Makamu wa Kwanza wa Rais azua balaa CCM

Makamu wa Kwanza wa Rais azua balaa CCM

GHIBUU

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
4,432
Reaction score
3,016
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AZUA BALAA CCM

Na Jabir Idrissa, Zanzibar

WAKATI wananchi hawajui hasa kinachojadiliwa kwenye vikao vya viongozi wakubwa waki wemo wastaafu Zanzibar, kuna fununu kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuna mvutano wa nani atashika wadhifa wa makamu wa kwanza wa rais wa kushiriki Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayoundwa na Maalim Seif mara akishatangazwa mshindi wa uchaguzi uliokwisha.

Taarifa kutoka ndani ya serikali, chama hicho zimesema kwamba inaonekana jina la Balozi Seif Ali Iddi ni kama halipendezi kwa pande zote mbili? upande wa chama alicho cha CCM, na upande wa Maalim Seif ambaye yumo katika kupigania haki yake ya kuongoza Zanzibar kwa kuwa ametoa takwimu zilizothibitishwa ndani ya Tume ya Uchaguzi kuwa zimempa ushindi wa urais kufuatia kura zilizopigwa Oktoba 25, mwaka huu.

Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amegombea wadhifa huo mara ya tano mfululizo, safari hii akiwa amefanikiwa kukusanya ushahidi wa wazi kuwa amechaguliwa na wananchi kwa zaidi ya asilimia 53.

Gazeti hili limefahamishwa na vyanzo vyake kwamba CCM baada ya kusalimu amri kuhusu kudai kuwa kimehujumiwa lakini kikipaisha malalamiko yake kinyume na utaratibu wa kisheria, viongozi wake wanahangaika kupata mtu atakayeshika umakamu wa kwanza, ule ambao Maalim Seif amemaliza kuutumikia kwa miaka mitano hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, ambayo mabadiliko yake ya mwaka 2010, ndiyo yaliyozaa utaratibu wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ikiongozwa na Rais na kusaidiwa na makamu wawili, mmoja kutoka chama kinachoibuka cha pili katika matokeo ya uchaguzi, safari hii itahitajika CCM ndio wateue makamu wa kwanza.

Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 39(1), inasema? Kutakuwa na makamu wawili wa rais ambao watajulikana kama makamu wa kwanza wa rais na makamu wapili wa rais. Kifungu cha 3 inaelezwa, ?Makamu wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa rais.?

Kama Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambayo Mwenyekiti wake Jecha Salim Jecha, alitoa taarifa Oktoba 28 ya kufuta uchaguzi mzima, itarudi kazini na kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya kura za urais za majimbo
 
1447735765033.jpg
 
Attachments

  • 1447735780784.jpg
    1447735780784.jpg
    55.2 KB · Views: 3,281
Nimemsikia mama Samia Suluhu akisema watanzania tuiombee hali ya Kisiasa huko Zanzibar ambayo wao ndio wameisababisha.
 
Maigizo maigizo, mwisho wa yote uchaguzi utarudiwa tu, nadhani mnapima upepo,
Matokeo yatenguliwe Halafu yatangazwe tena, nchi hizi kuja kukaa sawa ni mpaka katiba zote zibadilishwe, lakini kwa katiba hizi Hapo maalim seif aendelee kujitamanisha urais tu
 
Hujaweka jina la gazeti, na huo ni uongo,wenye nchi yao wameshaamua lazima uchaguzi urudiwe na ccm watangazwe washindi hata wakipata kura mia kati ya laki tano,nachoka kabisa na hii nchi.
 
Maalim Seif mwaka wa Ishirini 1995-2015 anapata 48% ikiongezeka 49.9%, hahahahah!! Jabir Idrissa anaota Urais wa Maalim
 
Jabir Idrissa ni cuf kindaki ndaki kiasi cha kuweka pembeni maadili ya uandishi.uchaguzi wa marudio ni february 2016,sasa huo mjadala wa makamu wa kwanza unatoka wapi
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.
 
Nimemsikia mama Samia Suluhu akisema watanzania tuiombee hali ya Kisiasa huko Zanzibar ambayo wao ndio wameisababisha.
Jinga moto muwashe nyie na kuwaomba wengi kuzima mtajijua wenyewe sisi Watanganyika poa tu,
 
Usiwe na akili ya ubinafsi jua ya kwamba amani ikitoweka Zanzibar hata Tanganyika haitakua salama
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Kwanini vurugu zitokee wakati wananchi watakuwa wamemchagua?
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

1447740982083.jpg
 
Attachments

  • 1447741006957.jpg
    1447741006957.jpg
    61.8 KB · Views: 1,328
Hujaweka jina la gazeti, na huo ni uongo,wenye nchi yao wameshaamua lazima uchaguzi urudiwe na ccm watangazwe washindi hata wakipata kura mia kati ya laki tano,nachoka kabisa na hii nchi.

Ungekuwa msomaji wa magazeti usingeshindwa kujua ni gazeti gani maana mwandishi wa hiyo habari katajwa "Jabir Idrisa"
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Hii akili mgando mpaka lini!? Kwa nini uamini kuwa kukishatangazwa serikali kuna watakao fanya fujo na sheria zikipuuzwa tu?
 
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AZUA BALAA CCM

Gazeti hili limefahamishwa na vyanzo vyake kwamba CCM baada ya kusalimu amri

Kama Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) itarudi kazini na kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya kura za urais za majimbo
Mkuu GHIBUU, hakuna ubaya kujipa matumaini kuwa Jecha anaweza kulamba matapishi yake!, lakini kujipa matumaini hewa, ni kuzidi tuu kujiumiza!.

Laiti ungezijua sababu halisi za kufutwa kwa matokeo hayo ya Zanzibar, usingeendelea kujipa matumaini hewa!.

Mimi niliwahi kuwaeleza humu lakini hamkuamini hadi yametokea!.

Maalim Seif ana siasa za jazba na chuki,

Maalim Seif anautaka urais wa Zanzibar kwa jazba, nguvu na usongo akiamini urais wa Zanzibar ni kama kitumbua chake alichopokwa kabla hakijaafika mdomoni ili hali ana njaa ya kufa mtu. Nadhani ni kweli siku zote anashinda uchaguzi Maalim ila nani atakubali kumpa urais mtu mshari mwenye kila dalili ya kulipiza kisasi na hata kuuvunja muungano hivyo hata akisimama mara mia hapewi dola ng'o labda adhikr ....

Tatizo jingine la Maalim Seeifu ni nasaba na sultan aliyepinduliwa,mpaka sasa mfadhili mkuu wa Maalim ni Sultan wa Brunei ndiye anayempa kiburi cha kuishi hotelini hapa bara kwa siku zote, sijui sasa. Sultani wa Brunei ni ukoo -ule ule wa Sultani wa Oman na ndio unaomgharimia Sultan wa mwisho aliyepinduliwa Zanzibar, Sultan Jamsed kuishi London mpaka sasa. Kwa vile Maalim ni ukoo huo, anahofiwa ataurudisha usultani na kuyakana mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyouwa ndugu zake na labda ndio maana jamaa ana hasira na usongo.

Tatizo kubwa la baadhi ya washabikiwa CUF ni mafanatik wa siasa za jino kwa jino huwaelezi kitu wao wanaangalia sura na sharubu sio uwezo wa mtu.
Natafakari tuu haya yanayotokea Zanzibar na hiki nilichoandika mwaka 2008!.

Pasco
Kwenye uzi huu

[h=3]Ni nini kinachosumbua Maalim Seif? - Page 11 -[/h]niliuliza hivi
Hili ni swali niliwahi kuuliza sikumbuki kujibiwa, kama ni kweli Maalim Seif huwa anashinda chaguzi za Zanziba lakini hapewi, nini kinachofanya asipewe?.

Hili ni swali tuu!.

Pasco
mr.London, niliuliza kama ni kweli kila siku huwa anashinda lakini hapewi,
  1. Kwa nini huwa hapewi?.
  2. Jee hizo sababu zinazofanya hapewi ni justifiable?.
  3. Kama ameshinda tena na safari hii, nini kitafanya apewe?!.
Pasco
Sikujibiwaga popote, ila kilichofanywa na Jecha ndilo jibu la swali hili!.

Pasco
 
Wabishane, wapindishane midomo ila mwisho wa siku wampe maalim seif haki yake.....hii ni kwa ustawi bora wa Zanzibar.
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Hivi wewe unaakili kweli??kwahiyo unataka kutuambia kuwa ccm ikiongoza ndio kutakuwa na amani??hivi mitanzania mijinga kama wewe unaishi ili nini?
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Vurugu atafanya nani? Waliochagua raisi wao ambao ni wengi sasa wanafurahia ushindi au mi mbwa koko ccm iliyosindwa? Naomba ujibu.
 
Back
Top Bottom