Makapuku Forum

Hahahaha
 
Duh amekula chumvi ya kutosha!
 
4/Juana Chox Yac
Alizaliwa Novemba 29 1893 nchini Guatemala
Amewahi kushikilia rekodi ya dunia ya mtu mzee zaidi duniani hadi mauti yalipomfika
Alipatiwa kitambulisho cha Taifa mwaka 2012 baada ya vielelezo kujitosheleza bila chenga kwamba kazaliwa karne ya 19
Ameacha vitu kuu kibao
Alikuwa na umri wa miaka 122 wakati anafariki dunia 2015
.......
 
3/Jeanne Calment Alizaliwa Februari 21 mwaka 1875
Ni bibi wa Kifaransa mpuliza fegi
Alikuwa anajishughulisha zaidi na kilimo
Alianza kufahamika pindi alipofikisha miaka 113 na kuwa maarufu dunia nzima...nafikiri ndiye Mfarabsa mzee zaidi kuwahi mutokea
Alifariki mwaka 1996 mwezi Agosti akiwa na umri wa miaka 122 na siku 164
......
 
2/Tuti Yusupova
Alizaliwa kati ya mwaka 1880 au 1882
Alikuwa ni bibi wa Uzbekistan.....wakati anazaliwa nchi hiyo ilikuwa sehemu ya Urusi sijui koloni lao kiufupi inachanganya
Akishikilia rekodi ya mtu mzee zaidi duniani hadi pale alipofariki
Alifariki dunia mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 134 na siku 270
........
 
Daaaaaah kweli chumvi kailaa
 
hawakujii bhinamu vile vyanga vyako amaiziiiing ....ulikuwa unatishaa

Sema ulikuwa unanogaa ukisikia kisauti cha Jesca wa primary 'usiniumizieeeee'

Utaniambiaa alienda wap


Ha ahhahahaha, mjomba unakumbukumbu sana, inafaa uwe mkutubi hakyanani. Jesca (sio yule wa udom) yupo sema anajiita Jessicar kujitofautisha na mtoto wa pale panaponuka shombo feri.

Unakumbuka that day tuna mechi na wale jamaa wa polisi Kota , wao wana jezi sisi kifua game?

Ile nimetanguliziwa krosi naikimbilia nasikia "usiniumizie"""" basi midadi ikaniongezea mbio .

Kitahamaki nasikia kifua kinabana bana, watu makelele obe obe obe obe huku wanacheka , nikajua wamefurahishwa na mbio zangu, kama Lunyamila.

Lahaula kujicheki kumbe VIP yangu ilikatika ikapanda juu ikatulia kifuani kama sidiria.
Mjomba hii story usiilete tena hapa, ilinitia haya sana
 
1/Dhaqabo Ebba
Ni Muethipia alizaliwa miaka ya 1850's
Muda wake mwingi anejishughulisha na kilimo
Sijaona mahali popote kama huyu babu keshafariki(sina uhakika)
Kinachomnyima tunzo ya kuwa mtu mzee zaidi duniani ni ukosevu wa ushahidi kamili pia Wazungu hujipendelea tu kwa kila jambo
Ana umri wa zaidi ya miaka 160
.
.
.
.
.
Shukrani kwa mliosapoti mada
Tukutane kesho
Mwisho
.............
 
Duh
Asante Bitoz kwa top 10
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…