Makapuku Forum

Makapuku Forum

Huyu ndiye watu humuita samaki mtu
Anajulikana kwa jina mermaid

Uhakika kama yupo au hayupo sijui

lakini huishi ndani y'a maji
Mara chache hujitokeza juu ili kuota jua au kupunga upepo

Kama unajua zaidi kuhusu mermaid tafadhali tuambie

Kwanza wapo kweli au ni matengenezo y'a watu
cc9b61eded2f0404b5fa7a036229dbc2.jpg
458ce168f6057899480711b2561c1927.jpg
1198b93eea8fed5dd2ddfc3cb1a687c6.jpg
c41980412b2067d29960b02d03ea8e7f.jpg
466084a42c7317904d3bbfb54a3684a3.jpg
Movie gan kiongozi
 
Huyu ndiye watu humuita samaki mtu
Anajulikana kwa jina mermaid

Uhakika kama yupo au hayupo sijui

lakini huishi ndani y'a maji
Mara chache hujitokeza juu ili kuota jua au kupunga upepo

Kama unajua zaidi kuhusu mermaid tafadhali tuambie

Kwanza wapo kweli au ni matengenezo y'a watu
cc9b61eded2f0404b5fa7a036229dbc2.jpg
458ce168f6057899480711b2561c1927.jpg
1198b93eea8fed5dd2ddfc3cb1a687c6.jpg
c41980412b2067d29960b02d03ea8e7f.jpg
466084a42c7317904d3bbfb54a3684a3.jpg
Mbona sijamuona mermaidi mweusi katika picha zako??
 
Asante Madenge ...ebhu twende sawa kiduchuuu kuhusu nyoka

MFAHAMU NYOKA MPOLE (KIBISA) NA
NYOKA MKALI (KOBOKO).

Kimsingi nyoka ni viumbe ambao wamepewa jina la jumla yaani nyoka, lakini viumbe hawa wapo wa aina mbalimbali na wa majina tofauti tofauti, wapo nyoka wazuri, wapole, wakali, wanaotisha nk, kwa leo nataka niwazungumzie nyoka wawili maarufu wa kwanza ni Kibisa na wa pili ni Koboko (Black Mamba), kimuonekano viumbe hawa wote wana rangi nzuri na za kuvutia, tofauti yao ni moja tuu wakati mmoja msatarabu mwingine ni mtata balaa na ninaposema mtata elewa mtata kweli, mwenye hasira na mkatili.
Nyoka katika makazi wamegawika sehemu mbili, wapo ambao huishi sehemu ambazo wanadamu wanafanya shughuli zao, hawa si wakali sana na sifa yao ni kwamba wanapomuona binadamu hukimbia na ukiona amekugonga ni ama umemkamkanyaga au umemshitua alipojificha na akahisi hatari, hivyo nyoka ambao huchangamana na binadamu hata wanaouma huwa si wakali.
Nyoka wa aina nyingine ni wale ambao hawataki kabisa kuchangamana na binadamu, na hata katika makazi yao binadamu wakianza kuonekana onekana nyoka hao huachana na makazi hayo, ogopa sana kukutana na nyoka wa aina hii hawa huwa hawaogopi mtu kwanza wengi wao wana mbio, pili ni wakali sana na tatu yeye akikuona binadamu ndio kwanza hakimbii bali atakukimbiza, kundi hili ndio hata Koboko anapatikana, nyoka hawa mbali ya ukorofi lakini wanaogopwa sana, mfano kuna nyoka anaitwa *SAWAKA*hata Tembo akimuona anakimbia utakuwa wewe!?
Asilimia kubwa ya nyoka wanaoweza kuchangamana na binadamu huuma tuu, lakini hawa wengine wapo ambao huuma na wapo ambao hurusha mate kama kinga, na wapo ambao humeza kabisa kama *boss Chatu*.
Kwa utangulizi huo turudi sasa katika mjadala wetu !
Kibisa
Kibisa ni nyoka ambao wamejizolea umaarufu mkubwa sana, kwa kuwa jina lao hutumiwa pia kuwaita wanaume ambao huwa na aibu kuwaeleza wanawake hisia zao kimapenzi, na kwa nini waitwe Kibisa ? Jibu ni moja tuu,nyoka huyu haumi hata umfanye nini , ni nyoka asiye na madhara kabisa, mpole, mzuri na anaishi katika sehemu ambazo binadamu hufanya shughuli zake kama kilimo nk.
Unaposikia Kibisa usije fikiri ni nyoka wa aina flani ! kama alivyo Chatu, Cobra nk, hapana nyoka hawa wapo wa aina mbalimbali na wa tofauti, wataalamu wa sayansi huweza kuwa ainisha kwa majina yao, wapo wa kijani, wapo wa njano na weusi weusi kidogo, wapo wa rangi ya ugoro nk, kifupi ni wapole na wana sura ya kuvutia sana na rangi zao huwafanya wapendeze zaidi.
Kama ilivyo kwa nyoka wengine Kibisa hula nyama hutumia wadudu wadogo wadogo kama chakula, kutokana na upole wake muda mwingi hutumia kujificha ili asionekane na maadui.
SIFA ZAKE
1. Huwa haonekani hovyo.
2. Unaweza ukaishi naye ndani kwako kwa muda na usijue yupo, ili mradi tuu uwe na mende, mijusi wadogo, panya, nk.
3.Haumi wala harushi mate.
4.Hupendelea kujifukia chini.
5. Pamoja kwamba haumi, mkwara wake ni hatari sana, ukikutana naye ili usimdhuru haraka sana hukimbilia mwilini mwako na hujiviriga katika mguu wako kisha anatulia, kama utampiga muumie wote! (Kama nakuona ndio kajifunga mguuni kwako unavyo utupatupa huo mguu) na wale mnaopendelea kuvaa pensi au sketi harahara akiona nafasi ndio atazidi kupanda juu, sasa sijui itakuwaje akifika mwisho huko ! Sipo.....!

KWA UCHACHE HUO TUMTIZAME KIDOGO NA KOBOKO.
Koboko ni nyoka mkali sana na ninaposema mkali uelewe ukali wenyewe, nyoka huyu huanza ukatili tangu anapotoka katika yai tuu, huweza kujitegemea na kupambana kuanzia hapo tuu, kiwango cha sumu anachokuwa nacho anapotoka kwenye yai ndio hicho hicho ambacho huwa nacho mama yake, hivyo chunga sana usije ukakadharau kwakuwa eti kadogo utaumia! Wakati nyoka wengine wakiuma na meno yao wakiacha walipouma hadithi hiyo haipo kwa Koboko, yeye akiuma meno yake bado huwa mali yake!
Akikuuma nyoka huyu huwezi kumaliza dakika 30, sumu yake husambaa haraka na huaribu mfumo mzima wa mwili sambamba na moyo.
Koboko ana rangi nzuri sana cha ajabu mdomo wake ndani ni mweusi tii wakati viumbe wengine ndani huwa wekundu, ndio nyoka mwenye mbio sana huwezi mshinda akikutaka hata uwe na baiskeli! Mbali na kutomshinda lakini hata ukitaka kumpiga pia sahau,huwezi kabisa anajua sana kukwepa, akikukimbiza akakufikia atakaa mbele yako na atasimama mbele yako kwa urefu wa kimo chako huku akikenua meno ambayo huwa na matone ya maji maji na hiyo ndio sumu yake !
Ana speed ya kila kitu unapokuwa katika hali kama hiyo usithubutu kutaka kupambana naye, kabla hujafanya unachotaka atakuwa tayari amekuadhibu kwani yupo shapu sana na ni mwerevu pia na endapo utatia huruma sana ukadondosha na chozi Koboko anaweza kukusamehe uende zako, kumbuka hii ni ikiwa hujamsumbua kabisa yaani umeshituka tuu huyu hapa!
Watu wengi hudhani nyoka huyu ana mabawa lakini ukweli ni kwamba anaweza kuruka kama warukavyo ndege lakini mwili wake ni kama nyoka wengine tuu, safari yake ya kuruka huianza awapo juu ya mti na kuruka kwake huwa si kwa umbali mrefu sana na ukiona kaanza michezo hiyo ujue kuna shambulio anataka kulifanya karibuni, au anawakimbia ndege waliomshitukia akifanya uharibifu katika viota vyao.
Nyoka huyu kama walivyo nyoka wengine naye ana sifa zake, pia ana wababe wake, pia ana namna ya kukabiliana naye ikiwa ni pamoja na namna ya kumuepuka.
Ila la mwisho nawaza tuu, huyu jamaa huwa mkali na mkorofi sana ukimpigia kelele, unapokuwa msituni ukipiga mluzi tuu unamkera, sasa najiuliza kwa kelele kama zile za Kariakoo ukiwatupa kumi tuu sijui itakuwaje?
Nadhani ndani ya saa moja patakuwa kimyaa utafikiri ni usiku kwani watu wote watakuwa wamelala.
Na bendera yaweza kupepea nusu mlingoti labda miezi sita hivi.
Aisee nimeogopaaajeer nitamalizia kesho kusoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom