EBENEZA YUPO ANATUSAIDIA
1 SAMWEL 7
11.Nao watu wa Israel wakatoka Mispa ,wakawafuatia Wafilisti,wakawapiga hata walipofika chini ya Beth-kari.
12.Ndipo Samweli akatwaa jiwe ,na kulisimisha kati ya Mispa na Sheni,akaliita jina lake Eben-ezeri ,akasema ,Hata sasa BWANA ametusaidia.
TUOMBE
MUNGU BABA wa mbinguni tunakushukuru kutuamsha salama ,asante tumekuona unatuponya,unatubariki,unatulinda,unatukinga na unatupa furaha BABA tunakuona unatupa Amani Asante kwa kuwa upo nasi kila siku unatusaidia wewe ni EBENEZA.
Tunaomba tutakase,wasaidie vijana wote wakujue,wasaidie wanaotafuta ada,kodi,nyumba na maendeleo mbalimbali.
Ponya wagonjwa, wape tumaini wafiwa,wajane yatima,na wasio na makazi.
Tutakase BABA ILI TUPITE KWENYE CHANGAMOTO MBALIMBALI SALAMA.
Saidia nchi yetu Tanzania sawasawa na mapenzi yako,wafanye viongozi wetu wawe na hofu yako na watende haki siku zote,iponye nchi yetu Tanzania BABA na maafa mbalimbali epusha mauaji yanayoendelea,wewe ndiye unajua siri ya yote na utatoa hukumu ya haki
Baba asante tunashukuru
Katika jina la Yesu Kristo Amen
SIKU NJEMA MBARIKIWE