Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Kuelekea Furahi Day

Najua upo kwenye utayari wa kuitafuta siku nzuri kabisa katika wiki, Ijumaa. siku hii kama zilivyo siku za wikend imekuwa na siku ya kipekee maana ndo siku kwanza kabisa inayoashiria mwisho wa siku za kazi, na hapa unaruhusiwa kuburudika. Na kwa ukipekee kabisa siku hii inakuja tarehe nzuri, ukisikia siku imekuja tarehe nzuri usipeleke mawazo yako kiunoni, soma kalenda na utajua leo ni siku ya kupokea mshahara kwa walioajirwa na waajiri kutulipa madoers (watendakazi).

Makapuku ni nyumba ya wengi, mmoja akitoka mwingine anaingia yaani kama Fid Q. Asante kwa Jimena kustep in kwenye segment ya Leo katika Historia. Na kama kawaida segment zimebamba kuliko kubambiana kwenyewe, yaani zimekuwa mswano.

Kilichojiri leo, nimeona tena kuwasilishwa kwa miswada ya maliasili za Tanzania kwa hati ya dharula, yaani ni kama jana na juzi na kesho itafika tutapiga makofi tukiwapongeza serikali na bunge kwa kulinda maliasili zetu kama ilivyo kawaida yao. Wageni wanachukua minofu sisi tunabaki na mapanki, kwa kuwa tu mapanki ni mazuri kwa supu (hayana tofauti na makongoro), nani anapenda dhahabu wakati kuna magwangala na makinikia. Hongera bunge letu na serikali kwa hati hzi za dharula.

Muziki sasa, kuitafuta siku bora kabisa katika juma hebu tuangalie kolabo ya Defao na Suke Chile, hawa wote ni wakongo ila sema Suke Tshile (Suke Chile) aliweka makazi yake Zambia kwa muda mrefu sana. Walifanya nyimbo nyingi na hasa ukizingatia kuwa suke Chile ni DJ, yeah mchezesha muziki na alitaka muziki wake uwe unachezeka katika klabu zake za Chez Nthemba. Kwa wa Mwanza kulikuwa na bar moja maarufu mitaa ya Nyakato-Mecco/Nundu ikiitwa Chezi Nthemba, yaani kuna watu wanazijua bar kuliko nyumba za ibada, hongereni sana.

Mjomba wangu lee empire aliupenda sana wimbo huu na sababu ya kuupenda anaijua yeye maana zama hizi za makinikia na wahamiaji haramu sichelewi kujiharibia, si unajua nishaulamba najiandaa na safari ya kuja mjini.

Furahia goma hili pale unapoitafuta Ijumaa. nakupenda Kapuku mwenzangu na unalijua hilo.


Obe Asante kwa music
 
Aunt yangu, uko poa! Kuna nini utasema nisifanye, juzi ulinikataza nisilete zile ishu za teller sijui tailor nikatuliza maana sipendi kukuudhi. Ukisema chochote nakuwa mtekelezaji zaidi kuliko mtelekezaji

hili goma nitalipandisha ufurahie wewe pale utakapofuta kauli ya kutokwenda ile safari yetu
Safari ya kg ipo au imekufa
 
645c17721465550b9b6a50ae155d11d0.jpg
bd82afe17303aa224ab4d5582e00bc54.jpg
Wanamlisha maneno km Mugabe zamani
......
 
Safari ya kg ipo au imekufa


Mdau, yaani hata sijui kuna nini kinaendelea maana safari ilikuwa imeiva kabisa na nishaulamba kama unaenda kukutana na kiongozi wa dini, nimepiga mokasini four angle, shati la ng'aro nimechomekea na suruali ya mchelemchele. Ila naona Shunie kakasirishwa na mjombaangu lee empire kasema niende na siju wa tukuyu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom