Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa

Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa

Uko sahihi mkuu, YESU alisema kesheni mkiomba. Halafu huyo mpinga KRISTO anakataza!!!! Ashindwe kwa jina la YESU aliye hai
ni kweli alituasa tukeshe tukiomba na alitufundisha namna gani tuombe,Yesu mwenyewe alikua anasali usiku kwa unyenyekevu kiasi kwamba hakusumbua wanafunzi wake wakiwa wamelala,nyie hiyo style ya kuomba na masebene mpaka unakosa kupatana na jirani/nduguo ambaye uliaswa upatane nae kabla hujamtolea(hujaingia kwenye ibada) Mungu sadaka mmeitoa wapi?
 
Devil worshippers ni wale wanajidai kukesha huku wanaimba kwa nguvu na na kelele nyingi ili wasikike ,kama mafarisayo ,kumuabudu mungu sio mpaka ufunge vipaza sauti ...unaweza kuingia ndan ya chumba cha siri umuombe Mungu wako naye atakujazi...kipindi vha yesu watu kama hao aliwapinga ,wanao kaa njii za makutano wakisali kwa nguvu ili wasikike

mndorwe;
Kweli Mungu aliumba. Mtu upo gizani tena giza nene unasema usoyajua? Devil worshipers kwako ni hao wanaomwita Mungu wako? Ama kweli, kwa nini tupungukiwe kiasi hiki? Huyo Mkuu wa mkoa aliyeamua kufa na makanisa ni kwa sababu watu wa makanisa si wasemaji sana au? Mbona tuna misikiti inayo kesha usiku kucha kama hao walokole? Hao hawapo Arusha? Mbona misikiti kila siku wanatushtua saa 10 za usiku na hata wengine wanatuambia kuwa tuzione hizi shuka zetu kama sanda na vitanda vyetu kama machela?? Hayo ni maneno ya kumwambia mtu uliyechoshwa na maisha haya??
Jamani, sijali; Wafunge, wabomoe hata wayachome moto makanisa lakini HAKI TU ITENDEKE. Hakuna dini ilo bora zaidi ya nyengine.
Amepofuka macho kiasi cha kutoona mabaa yaliyofurika kila kona Arusha na G house!! Ama kweli, sikio la kufa halina dawa. Utawala dhalim ukiisha kuwagandamiza watu wake ukamaliza na kuwaacha hoi, kifuatacho ni kuingilia imani zao.
 
Wiki mbili zilizopita niliona mkuu wetu wa arusha aliweka namba zake za simu kwenye gazeti. Tulimwandikia msg kuwa karibu na kanisa moja la kilokole alibakwa mama mmoja. Alipiga kelele lakini kelele iliambatana na za walokole wanaoomba na kulia. Wenyeji wa maeneo hayo walidhani ni walokole wanaolia kanisani hapo tu
 
Huyo Mkuu wa mkoa kakurupuka. Hii ngoma serikali waicheze vizuri vinginevyo itawagharimu. Kumbuka waombaji ndoo wanaoiombea nchi hii kuliko Hayo ma night club yao.
 
Kwa hapa nilipo kero kubwa hawa wa alfajiri,kwa kweli wameshanizoesha kila ukifika muda huo lazima niwe macho mpaka jua linachomoza.

Nimejijengea kautaratibu kila ikifika muda ule wakanishtua basi nafungulia radio
Binafsi naishi jirani na msikiti, kanisa la Pentekoste pamoja na ukumbi unaotumika kwa maharusi, muziki wa dance na taarabu pamoja na disco! But trust me; tukiweka itikadi za dini pembeni halafu ukaulizwa upo tayari kuishi karibu na nini kati ya hivyo nilivyokutajia; basi kama tatizo lako wewe ni kelele basi kuishi jirani na kanisa iwe ni last option! Adhana msikitini kwa mfano, inayowasumbua watu ni ile ya alfajir ambayo hata hivyo ina-last for few minutes! Na kwa mahali kama Dar penye shida ya usafiri; ile adhana inawakera wale wanaobaki home lakini watu wa michakato wengi wanakuwa wameshaamka!

Ukija ukumbi-- mosi ukeshaji wa ukumbi wa muziki ni tofauti na kanisani! Kanisani ukiambiwa wanakesha basi ni wanakesha kweli! Hapo hujataja siku za JPili ambazo mchana kutwa mwendo mdundo mambo ambayo huwezi kukuta kwenye kumbi za muziki!
 
Kudhibiti makanisa ni kumdhibiti YESU KRISTO!!! Washindwe na walegee........
 
nimeelewa point yako lakini usijenge hoja kwa kutunga hadithi.Labda tutajie hilo eneo ambalo lina mambo yote hayo kwa uuwiano huo tuthibitishe.Nijuavyo mimi,unapoenda kuomba kibali cha eneo uweke msikiti au kanisa basi huwa au ukumbi wa kwa ajili ya dance na maharusi basi lazima wahusika wafanye tathmini ya eneo husika na hii ni pamoja na kuangalia ujirani wa misikiti na makanisa ili kuzuia muingiliano.
Cha msingi wakiamua kuzuia hizi kelele wapige marufuku kabisa vipaza sauti,iwe asubuhi,mchana au hata usiku.
 
Nakumbuka niliwahi kuleta mada kuhusu nyumba za ibada kufungu vipaza sauti na kusababisha kero kwa wakazi wanaoishi jirani na nyumba hizo na wengi tulitaka vipaza sauti hivi vidhibitiwe kuondoa kero ya kelele

Leo gazeti la Uhuru linaongozwa na habari inayosomeka: "Makanisa ya Kilokole kudhibitiwa mitaani",ni kwa kuimba wakati wa usiku.Hili ni tamko la Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Tunaishauri serikali zoezi hili liwe kwa nchi nzima na liisiishie kwenye Makanisa tu bali hata Misikiti ambayo nayo inayofunga vipaza sauti kwa nje na kusabisha kero ya kelele kwa wanaoishi jirani na Misikiti hiyo wakati wa ibada.

20160408_043802.jpg

Wafungiwe kabisa. Wasitumie dini kuwakwaza wengine. Kwanza kupayuka si kusali
 
Devil worshippers ni wale wanajidai kukesha huku wanaimba kwa nguvu na na kelele nyingi ili wasikike ,kama mafarisayo ,kumuabudu mungu sio mpaka ufunge vipaza sauti ...unaweza kuingia ndan ya chumba cha siri umuombe Mungu wako naye atakujazi...kipindi vha yesu watu kama hao aliwapinga ,wanao kaa njii za makutano wakisali kwa nguvu ili wasikike
Kesheni muomba maana hamuijui siku wala saa atakapokuja mwana wa adamu.
 
Wapi imeandikwa watu wa sali kwa makelele bila kujali wagonjwa,watoto wadogo na watu wengine wanaothirika na kelele hizo?
Zaburi 66:1-2 "Mpigie Mungu kelele za shangwe nchi yote, imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake............." Zaburi 47:1-2 Enyo wote wote pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe, kwa kuwa Bwana aliye juu, mwenye kuogofya, ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
 
Wote mnatakiwa muokoke na muwe wafuasi wa Yesu, kumkataa Yesu ni kumkataa Mungu aliyemtuma yesu ili akuokoe. Yani ni hivyo tu.
Mimi mwenyewe mkristo lakini ukweli ni kwamba Yesu alikuwa asali kwa kupiga makelele wala kupayuka tena hakuwa mnafiki.
 
Mimi mwenyewe mkristo lakini ukweli ni kwamba Yesu alikuwa asali kwa kupiga makelele wala kupayuka tena hakuwa mnafiki.
Kutoelewa kwako kusiwe sheria ya wote. Unampinga YESU KRISTO halafu unajiona mjanja
 
Back
Top Bottom