We jamaa Unachekesha sana na cjui unazungumzia Tanzania ya sayari ipi! Hivi mahali kama Dar es salaam hicho unachoongea kina - apply? Hivi hufahamu kwamba Dar es salaam makanisa, misikiti na hadi kumbi zipo kwenye residential area? Yaani unacho sema ni kwamba endapo spot X kuna msikiti basi Wakristo hawatajenga kanisa spot Y simply because spot X kuna msikiti na sio mbali na spot Y? Au unachotaka kusema ni kwamba hapatatokea wa kujenga ukumbi spot Z simply because yupo jirani na X & Y?nimeelewa point yako lakini usijenge hoja kwa kutunga hadithi.Labda tutajie hilo eneo ambalo lina mambo yote hayo kwa uuwiano huo tuthibitishe.Nijuavyo mimi,unapoenda kuomba kibali cha eneo uweke msikiti au kanisa basi huwa au ukumbi wa kwa ajili ya dance na maharusi basi lazima wahusika wafanye tathmini ya eneo husika na hii ni pamoja na kuangalia ujirani wa misikiti na makanisa ili kuzuia muingiliano.
Cha msingi wakiamua kuzuia hizi kelele wapige marufuku kabisa vipaza sauti,iwe asubuhi,mchana au hata usiku.
Inawezekana sio mkazi wa Dar es salaam na kama ni mkazi basi jiji hulifahamu vizuri vingenevyo wala usingetaka ushahidi!!