Makapuku Forum

Maneno kuntu
 


Asante sana mdau Shimba, kuandika ni 'hobby' na ninafurahi na kujiskia vizuri kuwa sehemu ya familia hii, Makapuku ambako kumejaa member wanaojitambua na kujali masiha yao na ya wengine bila kukereka wala kukereketwa.
Nikiingia humu huwa najifunza mengi sana tena ya msingi na yananifanya niwe na wakati mzuri nikaa kusaka mkate wangu na wa wapwa zako.

Hapo nilipopabold, ndo wanapokosea, ni kweli wapo watoto wa shule humu, JF ni kama kokoro... na unajua kokoro linaleta si samaki tu. Humu makapuku kuna watu wa fani zote na mada humu huwa zinaongelewa japo kiurahisi rahisi lakini ndo zinaeleweka vizuri sana.

Nikupe mfano mdogo tu, enzi hizo gazeti la Daily News lilikuwa linaandikwa kwa kiingereza kigumu hadi unajiuliza hawa waandishi ni maAnglo Saxon ama vipi? Yalipokuja mengine kama The Express, Guardian na mengine nikaona kumbe huna haja sana ya kuandika mabombastic ili uonekane unajenga hoja.

Hoja ni hoja pale inapoeleweka, na hili ndilo linalofanywa na Makapuku
 
Jambo lingine la kujifunza kule China
Ni kwamba serikali yao hawataki pesa yao iwe na thamani kubwa ili tu kuvutia kibiashara yaani export trade ndiyo maana wametawala soko la dunia

Chukua mfano dola ya Marekani ina thamani kubwa sasa mbongo ukanunue TV huko kwa SHIMBA dola 500 sijui ikija huku Bongo utamuuzia Nyagei Tsh ngapi

.........
 
Karibu Koromije mkuu. Huku TV ni laki tatu tu unapata. Unachosema hata hivyo ni kweli. Ndiyo maana Marekani huwa wanamlaumu sana Mchina kuwa huwa anafanya currency manipulation - mbinu za makusudi ili kuifanya pesa yake ibakie chini ikilinganishwa na dola hata kama uchumi wake unakua kwa kasi. Vita vya wakubwa!
 
Ukiunganisha nguvu na SHIMBA YA BUYENZE mtafanikiwa kumrudisha Shedebe na hadithi yake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…