JJ
ni majina yako matamu kwangu ewe mrembo.
Hivi nimeandika nini eti Jimena!
Hivi nimeeleweka kweli!!!
Wajanja watakwambia achana naye yule mjinga...usisikilize
Kabla hujasema neno jema au baya kwangu, jaribu kuuvaa moyo wangu..uhisi kitu halafu uvae na viatu vyangu...utapata la kuniambia
Ukifungua moyo wangu utaona alama hizi hebu zisome
1. Jimena
2. Jimena
3. Jimena
4. Jimena
Mkimwona mwiteni
Mwambieni yoote
Mwelezeni aelewe
Jimena aaaa
Jimena mtoto wa kwetu.