Makapuku Forum

1976 - Patrick Vieira anazaliwa.

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa.

Alikuwepo katika kizazi cha dhahabu cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1998 katika ardhi ya nyumbani.

Klabuni Arsenal anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa sana katika eneo la kiungo cha kukaba.
 
Leo Katika Historia:

1887 - Banff National Park yaanzishwa huko Canada.

Ni moja kati ya hifadhi kongwe zaidi Duniani.

Ina ukubwa wa Kilometa za mraba 6641
Mchakato rasmi ilianza mwaka 1885......linapatikana kwenye safu za milima ya Rocky Mountains
Inaparikana katika umbali wa Km 110--180 Magharibi mwa Calgary katika jimbo la Alberta
.........
 
1972 - Watergate Scandal: Rais wa Marekani Richard Nixon na Mnadhimu Mkuu wa Ikulu ya Whiye House wanarekodiwa mipango yao ya kutaka kutumia CIA kuharibu upelelezi uliofanywa na FBI kuhusiana na Skendo hiyo nzito kuwahi kutikisa Marekani.
Ikumbukwe alikuwa ameshajiuzulu Juni 17 baada ya skendo kuwa kaa la moto...siyo huku kwetu Andrew Change ana skendo zaidi ya 10 lakini ni mwenyekiti wa bunge anadunda tu ....Daudi Bashite naye ni balaa Zipo filamu kibao zimechezwa ili tu kuakisi tukio hilo na mambo ya nyuma ya pazia
......
 
2016 - Uingereza yapiga kura ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya ( EU ).
Na kura zikatosha
Waingereza ni miongoni mwa watu wanaojisikia sana wanadai umoja huo hauna manufaa kwao(inawezekana ni kweli) ila ni wajivumi hata katika soka wanajiona wao ni zaidi ya FIFA na kung'olewa kwa Blatter kuna mkono wao na Wamarekani nyuma ya pazia
.......
 
1945 - John Garang anazaliwa.

Alikuwa ni Rais wa Sudan ya Kusini.

Alifariki kwenye ajali ya Helikopta.
Mdau Garang hajawahi kuwa Rais wa Sudan Kusini bali tu mwasisi wa Taifa hilo hadi wakati anafariki Sudan Kusini haikuwa nchi/bado haikupata Uhuru....kawahi tu kuwa sijui Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Sudan ya Omar Bashir Huyu jamaa mvuta bangi ambaye huko ni Waziri ni mwanawe
Jamaa ni mchafumchafu na Vituko kibao ila ana IQ kubwa fuatilieni interview zake
......
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…