Makapuku Forum

Ajira hugeuka kuwa utumwa pale ambapo baada ya kuipata hutaki kufikiria tena nje ya box hapo ni shida ila Ajira unaweza kuitumia kama Stepping stone na ikakuvusha ng'ambo ya pili pale ndoto yako ilipo..
Kumbuka braza mara zote huwa ngumu sana kuchomoka kutoka kwenye utumwa, pesa huwa haitoshi kwa kadri ya siku zinavyozidi kwenda. Ingelikuwa ni hivyo ni watu wengi sana wangelikuwa wameshaacha kazi ili wajiajiri maana kuna idadi kubwa ya wahanga wa ajira wanaotamani kuacha kazi za utumwa wapate kujiajiri.
 
Umeongea kweli tupu mkuu si rahisi kama tunavyoandika hapa...Lakin unajua kuna watu wengine huwa ni waoga kuthubutu akipata kazi mahali anachoangalia ni jinsi gani atadumu pale milele lakin mkikaa naye vijiwen na yeye ana-act kama vile anatafuta alternative ya kuondoka pale kumbe ni zuga tu.
 
Ndiyo maana siku zote nasema kuajiliwa ni utumwa.

Mfano unapata mshahara laki 5
Makato kibao.
Unalipa kodi ya nyumba.
Unasomesha
Unanunua mahitaji ya nyumbani
Unataka kujenga.
Watoto wataumwa.
Utahudumia ndugu.
Utanunua nguo na vitu vingine vya luxury.
Usafiri.
Utataka umiliki shamba.
Na mambo mengine kibao huo mshahara utatosha nini kama si kufa masikini.?
 
Wengi huwa hawachomoki, na wafanyakazi walio wengi huwa wanashindwa kuitumia fursa ya mshahala kama kipato kwa kuanzishia mtaji. Wanaishia kupanga nyumba za bei ya juu, gharama za maisha kupanda maana wanahitaji kuwa na maisha mazuri.
 
Ni kweli usipojiongeza hutoboi kabisa ndugu yangu...
 
Wengi huwa hawachomoki, na wafanyakazi walio wengi huwa wanashindwa kuitumia fursa ya mshahala kama kipato kwa kuanzishia mtaji. Wanaishia kupanga nyumba za bei ya juu, gharama za maisha kupanda maana wanahitaji kuwa na maisha mazuri.
Ni changamoto kubwa sana na wengine wanashindwa kutoka kwenye hzo ajira maana amechukua mkopo atakaoulipa miaka 5 then pesa yote hiyo ya mkopo kanunulia gari tena la kwendea kazin na jion kupaki Bar...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…