Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Kuelekea Furahi Day

Najua upo kwenye utayari wa kuitafuta siku nzuri kabisa katika wiki, Ijumaa. siku hii kama zilivyo siku za wikend imekuwa na siku ya kipekee maana ndo siku kwanza kabisa inayoashiria mwisho wa siku za kazi, na hapa unaruhusiwa kuburudika. Na kwa ukipekee kabisa siku hii inakuja tarehe nzuri, ukisikia siku imekuja tarehe nzuri usipeleke mawazo yako kiunoni, soma kalenda na utajua leo ni siku ya kupokea mshahara kwa walioajirwa na waajiri kutulipa madoers (watendakazi).

Makapuku ni nyumba ya wengi, mmoja akitoka mwingine anaingia yaani kama Fid Q. Asante kwa Jimena kustep in kwenye segment ya Leo katika Historia. Na kama kawaida segment zimebamba kuliko kubambiana kwenyewe, yaani zimekuwa mswano.

Kilichojiri leo, nimeona tena kuwasilishwa kwa miswada ya maliasili za Tanzania kwa hati ya dharula, yaani ni kama jana na juzi na kesho itafika tutapiga makofi tukiwapongeza serikali na bunge kwa kulinda maliasili zetu kama ilivyo kawaida yao. Wageni wanachukua minofu sisi tunabaki na mapanki, kwa kuwa tu mapanki ni mazuri kwa supu (hayana tofauti na makongoro), nani anapenda dhahabu wakati kuna magwangala na makinikia. Hongera bunge letu na serikali kwa hati hzi za dharula.

Muziki sasa, kuitafuta siku bora kabisa katika juma hebu tuangalie kolabo ya Defao na Suke Chile, hawa wote ni wakongo ila sema Suke Tshile (Suke Chile) aliweka makazi yake Zambia kwa muda mrefu sana. Walifanya nyimbo nyingi na hasa ukizingatia kuwa suke Chile ni DJ, yeah mchezesha muziki na alitaka muziki wake uwe unachezeka katika klabu zake za Chez Nthemba. Kwa wa Mwanza kulikuwa na bar moja maarufu mitaa ya Nyakato-Mecco/Nundu ikiitwa Chezi Nthemba, yaani kuna watu wanazijua bar kuliko nyumba za ibada, hongereni sana.

Mjomba wangu lee empire aliupenda sana wimbo huu na sababu ya kuupenda anaijua yeye maana zama hizi za makinikia na wahamiaji haramu sichelewi kujiharibia, si unajua nishaulamba najiandaa na safari ya kuja mjini.

Furahia goma hili pale unapoitafuta Ijumaa. nakupenda Kapuku mwenzangu na unalijua hilo.

Enzi zake defao jamaan
Binamu asante pamoja kuwa umechunia text yangu ila kigamboni hatuendi
 
Aunt yangu, uko poa! Kuna nini utasema nisifanye, juzi ulinikataza nisilete zile ishu za teller sijui tailor nikatuliza maana sipendi kukuudhi. Ukisema chochote nakuwa mtekelezaji zaidi kuliko mtelekezaji

hili goma nitalipandisha ufurahie wewe pale utakapofuta kauli ya kutokwenda ile safari yetu
sitaki mie jamaan
 
Hayawiiiii hayawiiiiii yamekuwaaaaaa.....asantee bhinamu kesho si unajua bill yangu japo leo umenikwepa
 
Aunt yangu, uko poa! Kuna nini utasema nisifanye, juzi ulinikataza nisilete zile ishu za teller sijui tailor nikatuliza maana sipendi kukuudhi. Ukisema chochote nakuwa mtekelezaji zaidi kuliko mtelekezaji

hili goma nitalipandisha ufurahie wewe pale utakapofuta kauli ya kutokwenda ile safari yetu
Afute kwanzaa kaulii
 
Nakumbuka bhinamu na mm mambo yale nayasawazisha hope kesho tutakuwa na weekend mujarabuuu ....

Niko poa kiukweliiii

Kesho anko itakuwa poa sana , wewe jipange nami najipanga maana si unajua ile buku jero kwa mjumbe imezaa, yaani kaizalisha pale nilipoenda kumwambia umesafiri ikawa buku tatu nzima yaani ukijumlisha inakosekana jero tu kufika mkoba yaani buku tano.

Vipi utakuja na ugeni wetu wa Tukuyu😀😀
 
Bhinamuu mbona wewe mara nyingi una tabia ya kusahau lakini buku jero huachi ...najua kasheria ni msumeno na tulijiwekeaa sisi ikilala inazaaa ....yaaa ikilala kweliii ....lakini ukumbukee ile siku nimelewaa kwenye mfuko kulikuwa na buku 2 na wewe ndo uliichukua ila ukachukua advantage kuwa nimelewa ntasahau ..unaikumbuka???

Kesho nafanya suprises ..
 
na wewe huwa husahau hata mambo madogo bhana! zile nilizitunza maana namna mlivyoondoka na cm nikajua tu hapa ungeondoka na wallet ungempa hela ya supu nikaona bora ukale bure. Sasa msala ukabaki kwangu, chapati zililala ikabidi mama Ashura adai nizilipie maana nilimpa gundu tulipoamka.

Okay , kama ni hivyo basi tufanye tunatoa hiyo buku mbili, zinabaki buku tatu, kama vipi tuombe assist kabisa mapema
 
Samahani bhinamu acha mzaha kwenye mambo ya msingi yanayohusu pesa ...na mm nakutega tu japo hutegekiii unaikumbuka vyema sheria yetu ibara ndogo inayohusu mikopo hasa kwenye riba ....

Kipengele cha 4 ibara ndogo baa nakopiii "hairuhusiwii kulipa deni kama anayedai anadaiwa " na kama unakumbuka hii sheria ilimfanya mama chausiku atoke kwenye umoja wetu ...

Kwa sheria hiyo deni lako halizaii kwa kipengele cha 5 kinachofuataa....niko makiniiii

Nafikiri kwa kile cha sita unajua natakiwa nilipwee sh ngapiii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom