Makamu wa Kwanza wa Rais azua balaa CCM

Makamu wa Kwanza wa Rais azua balaa CCM

Mkuu GHIBUU, hakuna ubaya kujipa matumaini kuwa Jecha anaweza kulamba matapishi yake!, lakini kujipa matumaini hewa, ni kuzidi tuu kujiumiza!.

Laiti ungezijua sababu halisi za kufutwa kwa matokeo hayo ya Zanzibar, usingeendelea kujipa matumaini hewa!.

Mimi niliwahi kuwaeleza humu lakini hamkuamini hadi yametokea!.

Natafakari tuu haya yanayotokea Zanzibar na hiki nilichoandika mwaka 2008!.

Pasco
Kwenye uzi huu

[h=3]Ni nini kinachosumbua Maalim Seif? - Page 11 -[/h]niliuliza hivi
Sikujibiwaga popote, ila kilichofanywa na Jecha ndilo jibu la swali hili!.

Pasco

Wewe unatakaje?Wazanzibar wameamua,hilo tu latosha!
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Kama 1954 ni mwaka uliozaliwa basi ubongo wako inaelekea umeshachoka kazi. Yaani wananchi wamchague kiongozi halafu wewe useme akiongoza hali tete?!!

Kuiombea Zanzibar ili isiendelee kuhujumiwa na wanaong'ang'ania madaraka eti?
 
Hivi wewe unaakili kweli??kwahiyo unataka kutuambia kuwa ccm ikiongoza ndio kutakuwa na amani??hivi mitanzania mijinga kama wewe unaishi ili nini?

Usiwe na jazba katika kujenga hoja. Usikimbilie kusema fulani hana akili. CCM imengoza kwa muda mrefu, amani imekuwepo although relatively.
 
Matumaini ya Maalim seif yanaanza kutoweka polepole
 
Mkuu GHIBUU, hakuna ubaya kujipa matumaini kuwa Jecha anaweza kulamba matapishi yake!, lakini kujipa matumaini hewa, ni kuzidi tuu kujiumiza!.

Laiti ungezijua sababu halisi za kufutwa kwa matokeo hayo ya Zanzibar, usingeendelea kujipa matumaini hewa!.

Mimi niliwahi kuwaeleza humu lakini hamkuamini hadi yametokea!.

Natafakari tuu haya yanayotokea Zanzibar na hiki nilichoandika mwaka 2008!.

Pasco
Kwenye uzi huu

Ni nini kinachosumbua Maalim Seif? - Page 11 -

niliuliza hivi
Sikujibiwaga popote, ila kilichofanywa na Jecha ndilo jibu la swali hili!.

Pasco
Pasco, hii ni shida ya CCM zaidi ya Maalim Seif.

Mimi huwa najiuliza mara mia sipati jibu. Hivi chama kilichokaa madarakani miaka 50+, kina haja ya kurudi madarakani kwa kutumia MABANGO, WASANII, WIZI WA KURA, VITISHO VYA DOLA dhidi ya chama ambacho hakijawahi kupewa nafasi ya kuonesha machejo yake?

Maalim Seif awe mbaya au mzuri, sasa ni wakati wa kuapishwa. CCM walikuwa na nafasi ya kufuta upinzani Zanzibar, kwa kununua mioyo ya hao watu ambao ukiwazidisha mara 2 bado hawaijazi wilaya ya Temeke. Badala yake leo CCM inaanzisha fujo eti kwa kisingizio cha kulinda muungano (kwa mujibu wa bandiko lako). Hii si sawa, kama CCM ina nia ya kulinda amani, basi HAKI itangulizwe mbele. Vinginevyo sasa, serikali itakuwa inachafua amani kwa vitendo.
 
Last edited by a moderator:
Kama 1954 ni mwaka uliozaliwa basi ubongo wako inaelekea umeshachoka kazi. Yaani wananchi wamchague kiongozi halafu wewe useme akiongoza hali tete?!!

Kuiombea Zanzibar ili isiendelee kuhujumiwa na wanaong'ang'ania madaraka eti?

Hayo ni mawazo yako. Ukiweka ID ya 1860 haina maana ya kuwa umezaliwa mwaka 1860. Halafu, hivi maaiim alichaguliwa au kupata kura ngapi? Kule uchaguzi umefutwa baaada ya irregularities.
 
Usiwe na jazba katika kujenga hoja. Usikimbilie kusema fulani hana akili. CCM imengoza kwa muda mrefu, amani imekuwepo although relatively.

Hiyo amani unayosema unayo wewe au hao Wazanzibari? Maana nijuavyo mimi, amani hukaa moyoni mwa mtu, tulio nje ya huyo mtu tunaiona kwa utulivu wa dhati alionao huyo mtu. Je, Zanzibar ni tulivu?
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Una upunguvu ktk ubongo wako ila hujijui.muombe sana mungu upone huo ugonjwa.other wise siku moja sintoshangaa kukuta ukiokota mabaki ya vyakula majaani.shame on u.
 
- Eti umesema source ya hii habari yako nini mkuu? Sijaiona maana ni kujiridhisha tu ukweli wa habari yako au?

le Mutuz
 
Hayo ni mawazo yako. Ukiweka ID ya 1860 haina maana ya kuwa umezaliwa mwaka 1860. Halafu, hivi maaiim alichaguliwa au kupata kura ngapi? Kule uchaguzi umefutwa baaada ya irregularities.

Nilikuwa najaribu tu kudhani ni kwa nini una akili za kale ilhali 1954 si mbali sana. Hapa unaongelea irregularities za uchaguzi ukiwapuuza wa upande wa pili wanaoongelea irregularities za tume. Au unafikiri watu wote hawana akili kwa kuwa tu neno linalokupendeza wewe limesemwa na aliyeshika mpini?

Ni unafiki kuisemea amani ilhali unapuuza haki za watu wengine. Nchi hii wananchi wake ni watulivu, lkn wanachokozwa na mamlaka zinapokosa haki. Na unaposhangilia haki ya mtu mwingine ikivunjwa, fanya ukiacha akiba ya maneno, kuna kesho. Mimi si mpenzi wa CUF wala siasa zake, lkn HAKI ni msingi wa amani.
 
Na: Mwandishi Wetu

Kuna usemi katika hadithi kongwe za paukwa pakawa usemao ulimi uliponza kichwa. Kisa cha ulimi kuponza kichwa ni kwa ile tabia yake ya kusema kila kionwacho na macho. Ulimi ukasahau kuwa mambo mengine hayasemwi hadharani kwani wahenga husema, ?ukiona jambo, usiposema jambo, hufikwi na jambo!?

Makala yangu hii kimuktadha na kimantiki ni mpya lakini kimaudhui ni kongwe sana. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika kuhusiana na viteweji mbali mbali vinavyofanywa na viongozi wetu hapa nchini kwa kuonyesha jinsi walivyotumia madaraka yao kwa kuvaa joho la mungu la kibri na kufanya mambo yaliyowamaliza au kuwapa fedheha ya kiasi cha kupata maradhi ya kiharusi kwa aibu.

Niliwahi kuandika kuhusu kiburi cha Nyerere kusema angeuona uchaguzi wa mwaka 2000 mnamo mwaka 1998. Akaishia kufa mwaka uliofuata. Niliwahi kuandika kiburi cha Rashid Abdalla Mamba, aliponyanyua mkono akasema; ?ikiwa kuna Mungu nauonyoosha mkono wangu huu, naukunje!? Akaishia kufa kipande kipande kama nguru au ng?onda wa masika.

Niliwahi kuandika kuhusu Hassan Mandera na Uungu wake kule gereza la Bamkwe kiinua miguu. Vipi alikufa walioshuhudia hawatapata muda wa kuhadithia kamwe kwa sasa. Nikaandika ya tekeburi za Salmin Amour (Komandoo) na yaliyomkuta. Wote hawa na wengine wengi, waliponzwa na ndimi zao tu zaidi ya vile vitendo vyao vilivyokuwa vikishadidiwa na ndimi zao hizo ovu.

Makala yangu ya mwisho, ilikuwa kuhusu aliyekuwa Mwakilishi wa Magomeni Bwana Salmin Awadh na kauli zake alizozitoa punde tu kabla Mungu hajampatiliza na kumrudisha mbele ya haki bila hata kupata kutubia, bila shaka. Leo hii narudi tena barazani na mada ile ile lakini wahusika wangu wakuu leo ni Viongozi wakuu wawili wa Serikali iliyomaliza muda wake visiwani mwezi huu. Mmoja wa hao Ni Balozi Mkaazi Seifu Ali Iddi na kada mkongwe visiwani, Bi Asha Bakari Makame.

Kuna siku baba yangu aliwahi kuniambia kuwa binadamu ni sawa na ng?ombe tu. Hata akiona mwenziwe achinjwa mbele yake, haimjii ibra kuwa nguvu zake ni kubwa kuliko hata wale binadamu waliopo lakini hajui la kufanya. Hubakia pale pale naye muda ukifika akachinjwa.

Siku nyingi baada ya baba kusema haya, nilikuja kubaini kuwa Binadamu wengi wa leo, hawajifunzi kutokana na makosa. Na hii husababishwa na utamaduni wa ulimbukeni wa madaraka, tekeburi na jeuri ya pesa au uwezo wa kidola walio nao baadhi ya binadamu wenzetu.

Kikubwa walichonacho watu wa aina ya Balozi Idd na wenziwe niliotangulia kuwataja, ni kujifanya kuwa uongozi wao ni uteuzi wa Mungu. Isitoshe, kiburi chao hicho hakishii hapo tu, licha ya uteuzi huo, watu kama hawa hujiona kuwa wao na Mungu wana mawasiliano na mkataba wa moja kwa moja wa yale wayasemayo kiasi kwamba walisemalo lolote huwa ?maqbuul?- waaminivyo. Hivyo ndivyo akili zao zinavyowapa. Kumbe sivyo kamwe!

Balozi Seif Ali Idi, mmoja kati ya Viongozi wachache wa Serikali ya umoja wa kitaifa ambaye amechukiza sana sio kwa Upinzani tu, hata ndani ya chama chake na ndani ya Zanzibar kwa ujumla ni mfano wa hao. Tatizo nini? Kauli tu. Tunafahamu kuwa balozi Idi asingekuwa mwakilishi wa Kitope kama hakupata msukumo fulani.

Tunafahamu pia kuwa balozi licha ya maridhiano yaliyofikiwa nchini, yeye alikuwa kinara wa kuandaa hujuma na fujo za uvunjifu wa amani. Mwanzo alifanya siri. Kisha akaja juu shahiri. Tunatambua kuwa sehemu kubwa ya biashara na makampuni Unguja na Pemba ni ya Balozi Idi tangu apate Uongozi kwa matumizi ya pesa hizi hizi za walipa kodi anaowapiga vita na kuwakandamiza kila siku. Hatusemi. Tumemuacha tu na biashara zake.

Kilichwakera watu na hata Mungu kwa Balozi Iddi ni kauli zake kama nilivyosema. Kwa mfano, bila kujali kuwa yeye ni Muislamu na Zanzibar ni nchi yenye wasilamu wengi maradufu, alithubutu kusema jukwaani eti viongozi wa uamsho, ? wako gerezani wananyea ndooni!?

Hivi Balozi hakuona kuwa wale anaowadhihaki ni waume na baba za watu wa hapa Zanzibar ambapo pamempa kula na ujuba alio nao? Pia hajui kuwa masheikh wale wanaheshimiwa na kila Mzanzibari, awe CCM au CUF au chama chochote? Viongozi wale wa dini walikuwa wanatumikia wazanzibari wote na sio chama hata kimoja. Lakini kwa kiburi tu, hili hakuliona.

Matokeo yake, kama sio kutumika nguvu ya ziada, jimbo la Mahonda alikuwa hanalo kabisa. Hata hivyo hakupata nusura. Kayakosa majimbo mengi Unguja na Pemba hakuambulia lolote. Kisa na sababu? Kauli zake za dharau za kuwasimanga masheikh wa Umma wa Zanzibar, zilimgharimu yeye na chama chake. Hilo moja
Kauli ya pili, iliyotoka kinywani mwa balozi Seifu Idi, ni pale alipopandishwa jazba na vijana wasio na hekima, elimu wala Busara wa UVCCM akina Shaka na Sadifa walipotumia muda wao wote Jukwaani pale Kiembe samaki kumtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Ilipofika zamu ya Balozi Sefu Iddi, kwa utuzima wake wengi wetu tuliamini atakuja kutuliza jazba za vijana na atasema jambo lenye heshima. Lakini hakufanya hilo. Kiburi guo zito kwa kiumbe. Lakini kwa kuwa Balozi alilivaa, akaishia kumtukana Maalim Seif hadi akafikia kusema; ?kila siku unaibiwa wewe? Basi wewe -----!?

Hebu fikiria mtu mzima kama Balozi Seif, kudiriki kumuita mtu mzima mwenziwe ?bwege? mbele ya kadamnasi ya watu, hilo mnalionaje? Bila shaka mtakubali kuwa halijakaa vizuri eeh? Basi Mungu hana haraka. Kauli hii ya kumuita maalim Seif ----- kwa mwelekeo wa sasa unaompa Maalim Seif ushindi wa Urais Zanzibar, huku Balozi akidai wameibiwa kura, bila shaka iko haja naye aitwe; ?BWEGE!?
Aitwe ----- kwa sababu licha ya vifaru, majeshi, wagambo, KVZ, KMKM, Mazombie na laana nyengine za nguvu ya dola itumikayo kupora haki ya wananchi kila ufikapo uchaguzi, Balozi na chama chake wameishia kushindwa kwa kishindo. Hivi kweli na wao waitwe; ?MABWEGE hadaharani wataona raha?? Tatizo kauli tu!

Tukiachana na Balozi Idi, tumshike kidogo Bi Asha Bakari. Kada Mkongwe wa ASP na hatimaye CCM. Mwanamke ambaye licha ya kutokuwa na elimu kiivyo, amekuwamo Serikalini tangu enzi za Jumbe hadi 2010. Kapata si haba. Bi Asha Bakari, ni mzaliwa wa Pemba na alisoma shule au darasa moja na Maalim Seif kule Fidel CASTRO Pemba miaka ya 60.

Miaka si mingi, Bi Asha amerudi Makka kufuta mavumbi na kujitakasa mbele ya Mola wake ambaye licha ya yote aliyoyatenda, alifikia siku akajua kuwa Muumba yuko na hana budi kuabudiwa na kuombwa maghufira. Kurudi kwa Bi Asha Makka kulitupa wengi wetu matumaini kuwa sasa ametubu na atachunga sana kauli zake awapo jukwaani.

Wahenga walisema, ?taa haachi mwibawe!? Katika hatua ya kutisha na kutia huzuni ya jinamizi, Bi Asha alidiriki kuvaa madira ya CCM na kusimama jukwaani kule Gombani ya kale Chake Pemba huku akinyanyua kidole mbinguni akisema; ? Wallwahi, wallwahi, wallwahi, Namwambia ndugu yangu Seifu Sharifu, kashindwa kutawala 1995, hatawali tena maisha.?

Kauli hiyo aliyoitoa kwa wengi wetu tuliomsikia tulijiuliza maswali mengi. Mimi binafsi nilipata kujiuliza kimoyo moyo, kwa nini hasa Bi Asha aape kiasi kile kana kwamba yeye ni katibu muhtasi wa Mungu? Hivi ana uhakika gani kuwa hayo anayoyasema ndiyo Mungu aliyokwisha kuyaandika? Au Bi Asha amekuwa vile vimondo vinavyokwenda mbinguni kusikiliza siri? Hatukupata jibu mpaka uchaguzi wa juzi Oktoba 25.

Uchaguzi ambao ulituthibitishia wazi kuwa Bi Asha hakuwa mjumbe wa Mungu wala hakuwa katibu wake. Tulijuaje? Naam, tulijua tena kwa ushahidi bayana. Usiku wa siku ya uchaguzi kufikia alfajiri tu, tulishajua kuwa Chama cha CUF kimeshinda ushindi wa ajabu. Na kulikuwa na ushihidi safi kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndiye mshindi halali wa kiti cha Urais wa Zanzibar.

Panapo heri na majaliwa, muda mfupi ujao, inshaalwah, Maalim Seif anaweza kutangazwa kuwa Rais wa nane wa visiwa vya Zanzibar. Mungu jalia, kwa Baraka zako, iwe ni hivyo kweli, basi yapasa tujiulize Bi Asha na hali ile ya ugonjwa aliyonayo hivi sasa atakuwaje? Waswahili husema mtu mzima hasutwi, hasa akiwa mgonjwa kama alivyo Bi Asha Bakari hivi sasa ambapo afya yake ni ?unga kifuuni?.

Nionavyo, kwa kuwa binadamu hana uwezo mbele ya muumba wake, kuna haja kubwa ya kuchunga ndimi zetu. Kauli zetu. Kwani neno au kauli tu inaweza kubomoa taifa zima kama ilivyokuwa kule Iraq na Libya. Tusihadaliwe na madaraka tukafanya kiburi, tukumbuke mungu yuko na ana nguvu ya kutupatiliza kwa kauli zetu. Tutubu na tumtake mola wetu atufishe kifo chema! Tujifunze mema kwa waliopita. Amin.
 
Nilikuwa najaribu tu kudhani ni kwa nini una akili za kale ilhali 1954 si mbali sana. Hapa unaongelea irregularities za uchaguzi ukiwapuuza wa upande wa pili wanaoongelea irregularities za tume. Au unafikiri watu wote hawana akili kwa kuwa tu neno linalokupendeza wewe limesemwa na aliyeshika mpini?

Ni unafiki kuisemea amani ilhali unapuuza haki za watu wengine. Nchi hii wananchi wake ni watulivu, lkn wanachokozwa na mamlaka zinapokosa haki. Na unaposhangilia haki ya mtu mwingine ikivunjwa, fanya ukiacha akiba ya maneno, kuna kesho. Mimi si mpenzi wa CUF wala siasa zake, lkn HAKI ni msingi wa amani.

Thanks, Irregularites zinazongumzwa ni pamoja na hizo za ZEC. Ni aibu kwa wajumbe wa ZEC kuchapana makonde wao kwa wao. It means they were not impartial. Professionalism was lackng.
 
1447754738932.jpg
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

Kwani CCM si mnao akina Hafidh Ali na Mitawi kwa hio ngoma droo au sio?
 
Jabir Idrisa anafaamika msimamo wake tangu alipokuwa gazeti la UHURU. Ukweli wa mambo Maalim Seif hawezi kuwa Rais wa Zanzibar. CUF wenyewe wanajua kuwa Maalim akiwa Rais vurugu kubwa itatokea Zanzibar na kumfanya Maalim Seif asiongoze hata kwa siku mbili. Hali ya Zanzibar ni tete. Watanzania wote wazalendo ni lazima waendelee kuiombea Zanzibar.

mawazo ya kijinga,kutoka kwa mjinga,suala hapa siyo maalim seif,suala hapa ni wananchi wamemchagua nani aongoze iwe maalim seif au yeyote ataongoza vizuri ikiwa amechaguliwa na wananchi.
 
Hii tabia ya kuendekeza MAOMBI yasiyo na tija kisa wanasababisha waroho wa madaraka mbona mnaiendekeza??? Yaani mijitu iamue kuhujumu uchaguzi na kushikilia matokeo then siye tukeshe tukiomba kwa upuuzi wao!!! Sali mwenyewe sala zenu za kinafiki hizo
 
mawazo ya kijinga,kutoka kwa mjinga,suala hapa siyo maalim seif,suala hapa ni wananchi wamemchagua nani aongoze iwe maalim seif au yeyote ataongoza vizuri ikiwa amechaguliwa na wananchi.

Let me tell you something my brother/sister. usikimbilie kusema Fulani mjinga ingawa for sure ujinga ideally siyo tusi. Ni muhimu uwe unaheshimu pia mawazo ya wengine. Siujui kama umewahi kusoma masuala ya politics na leadership. Sijui kama umeshawahi kusoma how Hitler came to power. Sijui kama umewahi kufanya utafiti wa historia ya Zanzibar na mapinduzi yake. Sijui kama uliwahi kufanya utafiti wa wapiga kura wa CCM na CUF huko Zanzibar ni akina nani. CCM ya Zanzibar ni tofauti na CCM ya Singida au Songea. CUF ya Zanzibar siyo CUF ya TEMEKE au MTWARA...
 
Hakuna vurugu yoyote ndg. Kama Upo ushahidi wa vurugu thibitisha la sivyo unachochea watu wafanye vurugu.
 
Back
Top Bottom