Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa

Makanisa ya kilokoke kudhibitiwa

Nakubaliana na wewe mkuu, kwa sisi waislam ipo clear kabisa kwenye Quran, tunaambiwa mnaosimama kwa ajili ya sala msisali kwa sauti ya juu bali msali kwa sauti ya katikati, hii inamaanisha sauti ya kawaida ambayo kama ni shekh anaongoza ibada niwaumini tu wa ndani ndio wanaopaswa kusikia. Lakini watu wameacha mafundisho wa Quran wanafata tu hisia na mkumbo.
Hata Biblia inakwambia "Nanyi mkiwa katika kusali,msipayuke payuke kama watu wa mataifa..Maana wao wanadhani kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi"
 
Wakristo wanakesha wanapigia watu kelele , bar za mtaani zinakesha nA mziki zinapigia watu kelele, waislam tunaamshana Usiku kuswali tuna amsha na wasio usika ... Haya mambo yote ya angaliwe kwa upana lasiivyo italeta hali yA uonezi
 
Hili suala liamuliwe kwa hekima,ukizuia watu wasipaze sauti kumuabudu Mungu wao huko ni kuingilia uhuru wa mtu kuabudu dini na imani aitakayo.Waende wapi kufanya ibada zao ambako hakuna watu wa kuona kero?
Wapi imeandikwa watu wa sali kwa makelele bila kujali wagonjwa,watoto wadogo na watu wengine wanaothirika na kelele hizo?
 
Siku wakiitaka roho yako uwaambie tuheshimiane una mambo yako mengi
kina sheikhe au kina nani? Mkuu wanaohitaji kulisikia hilo somo la mungu huja wenyewe humo kanisani au msikitini mwako sisi ambao hatuhitaji tunakuwa na hamsini zetu.sasa kwanini mtulazimishe kuwasikiliza wakati hatuhitaji? Halafu huu niaina ya ubakaji pia viongozi wa serikali mliangalie hili tunabakwa uhuru wetu.
 
Mwisho kabisa wa zoezi hili zitangazwe nafasi za kazi kuziba hizo hewa,kuna watu wa kuziba hewa.
 
Hawajasema eti kwa sabbu ya vipaza sauti ...kikubwa ni kwamba wanapiga muziki na kuimba mpaka asubuhi na kwa mdundo mkubwa kama vile uko ktk ukmbi wa burudani sasa vipaza sauti havina kero kwakuwa hutumika kwa muda mfupi na kwa sauti ndogo ukilinganisha na muziki ...acha ushabiki wa kidini...kama usha pata kero ya vigodoro ni sawa na muziki huo unakera hata kwa waumini wengine wanaotaka kulala..
 
Hili suala liamuliwe kwa hekima,ukizuia watu wasipaze sauti kumuabudu Mungu wao huko ni kuingilia uhuru wa mtu kuabudu dini na imani aitakayo.Waende wapi kufanya ibada zao ambako hakuna watu wa kuona kero?
 
Hili suala liamuliwe kwa hekima,ukizuia watu wasipaze sauti kumuabudu Mungu wao huko ni kuingilia uhuru wa mtu kuabudu dini na imani aitakayo.Waende wapi kufanya ibada zao ambako hakuna watu wa kuona kero?
 
kufa utakufa tu mkuu,hata uimbe mapambio mwaka mzima,hakuna haja ya kuhofia kitu ambacho lazima kitakupata
kuishi ni KRISTO na kufa ni faida........we unakufa huku umefungwa kamba baada ya kuweweseka sana kutokana na dhambi zako,......
kuishi ktk Kristo ni faida nakuwa na hakika nafsi inapopokelewa na malaika baada ya kutoka ktk dhiki na kejeli za dunia hii..
we unakufaje.?????
 
Bibli yenyewe inasema tiini mamlaka zilizo wekwa maana,mamlaka zote zatoka kwa Mungu....
usitafsiri biblia kinyume....unakuwa agent wa ibilisi bila kujielewa,...
tutii mamlaka kwa mambo ya kidunia,.huwezi kuniambia nitii mamlaka kwa kuabudu sanamu ndugu.hiyo haipo
siwezi kutii mamlaka kwakwa kunipangia muda wa kumtafuta Mungu wangu na kuongea nae...
siwez kutii mamlaka eti unicontrol nisimsifu MUNGU na nikimsifu Mungu niwe controlled na sheria....
kamwe haitotokea...nitamsifu MUNGU na neno la MUNGU litahubiliwa na mtasikia tu neno lake mtake msitake....
ni bora kufungwa/kufa nikililitetea na kulipigania jina la BWANA YESU
 
Nakumbuka niliwahi kuleta mada kuhusu nyumba za ibada kufungu vipaza sauti na kusababisha kero kwa wakazi wanaoishi jirani na nyumba hizo na wengi tulitaka vipaza sauti hivi vidhibitiwe kuondoa kero ya kelele

Leo gazeti la Uhuru linaongozwa na habari inayosomeka: "Makanisa ya Kilokole kudhibitiwa mitaani",ni kwa kuimba wakati wa usiku.Hili ni tamko la Mkuu wa Mkoa wa Arusha

Tunaishauri serikali zoezi hili liwe kwa nchi nzima na liisiishie kwenye Makanisa tu bali hata Misikiti ambayo nayo inayofunga vipaza sauti kwa nje na kusabisha kero ya kelele kwa wanaoishi jirani na Misikiti hiyo wakati wa ibada.

20160408_043802.jpg
Angalau.Biblia inasema 1 Korintho 10:31_33 Ikiwa nakula nikiwa na shukrani, kwa nini nitukanwe juu ya kile ninachotolea shukrani?Kwa hiyo, kama mnakula au mnakunywa au mnafanya jambo lingine lolote, fanyeni mambo yote kwa utukufu wa Mungu. Epukeni kuwa vikwazo kwa Wayahudi na vilevile kwa Wagiriki na kwa kutaniko la Mungu, kama vile mimi ninavyowapendeza watu wote katika mambo yote, bila kutafuta faida yangu mwenyewe bali ile ya walio wengi, ili wapate kuokolewa.
 
ATAKUTANA NA MUNGU HUYO COZ ANAGUSA JICHO LA MUNGU MUDA SI MLEFU ATAKUTANA NA MUNGU MWENYE KWANI MUNGU UJIPIGANIA IVYO AWEZI KUWAKOMESHA WATU WAKE
 
Itungwe Sheria Kuzingatia Muda, Ikifika Saa1 Usiku Au Muda Fulan, No Kipazasauti Kwa Dini Zote, Hii Itasaidia.

Au Kila Dini Itaje Siku Yao Ya Kuabudu Kisha Wapewe Nafasi Ya Kuweka Maspika Yao Lakn Mwisho Sa1 Usiku.

Wakifanya Hivi Tutazoea Tu Lakn Iwe Kwa Dini Zote Na Si1 Tu.
 
mathayo 24;14
tena habari njema ya ufalme itahubiliwa katika ulimwengu wote,kuwa ushuhuda kwa mataifa yote,hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
.injili itahubiliwa tu na kweli mtaambiwa ili mumjue YESU.
Stephano alipigwa mawe kisa neno la MUNGU,..hata tukienda gerezani its ok maadamu ntamuabudu MUNGU wangu ktk roho na kweli....hata wanifunge
sitaacha kulilitea jina la YESU.......
shetani anatafuta kubana neno la MUNGU lisiwafikie watu....neno litahubiliwa tu yani
mtake msitake
 
Mtawala yoyote duniani anaeanzaga kupambana na imani za watu huwa anashindwa vibaya sana! Hivi ili uonekane unafanya kazi lzm uanze kushughulika na walokole au waislamu!!??? Misikiti au makanisa???? Hivi ni vyombo vyenye utawala wake watu hawajui tu! Huu ni utamaduni wetu na hauwazuii watu kuendelea na shughuli za uzalishaji eti kwasababu ya kelele za usiku! Kisa nini kutetea usingizi au?? Kwa vi nchi vidogo kama cha kwetu ndio tunabaki kujadili vihoja vinyonge kama hivi!!! Mambo ya dini haya tuwaachie wazungu ndio wanatorelance na ustaarabu wa kuvumiliana sisi haya hatuyawezi! Jirani akila dagaa tu kero kwa jirani yake sembuse kelele za makanisa hii itakuwa chokochoko kubwa!!!tuiacheeeee!
 
Hapa mtaani kwetu tunajitahidi tu kuwavumilia lakini asiwaambie mtu-- kama issue ni kelele basi ni bora uishi jirani na baa kuliko makanisa ya Walokole! Hapa kwetu kwa mfano... kila wiki wanakesha cku tatu... cna haja ya kuwakumbusha sauti za vinanda vyao! Ikifika Jumapili, ni kuanzia asubuhi hadi jioni-- yaani kitu kinachoitwa kupumzika weekend hakipo kabisa! Narudia, bora uishi jirani na baa!
Hahahaaaaa mzee hatarii
 
Back
Top Bottom