Makapuku Forum

Hahahahaha huyu kweli amestahili kuwa wa kwanza. Yani anapiga assist hadi kwenye mabenki!!
Asante Bitoz kwa kumi kubwa
 
Shukrani
 
Acha bhana mbona wamesema wewe ndo utailetaa .....na kama umeipokeaa husiifungueee nakuombaa


...haiko kwenye bahasha yaani iko wazi unaona kila kitu. tangu lini summons ikawekwa kwenye bahasha. Unahitajika kwa mwenyekiti ukaelezee ule muziki uliofunga juzi uliutoa wapi! Na yule dj sasa ndo balaa yaani kakeshesha watu bila kupenda.
 
...haiko kwenye bahasha yaani iko wazi unaona kila kitu. tangu lini summons ikawekwa kwenye bahasha. Unahitajika kwa mwenyekiti ukaelezee ule muziki uliofunga juzi uliutoa wapi! Na yule dj sasa ndo balaa yaani kakeshesha watu bila kupenda.
Ya mziki tena hawa watu wananitakia nini jamaan bhinamu wangu ..

Na mm nilimwambia sawa nimekuletea mziki system ila nkamuomba apige kwenye mono sauti ya chini ona sasa apa yataibuka mengine ....hivi bhinamu umeshindwa kuwambia nimesafiri ??
 
Muziki: Kumekuchwa

Hivi unajua kuwa Makapuku Forum kuwa sehemu inayohusudiwa na kila mwana JF ni kwa sababu ya wewe kapuku unayesoma segment hii ya Muziki na Utamu wa gitaa. Ndiyo, wewe ni mtu bora sana na Makapuku Forum ni sehemu bora kabisa kwa sababu wewe, naam, wewe unayesoma bila kupepesa macho ni sehemu ya Makapuku forum. Hata mimi, kama ulivyo wewe ni muhimu humu, kifupi Makapuku wote tunaifanya forum hii kuwa bora kabisa. Yaani tumeifanya KF kuwa kama Geneva ya JF, kimbilio la kila mmoja, a buffer zone, shokomzoba (shock absorber). Utataka nini ukose huku, siasa, jamimi, maisha, elimu, utani, imani zote utazikuta.

Utakutana na viungo wa hatari wanaotoa assist na kama kawaida ma mastrika wa hatari ambao hatutoi assist kwenye kumi nane. Njoo ukabe utupe penati.

Kuanzia siku inapoanza tunapokutana na wewe mpenzi msomaji, ukiianza siku kwa maombezi, UF, then segment ninayoipenda sana, magazeti, halafu unakutana historia, hadithi halafu mchana tunakutana kwenye kipenzi cha wote, sogozi, jioni tunakuwa kwenye zile mambo nzuri kabisa za 10 kubwa na bora. Sijui kama kuna segment nimeisahau maana kabla ya kulala tunakutana kwenye muziki na mada rahisi. seriously, KF ni nzuri kwa sababu mimi na wewe tupo hapa.

BTW, wataalamu wa umeme wamekuja kwa hiyo wakati tukiendelea kufaidika na umeme wa gesi nchi nzima basi tusubiri umeme wa maji kule nini nini Gorge sijui.

Muziki sasa, anaitwa Ringo Mandlingozi, huyu kama ilivyokuwa jana (sitafanya kukosea tena kwa kuweka muziki tofauti na maelezo ) anatoka SA na ni mwimbaji na muandaaji wa muziki mwenye tuzo kibao kuanzia Kora hadi tuzo za ndani. Umaarufu wa Miriam Makeba uliwezeshwa kwa muziki mzuri wa huyu jamaa.

Ana sauti nzuri inayoshibisha masikio na muziki wake ndio utakaokuburudisha usiku huu. Hivi unajua nini? Wewe ni mtu muhimu humu na ninajiskia poa sana unapochukua muda wako adhimu kutembelea jukwaa hili. LLL

 
Ya mziki tena hawa watu wananitakia nini jamaan bhinamu wangu ..

Na mm nilimwambia sawa nimekuletea mziki system ila nkamuomba apige kwenye mono sauti ya chini ona sasa apa yataibuka mengine ....hivi bhinamu umeshindwa kuwambia nimesafiri ??


...ila mimi huyu mwenyekiti huwa ananishangaza, yaani hakosi visingizio. Ningemwambia umesafiri unajua ambacho angekifanya, vipi angeibuka kwa teller? si angechoma nguru mtaa mzima ujue.

Mimi nikaipokea ila nikampoza na buku jero, so jua kabisa unadaiwa, deni likikaa wiki naanza kuweka riba kama vicoba
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…