Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kabisa!!!!nina story ya uchungu iliwahi tokea tukiwa wadogo sikuelewa...kuna watu wangu wa karibu walifiwa na baba wakaachiwa mji,mama yao na wakwe wakabaki hapo ,mtoto wao mmoja siku moja alichukua mkaa akachora nyumba nzima....ilikua kesi nzito,mama akalaumiwa na kuambiwa amemfundisha mtoto,akatukanwa sana na kunyanganywa watoto na kufukuzwa hajui kulea

Nilipokua mtu mzima na Mungu kunijalia kupata watoto ,siku moja mwanangu wa chekechea alifundishwa shule kuandika jina,akajua kuandika na langu....aliporudi nyumbani alichora nyumba nzima jina langu na lake......ningemlaumu nani?

Nililia sana nikakumbuka yule mama alivyohukumiwa,nilitamani niwaelezee bahati mbaya wote hawapo
Aisee, watoto ndivyo walivyo
 
2 Mambo ya Nyakati 1

1.Basi Suleimani, mwana wa Daudi ,alithibitishwa katika ufalme wake naye BWANA,Mungu wake ,alikuwa pamoja naye akamtukuza mno.

Maombi yangu leo,MUNGU akuthibitishe katika nafasi uliyonayo kama Suleimani mwana wa Daudi alivyothibitishwa na BWANA Mungu.Awe nawe katika kila hatua unayopita.Wanaokupiga vita katika ndoa,kazi,shule,biashara,maisha,ujirani,undugu ,wana okukandamiza kiroho,kimwili,kiakili WAKASHINDWE katika jina lipitalo majina yote Jina la Yesu Kristo Amen Asante...Kazi njema
Amen
 
FAIDA 8 ZA KITUNGUU MAJI KAMA DAWA.

NA DR. SEIF EL BAALAWY KUTOKA ALJALILA HERBS.

Usijali machozi yanayoletwa na
vitunguu maji ni kama karata dume katika kupigana na
magonjwa. Ni mmea mahiri katika
familia ya lily, vinakupa faida
nyingi kiafya pia yaongeza ladha
nzuri katika chakula chako.

Tuangalia haraka haraka faida
zitokanazo na kula vitunguu maji.

1. Vitunguu maji vina kemikali ambazo
zinasaidia kazi ya Vitamini C katika mwili wako, hivyo kukuongezea kinga ya mwili.

2. Vitunguu maji vinakemikali aina ya
chromium ambayo inasaidia
kudhibiti sukari katika damu.

3. Kwa karne nyingi, vitunguu maji
vimekuwa vikitumika kupunguza uvimbe na kuponya maambukizi.

4. Unafurahia vitunguu maji vilivyokatwa kwenye chakula?
Kama ndio basi furahi! Vitunguu vibichi vinasaidia kutegeneza cholesterol nzuri (HDL) hivyo kuufanya moyo wako kuwa na afya njema.

5. Kemikali yenye nguvu iitwa
quercetin katika vitunguu maji
inatambulika kwa kusaidia kwa
kiasi kikubwa kuzuia saratani
(cancer).

6. Umeumwa na nyuki? Weka
juice ya kitunguu maji eneo ambalo
umeumwa upate nafuu ya maumivu na uvimbe kutowasha.

7. Vitunguu maji vinasaidia kuzuia
vidonda vya tumbo.

8. Sehemu ya kijani (kitunguu maji
kutoka shambani) imejaa
Vitamini A kwahiyo itumie mara kwa mara.
5cb31f56993837221fd9c84fcce4091a.jpg
 
ADOLF EICHMANN:Alinyongwa Kwasababu Hakupenda Kuuliza Maswali (kuhoji).

Adolf Eichmann, mtawala na mchapakazi mkubwa katika serikali ya kinazi kule ujerumani zama za Hitler. Kuanzia mwaka 1942 yeye ndio alikuwa amepewa jukumu la kusafirisha Wayahudi wa ulaya na kuwapeleka kwenye kambi za mateso nchini Poland, na maeneo ya Auschwitz. Hili ndilo lilikuwa ‘Suluhisho la mwisho’ (Final Solution) la Hitler katika mpango wake wa kuwaua Mayahudi walokuwa wakiishi kwenye ardhi iliyokuwa inakaliwa na majeshi ya Ujeruman. Eichmann hakuhusika kwa namna yoyote na sera za mauwaji hayo, hayo hayakuwa mawazo yake. Lakini alihusika kwa kiasi kikubwa katika kupangilia mifumo ya reli iliyofanikisha ukatili ule. Tangu miaka ya 1930 Wanazi walikuwa wametunga sheria ambazo zilichukuwa kabisa haki za Wayahudi. Hitler alilaumu wayahudi kwa kila baya lililotokea ujeruman na akaweka nadhiri kulipiza kisasi dhidi yao. Sheria zilizotungwa ziliwazuia wayahudi kwenda kwenye shule za serikali, kusalimisha pesa na mali zao na walilazimika kuvaa nguo zenye nyota ya njano. Wayahudi walizungukwa na kulazimishwa kuishi kwenye Maghetto –miji yenye misongamano mikubwa ambayo ilikuwa kama jela kwa kwao. Chakula kilikuwa shida, na maisha yalikuwa magumu kwa wayahudi. Lakini ‘Suluhisho la Mwisho’ ilianzisha hatua nyingine ya uovu. Maamuzi ya Hitler kuuwa mamilioni ya wayahudi kwasabu tu ya rangi zao (inavyosemakana) ilimaanisha kwamba Wanazi walihitaji njia ya kuwaondoa wayahudi nje ya miji na kuwapeleka maeneo ambayo wanaweza kuwaua kwa wingi.

Kambi za mateso zilizokuwepo ziligeuzwa kuwa viwanda kwa ajili ya kuwapilizia gesi na kuwachoma mamia ya watu kila siku (inavyosemekana…nina sababu za kusema hivi). Kwakuwa kambi hizi nyingi zilikuwa nchini Poland, ililazimika apatikane mtu mmoja wa kuandaa treni ambazo zitakuwa zinasafirisha wayahudi kwenye maeneo yao vifo (Akhera au Kuzimu). Pamoja na kwamba bwana Eichmann kazi yake ilikuwa ni kuketi ofisini kupanga karatasi zenye majina ya wahanga na kupokea simu hapa na pale, mamilioni walikufa kama matokeo ya kazi yake. Wengine walikufa kwa typhoid au njaa, na wengine walilazimishwa kufanya kazi ngumu mpaka kufa, lakini wengi waliuawa kwa gesi. Kutokea upande wa ujerumani, Eichmann alihakikisha treni zinaondoka na kufika kwa muda uliopangwa. Ufanisi wake yeye na wasaidizi wake uliwezesha kufanyika mauwaji ya kinyama. Ndani ya treni hizo walijazwa wanaume, wanawake na watoto kwenye safari ndefu na chungu kuelekea kufa, mara nyingi bila ya chakula wala maji, wakati mwingine kwenye joto au baridi kali. Wengi walifia safarini, hasa wagonjwa na vikongwe.

Walionusurika vifo vya njiani, walifika kwenye makambi wakiwa wamechoka huku wakilazimishwa kuingia kwenye chemba kwa kuzugwa kuwa ni vyumba vya kuogea na kulazimishwa kuvuliwa nguo. Baada ya hapo, vyumba hufungwa kwa nje. Ni kwa staili hii ndio Wanazi wakatekeleza mauwaji kwa gesi aina ya Zyklon. Miili yao ikachomwa moto na mali zao zikataifishwa. Ukipata bahati nzuri ya kutochaguliwa kifo cha namna hii, hatma yako ilikuwa ni kufanya kazi katika mazingira magumu bila chakula.
Askari wa kinazi waliwapiga mijeredi au hata risasi kwa ajili ya kujifurahisha. Mchango wa Eichmann ni mkubwa sana kwenye jinai hizi. Hata hivyo, baada ya vita ya pili ya dunia alifanikiwa kutoroka na kufika Argentina, ambapo aliishi kwa siri miaka kadhaa. Mnamo mwaka, makachero wa jeshi la polisi la Israel walimvizia katika mji wa Buenos Aires na kumkamata kasha wakampeleka nchini Israel ilikujibu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Unadhani Eichmann alikuwa mtu fulani muovu, shetani, mtu aliyependa au kufurahia maumivu ya watu wengine? Watu wengi waliamini hivyo kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa. Kama sio hivyo, basi ni nini kilisababisha jamaa huyu kushiriki katika mauwaji haya? Kwa miaka kadha huyu bwana kazi yake ilikuwa ni kutafuta ufanisi wa kuwapeleka watu kuzimu (Akhera). Bila shaka, ni zimwi pekee ndio linaweza kupata usingizi usiku baada ya kufanya unyama ule. Mwanafalsafa Hannah Arendt (1906–75), myahudi mwenye asili ya Ujeruman aliyehamia marekani aliwahi kuwa mtoa taarifa wa kesi ya Eichmann kwenye gazeti la New Yorker. Mwana mama huyo alivutiwa sana na kutamani (kawaida ya wanafalsafa kuwa na uchu wa kujua mambo) kukutana uso kwa uso na mtu ambaye ni mabaki ya utawala wa kiimla wa kinazi, dola ambayo ndani yake kulilikuwa na fursa ndogo sana kwa raia wake kufikiri au kohoji (little room for reasoning). Hannah alikuwa na uchu wa kumuelewa kiumbe/mtu huyu, ili apate walau hisia na kuona ni kwa jinsi gani Eichmann aliweza kufanya mambo yale ya kutisha. Yaani inawezekani vipi mtu mwenye akili zake timamu kushiriki kwenye unyama ule kwa binadamu wenzake?

Eichmann na Arendt waliishi katika vipindi viwili tofauti vya unazi. Yeye alibahatika kuwakimbia wanazi na kutimkia ufaransa, lakin hatimaye kufanikiwa kuwa raia wa marekani. Akiwa binti mdogo wa miaka 18 katika chuo kikuu cha Marburg aliolewa na mwalimu wake, alikuwa mwanafalsa Martin Heidegger. Kipindi hicho Heidegger alikuwa ‘busy’ na kuandika kitabu chake cha Being and Time (1962), moja ya vitabu vigumu kabisa kiasi baadhi yetu tunaheshimu mchango wake katika falsafa. Baadae akawa mwanachama kindakindaki wa kinazi, akiunga mkono sera za kupinga uyahudi. Mpaka akafikia kuondosha jina la rafiki yake wa zamani, mwanafalsafa Edmund Husserl, kwenye ukurasa wa ‘dedication’ katika kitabu chake cha Being and Time kwasababu Edmund alikuwa myahudi. Lakini kwa sasa, mwana mama Hannah anajikuta yupo Jerusalem, na anapaswa kukutana na mtu aliyeishi kwenye unazi ambao ni tofauti na ule wa mumewe. Mbele yake amesimama mtu ambaye ni wa kawaida tu, mtu aliyechagua kutojisumbua kufikiria kwa kile alichokuwa anakifanya. Kushindwa kwake kufikiri kabla ya kutenda, kulikuwa na matokeo mabaya. Hannah Alitegemea kuwa mbele yake angemuona mtumwenye sura ya uovu. Lakini haikuwa kama alivyodhani, sura na muonekano wa Eichmann haukuwa ule wa mtu muovu. Alikutana na mtu mwenye muonekano wa kawaida lakini hatari sana: mtu asiye ‘fikiri’ (unakumbuka Socrates aliitwa ‘mtu hatari’ kwasababu alikufa akifikiri sana). Kila analoambiwa yeye anafanya bila kuuliza (wengine kila wanaloambiwa wao hupiga makofi na kushangilia bila kufikiri wala kuhoji). Ndiyo, kwa kipindi kile nchini Ujerumani, nchi ambayo ilikuwa na mfumo mbaya wa ubaguzi uliotungiwa sheria, ilikuwa ni rahisi sana kwa mtu kama Eichmann kujishawishi kwamba anayoyafanya ni sahihi kabisa. Mazingira yale yalimpa fursa ya mafinikio ya kazi yake: na akaichukua fursa ile ili mkono uende kinywani. ‘Suluhisho la mwisho’ la Hitler ilikuwa ni fursa kwake kumuonyesha kwamba anaweza kufanya kazi kwa weledi. Ni vigumu kuamini, na hata wakosoaji wa bi Hannah mwenyewe wanampinga pale Hannah anaposema kuwa bwana Eichmann alikuwa anatimiza wajibu wake (na hata yeye pia alijitetea hivyo).

Tofauti kubwa na wanazi wengine, aliyoyafanya Eichmann hayakuonekana kama yalitokana na chuki kwa wayahudi. Yeye hakuwa na sumu ya aina hiyo. Kipindi kile kulikuwa na wanazi wengi ambao walikuwa tayari kukupiga mpaka kufa mtaani kwa kosa la kutompa heshima ya ‘Heil Hitler!’ kwa kiogozi wao Adolf Hitler, lakini Eichmann hakuwa mmoja wao. Pamoja na yote hayo, bado alikubali kuwaa sehemu ya mstari wa mbele wa wanazi, na mbaya zaidi akakubali kutumika kuwasafirisha mamilioni kuelekea kuzimu. Hata alipokuwa akisikiliza ushahidi dhidi yake mahakamani, alionekana kuona kama alifanya mambo madogo tu ya kawaida. Yeye alichojali ni kwamba hakuwa amevunja sheria yoyote ya nchi yake wakati ule na yeye hajaua mtu moja kwa moja (kwa mkono wake au amri yake). Yeye alilelewa na kufundishwa kutii sheria na kufu uata amri za wakubwa, na hata watu wa karibu yake aliofanya nao kazi walikuwa hivyo. Kwake yeye kitendo cha kupokea amri siku zote, kulimfanya ajihisi kuepuka lawama ya matukio na madhila ya kazi yake ya kila siku.

Kwa Eichmann hakuona haja ya kuona mabando ya watu kwenye malori yakibeba watu walokufa au yeye mwenyewe kwenda kutembelea kambi za mauaji. Hakufanya hivyo. Huyu ni mtu aliyeiambia mahakama kuwa katika maisha yake aliogopa sana kuwa daktari kwasababu aliogopa kuona damu. Hata hivyo damu ilikuwa mikononi mwake. Alikuwa ni zao la mfumo ambao kwa kiasi uliomzuia kwa kiasi flani kufikiri kwa makini (thinking critically) kuhusu matendo yake na madhara ya matendo yake kwa watu wengine. Yaani ni kama hakujali hisia za watu wengine, bali yeye alichojali ni kutii amri na sheria tu. Na hata katika masiku yote ya kesi mahakamani, Aliendelea kusisitiza imani yake kwamba haoni hatia yoyote juu ya mashitaka yanayomkabili. Msimamo wake wa kusimamia hoja kwamba alichokuwa anakifanya ni kutii amri, ulimshawishi mwanafalsafa Hannah Arendt.

Hannah Arendt alitumia neno ‘the banality of evil’ kutokuwa na ufahamu juu uovu, kwa tafsiri isiyo rasmi, kuelezea alichokiona kwa Eichmann. Anasema kuwa Uovu wa Eichmann ulitokana na uovu wa kirasimu wa kiongozi mkuu na sio uwovu wa shetani mwenyewe. Huyu Eichmann alikuwa mtu wa kawaida tu aliyeruhusu mitazamo ya kinazi kuathiri kila alichokifanya. Falsafa ya mwana mama Hannah ilitokana na kuathiriwa na matukio yaliyomzunguka. Hakuwa moja ya wale wanafalsafa ambao wanatumia muda wao mwingi vijiweni (armchair thinking) wakifanya tafakuri ya mawazo dhahania au kujadili bila ukomo kuhusu maana sahihi ya maisha na dunia kwa ujumla. Falsafa yake ilitokana na historia za karibu na uzoefu wa maisha yake. Alichokiandika katika kitabu chake Eichmann in Jerusalem kilitokana na ushuhuda wake kwa mtu mwenyewe (Eichmann) na lugha aliyotumia pamoja na utetezi wake mahakamani. Alichokiona ilikuwa ni maelezo tosha ya uovu wa utawala wa kiimla na madhara yake kwa wale walioshindwa kuupinga chati za mawazo yake.

Eichmann, kama wanazi wengine katika zama hizo, alishindwa kuyaona mambo katika mtazamo wa watu wengine (watu wa namna hii wapo kibao). Hakuwa na ujasiri wa kutosha kuhoji sheria na amri alizopewa: bali alijitahidi tu kutafuta namna bora ya kuzitekeleza. Alikosa mawazo. Hannah anamuelezea kama mtu ‘boya’ na asiye na ubongo. Lau angekuwa nyang’au au zimwi kama watu walivyodhani, basi angekuwa anaogopesha. Lakini angalau mazwimi huonekana kwa nadra sana. Kilichokuwa kinaogopesha ni kwamba pale mahakamani, Eichmann alionekana mtu wa kawaida sana. Wa kawaida ndio, lakini mtu aliyeshindwa kutumia kipawa chake cha akili kuhoji mambo aliyoyafanya, na akawa mmoja kati ya watu waliotenda jinai kubwa kuwahi kutokea katika historia ya wanadamu. Inawezakana kuwa kama asingeishi kwenye zama za unazi, ni wazi kuwa asingekuwa mtu muovu.

Mazingira yalikuwa dhidi yake. Lakini hilo halimuondosheii hatia kwa sababu alikuwa mtiifu kwa amri zisizo za kimaadili (immoral oders-nitaeleza siku moja kuhusu falsafa hizi inshallah). Kwa mujibu wa Hannah, kitendo chake cha kuzitii amri za kinazi, ilikuwa sawa na kuipa nguvu “suluhisho la mwisho” ya bwana Hitler. Kwa kushindwa kwake kuhoji yale aliyoamrishwa, na kwa kutii amri hizo, maana yake alishiriki katika mauwaji ya halaiki hata kama kazi yake ilikuwa ni kupanga ratiba ya treni tu kwa mtazamo wake. Kuna muda aliwahi kusikika pale mahakamani akisema kuwa alitenda kufuata nadharia ya ‘wajibu wa maadili’(moral duty) ya mwanafalsafa Immanuel Kant-kana kwamba alichokifanya ni sawa kutii amri bila kuhoji. Alishindwa kabisa kuelewa kwamba Kant aliamini katika kulinda heshima na hadhi ya mwanadamu ndio msingi wa kimaadili. Karl Popper ni mmoja wa wasomi wakubwa wa Vienna walioponea chupu chupu mauwaji yaliyokuwa yakipangwa na ratiba za treni za Eichmann.

Hatimaye mnamo tarehe 15 Disemba 1961, kesi iliyovuta hisia za wengi nchini Israel na sehemu zingine za dunia ilifika ukingoni na mahakama ilimkuta na hatia bwana Eichmann na kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Japo alikata rufaa, lakini rufaa yake ilikataliwa na mnamo tarehe 1 Juni 1962 alinyongwa. Ndio, alinyongwa kwa kosa moja tu. Hakuwa jasiri wa kuhoji na kuuliza maswali kama Socrates wa ugiriki. Haku hoji kwasababu hakutumia vizuri kipawa chake cha akili kufikiri na kuchambua mambo. Alitii kila amri aliyoletewa mezani kwake (siku hiz zinaletwa kwa hati ya dharura), alipongeza kila alipomsikia bosi wake akiongea. Maskini Eichmann, alionewa huruma na mwanafalsafa mkubwa bi Hannah Arendt kwakuwa muathirika wa mfumo wa dola la kinazi, na sio kwa ujinga wa kutofikiri au kuhoji. Socrates na Eichmann, wote walikumbana na hatima ya aina moja-Kifo. Lakini tofauti kubwa ya vifo vyao ni mbili tu; moja Socrates alihukumiwa kifo kwasababu alipenda kuhoji, wakati Eichmann aliona kuhoji kuna punguza ufanisi na kuchelewesha kufikia malengo ya kazi yake. Lakin kubwa zaidi ni kwamba, historia inamkumbuka Socrates kwa heshima kubwa zaidi kuliko Eichmann.
77a33ab03e30aae5a607554fbe67a300.jpg
Kazi nzuri
 
2 Mambo ya Nyakati 1

1.Basi Suleimani, mwana wa Daudi ,alithibitishwa katika ufalme wake naye BWANA,Mungu wake ,alikuwa pamoja naye akamtukuza mno.

Maombi yangu leo,MUNGU akuthibitishe katika nafasi uliyonayo kama Suleimani mwana wa Daudi alivyothibitishwa na BWANA Mungu.Awe nawe katika kila hatua unayopita.Wanaokupiga vita katika ndoa,kazi,shule,biashara,maisha,ujirani,undugu ,wana okukandamiza kiroho,kimwili,kiakili WAKASHINDWE katika jina lipitalo majina yote Jina la Yesu Kristo Amen Asante...Kazi njema
Ameeen
 
Kabisa!!!!nina story ya uchungu iliwahi tokea tukiwa wadogo sikuelewa...kuna watu wangu wa karibu walifiwa na baba wakaachiwa mji,mama yao na wakwe wakabaki hapo ,mtoto wao mmoja siku moja alichukua mkaa akachora nyumba nzima....ilikua kesi nzito,mama akalaumiwa na kuambiwa amemfundisha mtoto,akatukanwa sana na kunyanganywa watoto na kufukuzwa hajui kulea

Nilipokua mtu mzima na Mungu kunijalia kupata watoto ,siku moja mwanangu wa chekechea alifundishwa shule kuandika jina,akajua kuandika na langu....aliporudi nyumbani alichora nyumba nzima jina langu na lake......ningemlaumu nani?

Nililia sana nikakumbuka yule mama alivyohukumiwa,nilitamani niwaelezee bahati mbaya wote hawapo
Pole sana
Watoto watundu ni balaa
Hata sisi tukiwa wadogo kuna mambo ya kipuuzi tulifanya maana "hatukuwa na akili ya kujua jema na baya"
Wapo waliovunja TV,vyombo n.k
Wengine walichana vyeti muhimu vya wana familia
Wengine waliharibu chakula n.k
Utoto bhana
.....
 
Mmmmh.... pesa inaboost boost mkuu japo nakubaliana na wewe kuwa kuvaa ukapendeza ni kipaji
Ndio pesa unaweza kumuajiri mtu wa kukuvalisha
Ila mtu kama mtu (ww km ww) kujua kupiga pamba ni kipaji au pengine hobby
Hivyo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya uvaaji wa mtu na pesa

Km huamini chunguza wenzako makazini,vyuoni,shule ni,mtaani au pengine wanafamilia
........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom