Mkuu nimekuelewa, labda niongeze kidogo kwamba hao wanaofuturisha wanaelewa maana ya kufuturisha? anayetakiwa kufutirishwa ni yule asiye na uwezo kabisa, unaalika mawaziri na majirani zao unasema umefuturisha wakati kwake kaacha futuru zaidi ya hiyo uliyomwalika. Msaidie yule asiye na uwezo pia usijitangaze kwamba leo nimemfuturisha fulani sasa wao wanaita na vyombo vya habari nini maana yake? kama kweli wanania hiyo wapelekewe watoto yatima , mbona majumba yanayolea watoto yatima yapo maana hao wanahitaji misaada zaidi ya hiyo tena shukurani zao ni faraja kwako. Mashekhe wajaribu kutoa elim hiyo maana inatumika vibaya.